Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

kweli bora tufungwe yani timu ye2 haijajiandaa kimashindano hata tukikolify kwa kubahatisha tataenda kuaibike tu kama bra7 bora tufungwe tusikolify tujipange vizuri ili tukienda twende kuwin ehhhhhhhhhhh
timu ye2 ikikolify tutapoteza ela bure kwa kushiriki na kutolewa kwa aibu bora tufungwe yani ntafurahiiiiii

Sasa bora iende wakapate uzoefu na motisha ya mashindano we unadhani maandalizi ya kiwango gani ndo yanatakiwa ili wafike uko?
 
Kinachotakiwa kufanyika ni kuwapeleka wachezaji wa under 17 kwenye football academic za timu kubwa za ulaya.

Kama barcelona,real Madrid ,manchester city au united,arsenal,Chalsea nk.wakajifunze mpira kwa miaka 3...nafikiri wakikomaa hakuna timu ya Afrika itakayotufunga kirahisi...

uwezo tunao kwa kutumia mashirika makubwa ya wawekezaji wawalipie Ada ya mafunzo hayo.Vinginevyo tutatwanga maji kwenye kinu mpaka mwisho wa dunia.
 
ahsante Future president tujipange,tutafika.

Habari yako Mheshimiwa Raisi.
Kuna siku moja niliwaza kama ningebahatika kuwa Raisi wa TFF ningefanyaje tuwe na timu Bora kama za wenzetu?

1:Nilifikirria namna ya kuita wataalamu waweze kutufanyia Tathmini ya kuanzisha Academy kwenye Kanda zetu za nchi hii.(Kanda ya kati, Pwani, kaskazini,Kusini,nyanda za juu kusini magharibi n.k) NIlifikiri tuwe walau na Academy Kumi hivi.

2.Baada ya Tathmini na Gharama zote kujulikana,Zoezi la pili lingekua Kufanya fund raising ya kuhakikisha tunapata fedha za kuanzisha hizo Academy na kuziendesha.Ingefanyika kwa wadau, makampuni serikali na wapenda soka na hata fifa wenyewe.Tuwaonyeshe mpango kazi wetu kwani wangeweza kutuchangia..

3.Tungeagiza wataalam wa Scouting, kutafuta vipaji kuanzia Vijijini,wilayani,mikoani hadi Kanda husika.Kwani huko ndiko kuliko na vipaji.Baada ya kupata hivyo vipaji tuseme,tumepata vijana 1000,Tungeanzisha ligi za michujo huko wanakotoka kisha tukapata idadi ya wale tunaowaahitaji kwenye Academy zetu za Kanda.

4.Tungewasajili vijana wetu Rasmi kwenye Academy na kuanza mafunzo Rasmi.Baada ya Muda kama wa Mwaka mmoja, Tungeanzisha mashindano rasmi ya hizi academy kuweza kuchuja na kupata Top cream,ambayo tungeiweka kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa.

Nadhani hapa tungepata timu nzuri kabisa ya Taifa, sio kama hii ya Simba na Yanga.Nakumbuka Zambia baada kupoteza wachezai wake kwenye ile ajali walifanya Scouting nchi nzima na kupata kikosi kipya ambacho baada ya muda ndio kimekuja kuchukua Kombe la Africa.
 
mungu tubariki stars ishindiliwe magoli mengi na itolewe kabisaa

Enzi za Mwalimu ukiisema vibaya Serikali ilikuwa lazima ujikute matatani. Nakumbuka huku kwetu Usukumani kuna jamaa walikunywa pombe wakawa wanaimba 'Nyerere toka njiani, na hata Kawawa toka njiani, Kambona ututawale!'. Pombe ilipoisha walijikuta wako gerezani Mhumbu.

Leo hii, watu wanakosa uzalendo kiasi hiki bado tunawachekelea, kama hatuwezi kuwafunga gerezani basi tuwalaani tu! Mods wanaweza kuwapiga ban hata ya dk. 90 tu za mchezo ili wasiendelee kuwakatisha tamaa wachezaji wetu.

Laana ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yake mwenye kukosa uzalendo kwa nchi yake na yule anayemsapoti katika ujinga huo.

CC. Invisible
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi yetu na TFF yetu yaani timu ya Taifa inacheza tena nyumbani halau TBC hawarushi inamaana vipindi vingine mnavyorusha watu wakikata utepe ni vizuri zaidi ya mpira?
Mmeniuzi sana acha niendelee kushabikia Brazil tu. Halafu mechi kama hii mnaweka kiingilio kikuuuubwa wakati Zimbabwe waliweka buku buku.
Kaeni na li timu lenu
 
Mkuu, kwa mfumo uliopo kuanzia tff hadi serikalini si rahisi mdau wa chini kunufaika ama kufurahia michezo ya Tanzania. Ngoja Bundesliga ianze tujipatie uhondo bila mawaa.
 
Ingekuwa kuna mkutano wa ccm hapo wangerusha live kuanzia saa tano asubuhi kuwavutia watu waende uwanjani, ila kuhusu mpira au chama pinzani kina mkutano wa hadhara sahau.
 
Hii nchi yetu na TFF yetu yaani timu ya Taifa inacheza tena nyumbani halau TBC hawarushi inamaana vipindi vingine mnavyorusha watu wakikata utepe ni vizuri zaidi ya mpira?
Mmeniuzi sana acha niendelee kushabikia Brazil tu. Halafu mechi kama hii mnaweka kiingilio kikuuuubwa wakati Zimbabwe waliweka buku buku.
Kaeni na li timu lenu
NIPE MATOKEO YA taifa staa na mamb
aas ya Msubiji
 
Kilicho bakia Ni kuwasusia mechi zao mpaka waelewe umuhimu WA kucheza kwa uzalendo, tukiendelea kwenda uwanjani wataona tunaunga mkono ujinga wao, tumechoka jamani kila siku aibu
 
sitoweza kuhuzuria uwanja wa taifa ikiwa timu ya taifa inacheza hata siku moja....niongee tu ukweli siwezi kuishangilia timu ya taifa Tanzania jamani hata iweje never..
 
Hii nchi yetu na TFF yetu yaani timu ya Taifa inacheza tena nyumbani halau TBC hawarushi inamaana vipindi vingine mnavyorusha watu wakikata utepe ni vizuri zaidi ya mpira?
Mmeniuzi sana acha niendelee kushabikia Brazil tu. Halafu mechi kama hii mnaweka kiingilio kikuuuubwa wakati Zimbabwe waliweka buku buku.
Kaeni na li timu lenu

Brazil hii hii ya 7:1? Au kuna nyingine?
kwa upande wa TBC shame on you, mmetuonesha mechi zinachezwa brazil lakini mechi ya taifa letu inayocheza Dar mnashindwa!!!!!
 
Brazil hii hii ya 7:1? Au kuna nyingine?
kwa upande wa TBC shame on you, mmetuonesha mechi zinachezwa brazil lakini mechi ya taifa letu inayocheza Dar mnashindwa!!!!!

Hadi sasa sijajua hii timu imetokaje na msumbiji, TBC mnatia aibu wapi uzalendo wenu, mlikuwa mnatangaza na kuonesha mpira hadi saa saba usiku leo mechi ya mapema tu mnashindwa kuonesha aibu yenu
 
Back
Top Bottom