Mimi naomba kutofautiana na mawazo ya baadhi ya wachangiaji hapa.
sawa.
Imani yangu ni kwamba, mradi huu hautaishia kutoa kadi tu, bali utaunda database ya waTanzania wote ambayo itawekewa kumbukumbu zote za mwenye kadi kadiri inavyowezekana. Kama ikifanyika hivyo, itakuwa na manufaa makubwa sana.
unafikiri gharama ya bilioni 200 ni realistic kufanya hayo yote?
Mimi naamini pia kuwa nchi yetu imechelewa sana kutoa vitambulisho vya Taifa kwa watanzania.
Mbona vitambulisho hivyo vipo tayari, vinaitwa Passport na tumekuwa tukivitoa tayari na hivi karibuni tuliweka vya kisasa zaidi. Kwanini tusitumie passport ambazo tayari zina unique number, features, na tayari vinatutambulisha. Kwanini kwa mfano, tusiwe na utaratibu wa dual ID... moja ni Pass cha pili ni kitambulisho cha mkazi kinachotolewa kila mkoa?
Mpango huu ukitumika vizuri, utasaidia kujua kwa urahisi zaidi rasilimali watu tuliyonayo nchini na hivyo kuitumia kwa manufaa zaidi. Ilivyo sasa, Taifa/Serikali haijui ina wataalamu wangapi katika sekta zote. Kutokujua huku kunasababisha waone urahisi kutumia wataalam kutoka nje na hivyo kuliingizia taifa gharama kubwa zaidi za kuwatunza na pia kunyima wananchi fursa ya kutumia vipaji vyao.
Nadhani hili linahusiana zaidi na utendaji na ufuatiliaji wa taratibu ambazo tayari tunazo kuliko kukosekana kwa vitambulisho.
Fikiria: Kila mtoto anayezaliwa anapewa cheti cha kuzaliwa! Cheti hicho kinasema huyo ni mtoto ni wa jinsi gani, wazazi wake ni nani, alizaliwa lini na wapi. kwanini Cheti hicho kisiwe ndiyo msingi wa utambulisho wa uraia? Kinachofanyika ni kutengeneza database inayounganisha taasisi zote za serikali na ofisi ya msajili wa uzazi na vifo?
Ninachoona na ambacho tunakifanya vizuri ni duplication of services! Je tukiwa na Smart ID, tutaendelea kuwa na Passport?
Zaidi ya hayo, ni rahisi zaidi kwa mtu mwenye kadi inayoaminika na yenye kumbukumbu za kutosha kuweza kufungua account Bank, kuomba mikopo Bank na kupata hati mbalimbali ikiwemo passport.
Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, zaidi ya kufungua akaunti na kupata mikopo hizo kadi atazitumia wapi zaidi. Ni lazima ziwe na mahali pa kutumiwa vinginevyo itakuwa kama inavyofanyika sasa, mtu anakadi ya fedha anachofanya ni kwenda kwenye ATM na kuchukua fedha taslimu kwenda dukani kununua kitu! and hence defeat the whole purpose! Ni vituo vingapi vya mafuta vinapokea kadi hizi za kibenki kulipia mafuta at POS?
Ulinzi na usalama wa Taifa utaimarika zaidi. Hivi sasa, sio rahisi kuweza kumtafuta na kumpata muhalifu bila ushirikiano wa karibu sana wa wananchi. Hivyo kazi za Polisi zinakuwa ngumu sana na watu wengi kubambikiwa kesi (either kwa Polisi kujua au kutojua). Masuala ya uraia kwa watu mbalimbali pia itakuwa rahisi kuyabaini kwa njia ya vitambulisho hivi.
Kuna suala la faragha hapa ambalo ni kubwa zaidi. Sitaki mtu mmoja awe na uwezo wa kujua benki yangu, taarifa zangu za afya, kazi yangu, n.k kwenye kikadi kimoja!
Hivyo, kwa kifupi, utendaji na ufuatiliaji wa mambo mbalimbali utakuwa wa rahisi zaidi. Gharama ya kadi moja kwa sasa ni wastani wa shilingi za kitanzania elfu tano na mia tano tu (TZS 5,500/-). Gharama hiyo ni ndogo kulinganisha na haki ya mtanzania kuwa na utambulisho huo.
Sijui umepata wapi figure hiyo, lakini let me assume for a second kwamba ni sahihi. Hii ina maana kuwa ni Tsh bilioni 220. Je gharama ya kuleta mitambo ya kusomea kadi hizo, kuandaa database, kuajiri wafanyakazi, kufanyia matengenezo, n.k inafikia kiasi gani?
Mimi ningependa kuwepo na vitambulisho vya Taifa haraka iwezekanavyo. Masuala ya kurubuniwa kwa mradi ni vyema yakaangaliwa kwa makini ili azma hiyo njema ifanikiwe kwa gharama iliyopangwa.
Tatizo ni kuwa, twaweza kuwa na vitambulisho vizuri vya raia bila kuwa ni lazima viwe hivi vya Smart Cards. Hivi kweli unaamini njia pekee na bora ni hiyo ya smart card? l