Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

toleola27.jpg
 
Attachments

Thanks wakuu kwa kazi nzuri ya kutengeneza hiki kijarida ambacho hutupatia Elimu ya uraia at Zero cost!

Cheers
 
Thanks wakuu kwa kazi nzuri ya kutengeneza hiki kijarida ambacho hutupatia Elimu ya uraia at Zero cost!

Cheers

tumetambua kuwa karibu vitu vyote ambavyo ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu (kama hewa, jua, maji, n.k) vinapatikana bure! na vile ambavyo havina umuhimu mkubwa katika maisha yake vinapatikana kwa gharama kubwa sana (kama Almasi na dhahabu!).

So, tunaamini fikra zilizohuru na zenye uwezo wa kuchambua na kupangua mambo zinaangukia kwenye kundi hilo la kwanza.

Thanks!
 
Huu mradi ukiangalia kwa kiundani zaidi faida zake ni ndogo sana ila hasara ni kubwa.Ni vizuri serikali ikatumia busara zake kuusitisha kwanza kama Mtanzania anashindwa kutunza card ya ya kupigia kura hiki kicard cha kura ataza kweli kukitunza? na inapaswa muda wote atembee nacho kama uthibitisho ni raia.
 
Sasa ni mwaka wa 47 tangu tupate uhuru. Katika muda wote huo harukuwa na vitambulisho vya uraia lakini hatukuwa na matatizo yoyote ya kutishia usalama wa Watanzania au uhuru wetu.

Shilingi bilioni 222 ni pesa nyingi sana kama baadhi ya pesa hizo zikielekezwa kwenye Kilimo, Elimu, hospitali zetu, upatikanaji wa maji safi basi tunaweza kuinua maisha ya Watanzania walio wengi na kuyaboresha pia.

Kutumia mapesa mengi kiasi hicho hakuongezi tija wala maendeleo yoyote kwa nchi yetu, bali ni mradi uliotengezwa na wakubwa ili wajipatie mapesa ya kujiandaa kwa uchaguzi wa 2010.

Zamani CCM ilikuwa inaendeshwa kwa ada toka kwa wanachama ambao siku hizi hawafanyi hivyo tena maana CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma bali ni chama cha mafisadi.

Na sasa hivi CCM hawana pesa hivyo lazima wauchangamkie mradi huo wa kifisadi na kuupitisha haraka haraka ili wajipatie mabilioni ya uchaguzi huo wa 2010.

Kigumu chama cha mafisadi....kigumu!
 
Huu mradi ukiangalia kwa kiundani zaidi faida zake ni ndogo sana ila hasara ni kubwa.Ni vizuri serikali ikatumia busara zake kuusitisha kwanza kama Mtanzania anashindwa kutunza card ya ya kupigia kura hiki kicard cha kura ataza kweli kukitunza? na inapaswa muda wote atembee nacho kama uthibitisho ni raia.

Na ukishapoteza ukitaka kukireplace hicho kicard cha uraia tutaambiwa gharama ya kufanya hivyo ni $100 au hata zaidi. Watanzania walio wengi ambao mlo mmoja tu wa siku unawapa shida jinsi ya kuupata, watakuwa na uwezo wa kulipia hiyo $100 au zaidi kureplace card ambayo haiwaongezei chochote katika maisha yao ya kila siku!!!?

Huu mradi unanuka ufisadi wa hali ya juu. Nakumbuka kauli ya Pesambili Mramba, "Hata majani tutakula lakini rada lazima inunuliwe." na matokeoa ya ununuzi wa rada hiyo Watanzania tunayajua. Sasa hapa naona pia kuna kauli hiyo, "Hata majani tutakula lakini mradi wa vitambulisho vya uraia lazima upitishwe."

Mungu inusuru Tanzania.
 
Unajua.. mradi wa minara ya benki kuu ulikuwa utumie kiasi cha kama dola milioni kama 200 hivi. Leo hii umevuka na kufikia milioni 369 hivi na bado haujaisha. Sasa kwanini watanzania wanafikiri kuwa mradi wa vitambulisho utatumia dola milioni 200 tu? Ni mradi gani mkubwa ambao umesimama kwenye makadirio yake?
 
Mimi naomba kutofautiana na mawazo ya baadhi ya wachangiaji hapa.

Imani yangu ni kwamba, mradi huu hautaishia kutoa kadi tu, bali utaunda database ya waTanzania wote ambayo itawekewa kumbukumbu zote za mwenye kadi kadiri inavyowezekana. Kama ikifanyika hivyo, itakuwa na manufaa makubwa sana.

Mimi naamini pia kuwa nchi yetu imechelewa sana kutoa vitambulisho vya Taifa kwa watanzania. Mpango huu ukitumika vizuri, utasaidia kujua kwa urahisi zaidi rasilimali watu tuliyonayo nchini na hivyo kuitumia kwa manufaa zaidi. Ilivyo sasa, Taifa/Serikali haijui ina wataalamu wangapi katika sekta zote. Kutokujua huku kunasababisha waone urahisi kutumia wataalam kutoka nje na hivyo kuliingizia taifa gharama kubwa zaidi za kuwatunza na pia kunyima wananchi fursa ya kutumia vipaji vyao.

Zaidi ya hayo, ni rahisi zaidi kwa mtu mwenye kadi inayoaminika na yenye kumbukumbu za kutosha kuweza kufungua account Bank, kuomba mikopo Bank na kupata hati mbalimbali ikiwemo passport.

Ulinzi na usalama wa Taifa utaimarika zaidi. Hivi sasa, sio rahisi kuweza kumtafuta na kumpata muhalifu bila ushirikiano wa karibu sana wa wananchi. Hivyo kazi za Polisi zinakuwa ngumu sana na watu wengi kubambikiwa kesi (either kwa Polisi kujua au kutojua). Masuala ya uraia kwa watu mbalimbali pia itakuwa rahisi kuyabaini kwa njia ya vitambulisho hivi.

Hivyo, kwa kifupi, utendaji na ufuatiliaji wa mambo mbalimbali utakuwa wa rahisi zaidi. Gharama ya kadi moja kwa sasa ni wastani wa shilingi za kitanzania elfu tano na mia tano tu (TZS 5,500/-). Gharama hiyo ni ndogo kulinganisha na haki ya mtanzania kuwa na utambulisho huo. Mimi ningependa kuwepo na vitambulisho vya Taifa haraka iwezekanavyo. Masuala ya kurubuniwa kwa mradi ni vyema yakaangaliwa kwa makini ili azma hiyo njema ifanikiwe kwa gharama iliyopangwa.
 
Asante MKJJ kwa kijaridi tukipendacho. Naomba matoleo yanayofuata neno "page" libadilishwe kuwa "ukurasa"
 
Mimi naomba kutofautiana na mawazo ya baadhi ya wachangiaji hapa.

sawa.
Imani yangu ni kwamba, mradi huu hautaishia kutoa kadi tu, bali utaunda database ya waTanzania wote ambayo itawekewa kumbukumbu zote za mwenye kadi kadiri inavyowezekana. Kama ikifanyika hivyo, itakuwa na manufaa makubwa sana.

unafikiri gharama ya bilioni 200 ni realistic kufanya hayo yote?

Mimi naamini pia kuwa nchi yetu imechelewa sana kutoa vitambulisho vya Taifa kwa watanzania.

Mbona vitambulisho hivyo vipo tayari, vinaitwa Passport na tumekuwa tukivitoa tayari na hivi karibuni tuliweka vya kisasa zaidi. Kwanini tusitumie passport ambazo tayari zina unique number, features, na tayari vinatutambulisha. Kwanini kwa mfano, tusiwe na utaratibu wa dual ID... moja ni Pass cha pili ni kitambulisho cha mkazi kinachotolewa kila mkoa?

Mpango huu ukitumika vizuri, utasaidia kujua kwa urahisi zaidi rasilimali watu tuliyonayo nchini na hivyo kuitumia kwa manufaa zaidi. Ilivyo sasa, Taifa/Serikali haijui ina wataalamu wangapi katika sekta zote. Kutokujua huku kunasababisha waone urahisi kutumia wataalam kutoka nje na hivyo kuliingizia taifa gharama kubwa zaidi za kuwatunza na pia kunyima wananchi fursa ya kutumia vipaji vyao.

Nadhani hili linahusiana zaidi na utendaji na ufuatiliaji wa taratibu ambazo tayari tunazo kuliko kukosekana kwa vitambulisho.

Fikiria: Kila mtoto anayezaliwa anapewa cheti cha kuzaliwa! Cheti hicho kinasema huyo ni mtoto ni wa jinsi gani, wazazi wake ni nani, alizaliwa lini na wapi. kwanini Cheti hicho kisiwe ndiyo msingi wa utambulisho wa uraia? Kinachofanyika ni kutengeneza database inayounganisha taasisi zote za serikali na ofisi ya msajili wa uzazi na vifo?

Ninachoona na ambacho tunakifanya vizuri ni duplication of services! Je tukiwa na Smart ID, tutaendelea kuwa na Passport?

Zaidi ya hayo, ni rahisi zaidi kwa mtu mwenye kadi inayoaminika na yenye kumbukumbu za kutosha kuweza kufungua account Bank, kuomba mikopo Bank na kupata hati mbalimbali ikiwemo passport.

Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, zaidi ya kufungua akaunti na kupata mikopo hizo kadi atazitumia wapi zaidi. Ni lazima ziwe na mahali pa kutumiwa vinginevyo itakuwa kama inavyofanyika sasa, mtu anakadi ya fedha anachofanya ni kwenda kwenye ATM na kuchukua fedha taslimu kwenda dukani kununua kitu! and hence defeat the whole purpose! Ni vituo vingapi vya mafuta vinapokea kadi hizi za kibenki kulipia mafuta at POS?

Ulinzi na usalama wa Taifa utaimarika zaidi. Hivi sasa, sio rahisi kuweza kumtafuta na kumpata muhalifu bila ushirikiano wa karibu sana wa wananchi. Hivyo kazi za Polisi zinakuwa ngumu sana na watu wengi kubambikiwa kesi (either kwa Polisi kujua au kutojua). Masuala ya uraia kwa watu mbalimbali pia itakuwa rahisi kuyabaini kwa njia ya vitambulisho hivi.

Kuna suala la faragha hapa ambalo ni kubwa zaidi. Sitaki mtu mmoja awe na uwezo wa kujua benki yangu, taarifa zangu za afya, kazi yangu, n.k kwenye kikadi kimoja!

Hivyo, kwa kifupi, utendaji na ufuatiliaji wa mambo mbalimbali utakuwa wa rahisi zaidi. Gharama ya kadi moja kwa sasa ni wastani wa shilingi za kitanzania elfu tano na mia tano tu (TZS 5,500/-). Gharama hiyo ni ndogo kulinganisha na haki ya mtanzania kuwa na utambulisho huo.

Sijui umepata wapi figure hiyo, lakini let me assume for a second kwamba ni sahihi. Hii ina maana kuwa ni Tsh bilioni 220. Je gharama ya kuleta mitambo ya kusomea kadi hizo, kuandaa database, kuajiri wafanyakazi, kufanyia matengenezo, n.k inafikia kiasi gani?

Mimi ningependa kuwepo na vitambulisho vya Taifa haraka iwezekanavyo. Masuala ya kurubuniwa kwa mradi ni vyema yakaangaliwa kwa makini ili azma hiyo njema ifanikiwe kwa gharama iliyopangwa.

Tatizo ni kuwa, twaweza kuwa na vitambulisho vizuri vya raia bila kuwa ni lazima viwe hivi vya Smart Cards. Hivi kweli unaamini njia pekee na bora ni hiyo ya smart card? l
 
Unajua.. mradi wa minara ya benki kuu ulikuwa utumie kiasi cha kama dola milioni kama 200 hivi. Leo hii umevuka na kufikia milioni 369 hivi na bado haujaisha. Sasa kwanini watanzania wanafikiri kuwa mradi wa vitambulisho utatumia dola milioni 200 tu? Ni mradi gani mkubwa ambao umesimama kwenye makadirio yake?

It doesn't matter mradi huu utatumia kiasi gani cha pesa c'mon Mwanakijiji be realistic kuwa na vitambulisho ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa tuache unazi hapa tusiwe tunapinga tu bila sababu kama tunavyojiuliza sisi kwa nini hatuna vitambulisho hadi sasa na watoto na wajukuu wetu wetu watatujudge kwa hilo...think twice.

SAHIBA.
 
Kuna faida nyingi sana na kuwa na mradi wa vitambulisho. Hivyo ubaya usiwe kwenye mradi wenyewe bali kwenye implementation.
 
Hivi kwani hivi vitambulisho ni lazima? Kipi cha muhimu hapa? Maji safi ya bomba kwa kila Mtanzania, umeme kila sehemu, au vitambulisho?
 
Na ukishapoteza ukitaka kukireplace hicho kicard cha uraia tutaambiwa gharama ya kufanya hivyo ni $100 au hata zaidi. Watanzania walio wengi ambao mlo mmoja tu wa siku unawapa shida jinsi ya kuupata, watakuwa na uwezo wa kulipia hiyo $100 au zaidi kureplace card ambayo haiwaongezei chochote katika maisha yao ya kila siku!!!?

Huu mradi unanuka ufisadi wa hali ya juu. Nakumbuka kauli ya Pesambili Mramba, "Hata majani tutakula lakini rada lazima inunuliwe." na matokeoa ya ununuzi wa rada hiyo Watanzania tunayajua. Sasa hapa naona pia kuna kauli hiyo, "Hata majani tutakula lakini mradi wa vitambulisho vya uraia lazima upitishwe."

Mungu inusuru Tanzania.

Bubu please don't let me judge you for this issue sijui unaishi katika ulimwengu gani just to have a negative vibe about this project,huu mradi wa vitambulisho utasaidia sana kukuza kipato cha taifa,nani kasema vitambulisho vitauzwa this is home of great thinkers let's represent jf and stop critisizing.

Si ajabu hawa jamaa huko walipo wanatembea na vipande vyao mfukoni, lakini hawataki nasi tuwe navyo ... kesho na kesho kutwa watakuja na vioja vingine vya "Taifa lisilotunza kumbukumbu za watu wake".

Majabu haya!!!
 
Hivi kwani hivi vitambulisho ni lazima? Kipi cha muhimu hapa? Maji safi ya bomba kwa kila Mtanzania, umeme kila sehemu, au vitambulisho?

Nyani you don't get it hivyo vyote ni muhimu vitambulisho vitasaidia kwenye kupunguza uhalifu,vitazidisha mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa sana,vitasaidia banking system/mikopo leo hadi baba yako awe na nyumba mjini kama hana umekwisha hata school loan hupati na hizi ni mfano tu wa faida zake.

SAHIBA.
 
It doesn't matter mradi huu utatumia kiasi gani cha pesa

This is what I call an extravagant mentality! It doesn't matter how much it gonna cost us, as long as we need it! So lets just spend it!
c'mon Mwanakijiji be realistic kuwa na vitambulisho ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa tuache unazi hapa tusiwe tunapinga tu bila sababu kama tunavyojiuliza sisi kwa nini hatuna vitambulisho hadi sasa na watoto na wajukuu wetu wetu watatujudge kwa hilo...think twice.

I usually don't get offended easily (almost not at all).. kuchukulia maneno yangu kuwa ni sawa na unazi ni jambo ambalo silichukuli kiurahisi kwani ni kulazimisha hoja kwa kutumia nguvu.

Sijasema mradi wa vitambulisho ni mbaya, na wala sijapinga dhana nzima ya vitambulisho lakini kuna vitu vya msingi zaidi kuliko kurukia vitambulisho vya Smart Card kwenye taifa ambalo milioni 32 wanaishi vijijini! Is the smart card the best, cost efficient and much needed solution to their problems?

My answer, not in a long shot!
 
Nyani you don't get it hivyo vyote ni muhimu vitambulisho vitasaidia kwenye kupunguza uhalifu,vitazidisha mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa sana,vitasaidia banking system/mikopo leo hadi baba yako awe na nyumba mjini kama hana umekwisha hata school loan hupati na hizi ni mfano tu wa faida zake.

SAHIBA.

Kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo maana hata kupima ulazima na umuhimu wa vipaumbele inakuwa shida.....aaaaghhh....

Eti vitapunguza uhalifu? What the...? Unataka kunambia kati ya Marekani na Tanzania ni ipi yenye uhalifu mwingi zaidi? Na ipi yenye mfumo bora wa ku wa trace raia wake? Na unazungumzia uhalifu gani? Udokozi? Ufisadi? Ujambazi? Utapeli? Mauaji ya Albino?

Vitazidisha mapato ya serikali? Hmmmm...really? How so?
 
Nyani you don't get it hivyo vyote ni muhimu vitambulisho vitasaidia kwenye kupunguza uhalifu,vitazidisha mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa sana,vitasaidia banking system/mikopo leo hadi baba yako awe na nyumba mjini kama hana umekwisha hata school loan hupati na hizi ni mfano tu wa faida zake.SWAHIBA.

Swahiba

Unataka kutuambia tukiwa na vitambulisho basi EPA wala Richmond hakuna!! na ujambazi utakwisha grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom