Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Thanks wakuu kwa kazi nzuri ya kutengeneza hiki kijarida ambacho hutupatia Elimu ya uraia at Zero cost!
Cheers
Huu mradi ukiangalia kwa kiundani zaidi faida zake ni ndogo sana ila hasara ni kubwa.Ni vizuri serikali ikatumia busara zake kuusitisha kwanza kama Mtanzania anashindwa kutunza card ya ya kupigia kura hiki kicard cha kura ataza kweli kukitunza? na inapaswa muda wote atembee nacho kama uthibitisho ni raia.
Mimi naomba kutofautiana na mawazo ya baadhi ya wachangiaji hapa.
Imani yangu ni kwamba, mradi huu hautaishia kutoa kadi tu, bali utaunda database ya waTanzania wote ambayo itawekewa kumbukumbu zote za mwenye kadi kadiri inavyowezekana. Kama ikifanyika hivyo, itakuwa na manufaa makubwa sana.
Mimi naamini pia kuwa nchi yetu imechelewa sana kutoa vitambulisho vya Taifa kwa watanzania.
Mpango huu ukitumika vizuri, utasaidia kujua kwa urahisi zaidi rasilimali watu tuliyonayo nchini na hivyo kuitumia kwa manufaa zaidi. Ilivyo sasa, Taifa/Serikali haijui ina wataalamu wangapi katika sekta zote. Kutokujua huku kunasababisha waone urahisi kutumia wataalam kutoka nje na hivyo kuliingizia taifa gharama kubwa zaidi za kuwatunza na pia kunyima wananchi fursa ya kutumia vipaji vyao.
Zaidi ya hayo, ni rahisi zaidi kwa mtu mwenye kadi inayoaminika na yenye kumbukumbu za kutosha kuweza kufungua account Bank, kuomba mikopo Bank na kupata hati mbalimbali ikiwemo passport.
Ulinzi na usalama wa Taifa utaimarika zaidi. Hivi sasa, sio rahisi kuweza kumtafuta na kumpata muhalifu bila ushirikiano wa karibu sana wa wananchi. Hivyo kazi za Polisi zinakuwa ngumu sana na watu wengi kubambikiwa kesi (either kwa Polisi kujua au kutojua). Masuala ya uraia kwa watu mbalimbali pia itakuwa rahisi kuyabaini kwa njia ya vitambulisho hivi.
Hivyo, kwa kifupi, utendaji na ufuatiliaji wa mambo mbalimbali utakuwa wa rahisi zaidi. Gharama ya kadi moja kwa sasa ni wastani wa shilingi za kitanzania elfu tano na mia tano tu (TZS 5,500/-). Gharama hiyo ni ndogo kulinganisha na haki ya mtanzania kuwa na utambulisho huo.
Mimi ningependa kuwepo na vitambulisho vya Taifa haraka iwezekanavyo. Masuala ya kurubuniwa kwa mradi ni vyema yakaangaliwa kwa makini ili azma hiyo njema ifanikiwe kwa gharama iliyopangwa.
Unajua.. mradi wa minara ya benki kuu ulikuwa utumie kiasi cha kama dola milioni kama 200 hivi. Leo hii umevuka na kufikia milioni 369 hivi na bado haujaisha. Sasa kwanini watanzania wanafikiri kuwa mradi wa vitambulisho utatumia dola milioni 200 tu? Ni mradi gani mkubwa ambao umesimama kwenye makadirio yake?
Na ukishapoteza ukitaka kukireplace hicho kicard cha uraia tutaambiwa gharama ya kufanya hivyo ni $100 au hata zaidi. Watanzania walio wengi ambao mlo mmoja tu wa siku unawapa shida jinsi ya kuupata, watakuwa na uwezo wa kulipia hiyo $100 au zaidi kureplace card ambayo haiwaongezei chochote katika maisha yao ya kila siku!!!?
Huu mradi unanuka ufisadi wa hali ya juu. Nakumbuka kauli ya Pesambili Mramba, "Hata majani tutakula lakini rada lazima inunuliwe." na matokeoa ya ununuzi wa rada hiyo Watanzania tunayajua. Sasa hapa naona pia kuna kauli hiyo, "Hata majani tutakula lakini mradi wa vitambulisho vya uraia lazima upitishwe."
Mungu inusuru Tanzania.
Bubu please don't let me judge you for this issue sijui unaishi katika ulimwengu gani just to have a negative vibe about this project,huu mradi wa vitambulisho utasaidia sana kukuza kipato cha taifa,nani kasema vitambulisho vitauzwa this is home of great thinkers let's represent jf and stop critisizing.
SAHIBA.
Hivi kwani hivi vitambulisho ni lazima? Kipi cha muhimu hapa? Maji safi ya bomba kwa kila Mtanzania, umeme kila sehemu, au vitambulisho?
It doesn't matter mradi huu utatumia kiasi gani cha pesa
c'mon Mwanakijiji be realistic kuwa na vitambulisho ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa tuache unazi hapa tusiwe tunapinga tu bila sababu kama tunavyojiuliza sisi kwa nini hatuna vitambulisho hadi sasa na watoto na wajukuu wetu wetu watatujudge kwa hilo...think twice.
Nyani you don't get it hivyo vyote ni muhimu vitambulisho vitasaidia kwenye kupunguza uhalifu,vitazidisha mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa sana,vitasaidia banking system/mikopo leo hadi baba yako awe na nyumba mjini kama hana umekwisha hata school loan hupati na hizi ni mfano tu wa faida zake.
SAHIBA.
Mwanakijiji be realistic kuwa na vitambulisho ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa
Nyani you don't get it hivyo vyote ni muhimu vitambulisho vitasaidia kwenye kupunguza uhalifu,vitazidisha mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa sana,vitasaidia banking system/mikopo leo hadi baba yako awe na nyumba mjini kama hana umekwisha hata school loan hupati na hizi ni mfano tu wa faida zake.SWAHIBA.