Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Mimi nadhani hii ni UDAKU.
Kuna uthibitisho gani kuwa Membe ana kampuni na anamtumia Mwikalo kama front man wake?, Ina maana Mwikalo akiamua kuwa na kampuni yake na ujuzi anao, asipewe kwasababu anamjua/kufahamina na Membe?!
Acheni wivu jamani!
Hata hiyo kampuni ya Gotham International amabyo inazungumziwa hapa na ambayo ina utaaalam wa kutosha sana na ambayo ilistahili kupata tenda hiyo ya feasibility study na consultancy
Mjadala huu ni mzuri lakini nasikitika kwamba umejikita zaidi katika mambo ambayo si tu kwamba hayan utafiti wa kina bali ni uongo mkubwa ambao umelenga tu kuchafua majina ya watu na ninaogopa hili linaweza kuharibu heshima ya JF ambayo inasifika kwa kuwa kisima cha mijadala ya kina nailiyojikita kwenye utafiti na ukweli.
Membe na Urais
Kwanza limekuwa ni jambo la kufikirika na hisia miongoni mwa watu kwamba Mheshimiwa huyu ana ambition ya Urais. Ushahidi pekee kama aweza kuita hivyo au link yake na Urais ni kuwa kwake Waziri wa Mambo ya Nje na mazoea ya kwamba wawili kati ya Marais wetu walishika nafasi hiyo kabla. Yeye mwenyewe hajawahi kutamka wala kuonyesha kwa namna yoyote kwamba anapanga kuwania nafasi hiyo. Lakini pia yeye mwenyewe ametamka wazi kwenye kipindi cha Hamza Kassongo (Channel 10) wiki mbili zilizopita kwamba hana nia hiyo na kwamba amefika kilele cha mafanikio au utumishi wake serikalini. kwa hiyo hofu au fikra za ambition hiyo sioni kama zina msingi wowote.
Vitambulisho
Kama mchangiaji mmoja alivyosema, mradi huu ulianza toka wakati wa awamu ya pili na ni kweli kwamba wizara inayohusika ni ile ya Mambo ya Ndani ambayo Membe alikwa Naibu Waziri kwa kipindi cha miezi isiyofika au kuzidi kumi. Inawezekana katika kipindi hicho cha utumishi wake hapo alipata kuhusika lakini nafikiri ni kwa kipindi kidogo sana ambacho kwa vyovyote vile hakikuwa cha mchakato wowote wa uteuzi wa Mkandarasi wa kusupply au hata kufanya feasibility study. Hata hiyo kampuni ya Gotham International amabyo inazungumziwa hapa na ambayo ina utaaalam wa kutosha sana na ambayo ilistahili kupata tenda hiyo ya feasibility study na consultancy ilipata tenda hiyo wakati wa utawala wa awamu ya tatu ambayo membe hakuwa mmoja wao zaidi ya kuwa mbunge kwa kipindi cha miaka mitano ya mwisho ya awamu hiyo. Kwa vyovyote vile Membe asingeweza (hata angetaka) kuwa na influence ya kufanikisha uteuzi wa kampuni hiyo.
Kampuni ya Mwikalo
Ni ukweli ulio wazi na ambao hata mtoa hoja wa kwanza anaujua ni kwamba Membe hana hisa wala uhusika katika kampuni yoyote achilia mbali hiyo inayotajwa ya Mwikalo ambayo hata hivyo haifahamiki na wala hatuna uhakika kama ipo. Kwa hiyo kwa maoni yangu kufahamiana na Mwikalo au yeyote mwenye uwaniaji au kampuni hakuwezi kumfanya Membe ahusike na kampuni hiyo. Kwa ujumla ni uzushi ulio wazi kusema kwamba kampuni ya Mwikalo au kampuni yoyote kama ipo ina uhusiano na Membe au kwamba yeye anahusika na suala la vitambulisho. Kinachoonekana hapa ni kujaribu kuchafua jina la mtu si kwa kile alichofanya bali kwa hofu ya kwamba ana ambition ya urais ambayo ni perceived and not real. UKWELI NI KWAMBA MEMBE HANA INTEREST NA KAMPUNI YOYOTE INAYOOMBA KUCHUKUA MRADI HUU!
Kutokulewana na Waziri Mkuu
Ni uongo ulio wazi na mweupe kwamba Membe haelewani na Waziri Mkuu au vinginevyo. Waziri Mkuu kama kiongozi wa Membe amekuwa na uhusiano mzuri na Membe na wote hao wanafanya kazi kwa karibu bila tatizo. mahusiano yao ya kikazi na kijamii yamekuwa mazuri na yameendelea kuimarika. Kinachojitokeza ni hila za watu kuwagombanisha au ku-create na kuchochea migongano kati yao ambayo wao kama watu wazima wamekuwa wakiipuuza. Sasa kama WM ana nia ya kugombea kiti kikubwa amabyo ni haki ya kila mmoja naye akiwemo, hiyo haiwezi kuwa sababu ya ugomvi wao.
NASHAURI WACHANGIAJI WA JF TUWE WAKWELI NA WATAFITI WA KINA. TULINDE HESHIMA YA FORUM KWA KUJA NA HOJA ZA UKWELI NA ZENYE USHAHIDI WA KUTOSHA.
Jamani hivi hiyo Tenda ilitangazwa kihalali? Je, adjudication yake ilikuwa transparent?
Kama haikuwa hivyo bunge ambalo limeanza kikao lilivalie njuga jambo hili. GT ana point na hawa wanaotetea hawafai kabisa kutetea maana kama kweli Membe hana ambition ya kuwa rais then hata huo uwaziri ajiuzulu, hii ndio mizoga ambayo hatuitaki katika serikali maana imefikia kikomo.
..JACK GOTHAM NI KWELI ALISHINDA TENDA YA VITAMBULISHO KAM CONULTANT TOKA MWAKA 2002.JACK NA MEMBE NI MARAFIKI WA MUDA MREFU SANA,NA WALA WAKATI JACK ANASHINDA HIO TENDA MEMBE HAKUWA SERIKALINI
MBOPAAAAAAA!!!! KARIBU MUHASHIMIWA ...JAPO ULIKUWA UKISOMA KWA PEMBENI....INAFURAHISHA UKIAMUA KUINGIA BINAFSI AU PROXY KUTETEA HOJA HAPA..WENZENU WA UPINZANI KAMA MUHASHIMIWA ZITTO,FREEMAN,JJ MNYIKA ..ETS WANAINGIA NA MAJINA HALISI....TUNGETOA CHANGAMOTO UPANDE WA PILI NAO MUANZE KUINGIA NA MAJINA HALISI....
POST YAKO YA KWANZA ULIYOTUMIA KUTETEA CREDIBILITY ...TUMEIONA ..NADHANI SISI HATUNA NENO NA LEGACY YAKO ILA HISTORIA NDIO ITAKUHUKUMU KAMA NI KWA UCHAPA KAZI AU SMOOTH OPERATOR ..THE TIME WILL TELL...ILA KWA UPANDE WA UTENDAJI KIKAZI UNAJITAHIDI....KUONDOA HIZO KASORO ZA KUWAFANYIA WENZIO POLITICAL SUICIDE BEHIND THE SCENE[ I MEAN WATU KAMA DR HASSY KITINE,SUMAYE,IDDI .,.NA WENGINE WANAJUA MAKALI YAKO...]..NA MCHANGO WAKO KWENYE KAMATI YA USHINDI NI MKUBWA ....
KARIBU!!
Kaka kawachafua wengi sana uliowataja ni wachache. anajifanya rais na mbili anamuona DR.Shein hana chake.
Fikiraduni uko wapi kwenye udaku? njaa itakuua kutetea kila jambo, namshukuru GT kutuletea mada ya Suzane Mungi kwenye hiyo picha namuona dada yako Suzane kikwapa kinatoka jasho mnunulie Deodrant.
Masatu nawe ni njaa au kujikomba?
kaka Mbopo njoo mheshimiwa au uko kenya kwenye mgogoro nimekumbuka utakuwa Bungeni?
karibu MBOPO
Membe ni miongoni mwa mawaziri wachache wachapazi na waadilifu sana ktk baraza zima la JK.
Hayo mnayo msingizia hana kabisa JF tusiji shushie hadhi kiasi hiki.
Binafsi namfahamu Bw Membe, kikubwa nilichokiona kwake ni umakini, uzalendo kwa nchi yake na mapenzi kwa watanzania kwa ujumla.
Kama Membe anawekwa ktk fungu la watu wasio waadilifu basi neno uadilifu halina maana.
Lunyungu.
Njaa ya Masatu hiyo hapo juu.au tuite kujikomba?
mshauri ndugu yako.
ya suzanne Mungi makubwa umenitisha basi hana mume ana Bushoke. jee huyo kijana aliyezaa nae kashindwa kumnunulia dawa ya kijasho cha kwapa?
..di Mtoto,
Huyu sindiye waliibandika picha yake kwenye magazeti (Daily News)kuwa "Armed and Dangerous" kitapeli - na kuwa hajaajiriwa wala hana mahusiano na ofisi ya rais au ni Jack mwingine, sasa inakuwaje mtu kama huyu ndiye mshauri mkuu wa mradi kama huu? Huoni kuwa kuna mushkeli au ndio yakale hayanuki?
JF kwa ku spin hivi r we serious tunaamini kuwa Waziri Membe aje kujibu udaku hapa JF? Haya endeleeni kuishi kwa matumaini tu...
....