Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

I smell someone to be at work here . Let me shut my mouth and watch .GT njoo u save ama upunguze hii kasi ila njoo na data sasa .Maana ngoma imepata wachezaji .
 
Ndg yangu Lunyungu,

wewe umenena.... unajua ni vizuri tukawa na uhakika na tuyasemayo, na hasa pale wanapohusishwa watu kwa majina yao hadharani. Heshima ya mtu haiuzwi sokoni au barabarani, hivyo tuheshimu wenzetu kama ambavyo nasi tungependa wao watuheshimu.

Watu wasitumie JF kama kijiwe cha "porojo" za hekaya ya abunuwasi. JF ina heshima ktk jamii. GT, tuletee jina la kampuni ya Mwikalo/Membe, na ukiweza tutajie jina la kampuni ya Lowassa inayoshindania mradi wa vitambulisho Tanzania.
 
Nadhani kuna mgogoro kdogo wa lugha hapa. Wewe unapotuma ujumbe unategemea kusomwa na wengi, na sio mtu mmoja. Suala hili linajadiliwa na watu wengi, sasa sidhani kama nitakuwa sahihi kujisemea mwenyewe tu. Hivi kuna tabu gani kwa mtoa hoja kutuletea majina ya hayo makampuni ya Lowassa na Membe/Mwikalo? Tatizo ni nini? Ni kweli alikuwa anataka kufichua ufisadi au alikuwa ana mambo yake na akataka kuyapitishia JF? Nasikia Mwikalo ametoa offer ya USD. 200 kwa mtu atakayemletea jina la kampuni yake hiyo, je mtoa hoja hazitamani hela hizo? Mbona kaingia "mitini" bila kutuaga? Hapa ndipo ninapokuwa na mashaka na usahihi wa taarifa zake hizo. Kama hana basi ajitokeze aseme tu kuwa naye alidanganywa, aombe radhi kwaMwikalo basi yaishe, huo ndio uungwana jamani

Sidhani kama GT kaingia mtini ila anasubiri Membe au Mwikalo waje kujieleza wenyewe na sio kutumia wasemaji wao ambao bado hawajajitambulisha!
 
wewe umenena.... unajua ni vizuri tukawa na uhakika na tuyasemayo, na hasa pale wanapohusishwa watu kwa majina yao hadharani. Heshima ya mtu haiuzwi sokoni au barabarani, hivyo tuheshimu wenzetu kama ambavyo nasi tungependa wao watuheshimu.

Watu wasitumie JF kama kijiwe cha "porojo" za hekaya ya abunuwasi. JF ina heshima ktk jamii. GT, tuletee jina la kampuni ya Mwikalo/Membe, na ukiweza tutajie jina la kampuni ya Lowassa inayoshindania mradi wa vitambulisho Tanzania.
__________________
Kinvaba

Bold, simple, Loud, and Clear! na ndiyo kumkoma nyani mpaka milima ya golani!
 
wewe umenena.... unajua ni vizuri tukawa na uhakika na tuyasemayo, na hasa pale wanapohusishwa watu kwa majina yao hadharani.

Heshima ya mtu haiuzwi sokoni au barabarani, hivyo tuheshimu wenzetu kama ambavyo nasi tungependa wao watuheshimu.

Watu wasitumie JF kama kijiwe cha "porojo" za hekaya ya abunuwasi. JF ina heshima ktk jamii. GT, tuletee jina la kampuni ya Mwikalo/Membe, na ukiweza tutajie jina la kampuni ya Lowassa inayoshindania mradi wa vitambulisho Tanzania.
__________________
Kinvaba

Nami ninasisitiza. Kama hamna data OMBA RADHI. Kama hutaki ACHA UMBEYA, UMBEYA SIO MZURI!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Field Marshall ES
Topic ifutwe tu, maana hata kuihamisha haifai, ni too shallow kwa heshima ya JF! ,

nilizania jina limebadilika kutoka kwa JAMBO furums kwenda kwenye JUNGU forums
....kulikoni
 
GT, unadhani itakuchukua muda gani kutuletea jina la kampuni ya Membe/Mwikalo, na ya Lowassa ambazo umezitaja kuwa zinagombania mradi wa vitambulisho Tanzania? Maana tumekaa mkao wa hamu kubwa kupata majina hayo ili tuanze kuyafanyia kazi kikamilifu.

USHAURI WA BURE: Kama ukiona kuwa taarifa uliyoitoa haikuwa sahihi, basi rudi na kuomba radhi usamehewe ili wakati mwingine ujao tuendelee kuheshimu hoja zako. Siku zote mwanadamu huwa anakosea, na nadhani si vibaya ukakiri kuwa ktk hili UMEKOSEA. Kwani ukijitokeza na kuomba radhi itakugharimu kiasi gani? Sema tukusaidie. Kama hukufanya hivyo utatuweka ktk hali ya mashaka makubwa ya kuziamini hoja zako.

JF isiharibu heshima yake ktk jamii kwani ina mchango mkubwa sana wa kufichua maovu yanayofanyika nyumbani, hivyo hatutawatendea haki wasomaji wengine kama habari zake zitakuwa zinatiliwa mashaka.
 
Habari njema hizo, lakini kwanini asitupe muda atakaotumia huko msituni? Tuna hamu kubwa ya kumsikia kiumbe huyo wa Mungu.

Kama tungejua ni msitu gani kaingia tungeweza kukadiria ni muda gani atachukua, lakini ni yeye ndio anayejua msitu huo, hivyo ni yeye mwenye wajibu wa kutuambia. Sidhani kama hili nalo ni tatizo kusema, au nalo atahitaji kuingia msituni kwanza? na kama hivyo ndivyo, basi nitaanza kuwa a mashaka na hoja za mwanadamu huyu.

Hoja zangu za mashaka zitazingaia mambo makubwa mawili, la kwanza nitafikiria kuwa uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo, na la pili nitafikiria kuwa yeye ni kibaraka wa "makuhani" fulani wa siasa za nyumbani. Wakati utakapofika kila hoja nitaichambua kwa kina, na nitawaachia wasomaji waamue.
 
Kinvaba kuna mahali umeguswa nini ? Mbona una moto sana.

Hakuna kufuta wala kuhamisha hili wanja la kusema .Mpeni muda GT atakuja na majibu badala ya wewe Kinvaba kuleta busara za kufuta maana nzima ya bandiko.

Kuna uopotoshwaji kwenda kwenye Urais lakini tender inasimama kama ilivyo wacha tumngoje ndiyo tabia ya JF na si kufuta na kudai samahani .Unataka kuombwa samahani sema kama wewe n Muhusika watu wajue .
 
Kinvaba kweli ana moto,

Ishu inaonyesha inataka kumtoa roho, mimi mbona sina evidence na wala siishiki bango???issue ngapi ziko ndani ya JF na kwingineko na zinaendelea kupewa nafasi bila kutoa hiyo evidence unayotaka?

Kwa ushauri, angalia nyuma ya nia ya kuweka national IDs. Ni tokea lini tunahitaji hivi vitu? Leo watanzania walioichagua hii serikali nadhani ukiwauliza wanataka nini, hilo la ID halitasikika kabisa.

Kwanini hawa viongozi wasitafute kutimiza matakwa na mahitaji ya wananchi kwanza? Mimi kwa kweli sihitaji hiyo ID, nataka barabara, hospitali, affordable education at all levels, maji safi, na umeme. Kama si Mwikalo/Membe/Lowassa mwenye kampuni, basi ni mmojawao kwenye serikali, haiwezekani ishu isio na kipaumbele ikashikiwa bango namna hiyo.

GT thanks for good info, JF sio mahakamani ili ulete evidence.....
 
"Hapa imeletwa hoja ya MEMBE na LOWASSA washindania mradi wa ID"

Ikasemwa kwamba Membe ana kampuni aliyoisajili Marekani na amemuweka Mwikalo kuiendesha. Mtoa hoja hakuitaja kampuni ya Lowassa, maana sidhani kama Lowassa angependa kushiriki kama Lowassa.

Halafu ikaonekana kuwa ktk mradi huo kuna dalili za ufisadi. Mtoa hoja hajatuambia ni ufisadi wa namna gani.

Mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji wakageuza somo halisi na kutupeleka kwenye kiny'ang'anyiro cha urais mwaka 2015.
Ningependa mtoa hoja akamilishe hoja yake ya msingi kwanza kabla hajavamia nyingine. Wakati anatuletea hoja yake ya msingi, niliamini kuwa ana majina ya hizo kampuni, na ndio maana ninamuomba azitamke kampuni hizo ili tuzichambue.

Nimelivalia njuga sula hili kwa sababu Rais Kikwete ametangaza rasmi azma yake ya kurudisha maadili ya viongozi. Mimi naungana nae moja kwa moja ktk hili kwani madahara ya kutokuwa na maadili ya viongozi wote tumeyaona.
 
Mimi nadhani suala la Muungwana uliacha kwanza, koz naona hofu yako nyingine ni kugeuza somo. Ukitaja matamshi ya Muungwana popote katika vitu vinavyotofautiana kiukweli utazua mjadala mwingine tena.

Kama unataka majina ya makampuni uwe na subira, mtoa hoja akiweza atalisaidia. Nimefurahi kuona umebadili kidogo maneno yako kwamba nia ni kuzichambua hizo kampuni, na sio kwa mtoa hoja kuthibitisha hoja yake.

Hapo kweli tutakuwa kwenye mjadala pamoja....
 
Unajua hata PM ni kati ya watu wanaopenda dili sana,kwa maana nyingine PM ni fisadi pia. Kiongozi anayetumia madaraka yake kuweza kupata kitu huyo siyo kiongozi anayetakiwa katika ahadi za TANU.

Ukimwangalia Membe, he appaers to be honest but is good in dirty games.
 
Ninajiweka pembeni kwa muda kidogo nikitoa muda kwa GT tuliyeambiwa ameenda msituni kutuletea majina ya kampuni za Membe/Mwikalo na Lowassa zinazoshindania mradi wa ID. Naogopa "mtindi mkali" kama aliomwagiwa ndugu yangu hivi karibuni.

GT, ukiona huko msituni kuna giza nene sana, rudi tu ndugu yangu urekebishe mambo tuendelee na mijadala mingine kwani mchango wako humu ni muhimu sana. Haya ni mambo ya kawaida tu, hata BUSH huwa anadanganywa. Usitokomee huko, huna kesi ya mauaji.

Ukikosa nauli ya kurudia tu-beep tukutumie, ila nakushauri usipoteze muda wako mwingi huko msituni, ktk hili "UMELIKOROGA", waliokuletea jungu hili si wema kwako, kuwa makini nao huenda wanataka kukuharibia sifa yako nzuri uliyoijenga kwa muda mrefu ktk JF.

Namalizia kwa kukukumbusha kuwa kuna aina mbili za uongo. Kuna uongo mdogo hufanywa na watu wadogo, madhara yake huwa yanakuwa madogo kwa sababu huyu mdogo anaweza kukemewa na akaacha. Uongo mkubwa hufanywa na watu wakubwa, madhara yake huwa yanakuwa makubwa (hasa kwa yule anayesingiziwa uongo huo) kwa sababu huyu mkubwa hana wa kumkemea.
 
"Hapa imeletwa hoja ya MEMBE na LOWASSA washindania mradi wa ID"

Ikasemwa kwamba Membe ana kampuni aliyoisajili Marekani na amemuweka Mwikalo kuiendesha. Mtoa hoja hakuitaja kampuni ya Lowassa, maana sidhani kama Lowassa angependa kushiriki kama Lowassa.

Halafu ikaonekana kuwa ktk mradi huo kuna dalili za ufisadi. Mtoa hoja hajatuambia ni ufisadi wa namna gani.

Mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji wakageuza somo halisi na kutupeleka kwenye kiny'ang'anyiro cha urais mwaka 2015.
Ningependa mtoa hoja akamilishe hoja yake ya msingi kwanza kabla hajavamia nyingine. Wakati anatuletea hoja yake ya msingi, niliamini kuwa ana majina ya hizo kampuni, na ndio maana ninamuomba azitamke kampuni hizo ili tuzichambue.

Nimelivalia njuga sula hili kwa sababu Rais Kikwete ametangaza rasmi azma yake ya kurudisha maadili ya viongozi. Mimi naungana nae moja kwa moja ktk hili kwani madahara ya kutokuwa na maadili ya viongozi wote tumeyaona.

Umelivalia njuga hili kwa sababu wewe ni mhusika na mtetezi wa mafisadi na wala sio kutetea maadili ya viongozi!
 
Back
Top Bottom