Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Ninajiweka pembeni kwa muda kidogo nikitoa muda kwa GT tuliyeambiwa ameenda msituni kutuletea majina ya kampuni za Membe/Mwikalo na Lowassa zinazoshindania mradi wa ID. Naogopa "mtindi mkali" kama aliomwagiwa ndugu yangu hivi karibuni.
GT, ukiona huko msituni kuna giza nene sana, rudi tu ndugu yangu urekebishe mambo tuendelee na mijadala mingine kwani mchango wako humu ni muhimu sana. Haya ni mambo ya kawaida tu, hata BUSH huwa anadanganywa. Usitokomee huko, huna kesi ya mauaji.
Ukikosa nauli ya kurudia tu-beep tukutumie, ila nakushauri usipoteze muda wako mwingi huko msituni, ktk hili "UMELIKOROGA", waliokuletea jungu hili si wema kwako, kuwa makini nao huenda wanataka kukuharibia sifa yako nzuri uliyoijenga kwa muda mrefu ktk JF.
Namalizia kwa kukukumbusha kuwa kuna aina mbili za uongo. Kuna uongo mdogo hufanywa na watu wadogo, madhara yake huwa yanakuwa madogo kwa sababu huyu mdogo anaweza kukemewa na akaacha. Uongo mkubwa hufanywa na watu wakubwa, madhara yake huwa yanakuwa makubwa (hasa kwa yule anayesingiziwa uongo huo) kwa sababu huyu mkubwa hana wa kumkemea.
Oh Come on!
GT juzi aliaga hapa (kabla hujasajili kwa hili jina) na kusema kuwa atakuwa bize for the next few days. Kwa sasa wakati akiwa bize tunaendelea kujadili kuhusika kwa membe kwenye mkataba wa Buzwagi na kuhusika kwa Lowasa kwenye richmonduli!