Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

are you kidding me? yaani haya ni makosa ya kwanza kuitwa makosa kwenye jamii yetu? Unakumbuka kesi ya Simbaulanga?



Kasheshe sheria lazima ifuatwe siyo kwa sababu ya convenience bali ni kwa sababu ni sheria. Vinginevyo tunahalalisha watu kujichukulia sheria mikononi mwao kwa sababu wanajua adhabu itakayotolewa ni ndogo. Tunaposema sheria ni msumeno maana tukubali inaweza kukata pande zote. Haiwezekani tukimbilie mahakamani pale tunapoona sheria iko upande wetu lakini pale ambapo haipo hatuendi.

Kutokwenda mahakamani kumedhihirisha jambo moja kuwa serikali haina kesi dhidi ya watu wa EPA. Kosa la kughushi ni kosa ambalo kuna watu wanasota leo lupango; na inajulikana kuwa Kagoda walighushi nyaraka na wakachotewa bilioni 40. Kwanini Kagoda hawakupelekwa mahakamani kwa kosa la kughushi? Serikali haitaki kwenda mahakamani kwa sababu ikienda ushahidi utawekwa wazi na watu watahojiwa hadharani, na majina yatatajwa!!!! Si kwa sababu inaogopwa kiwango cha adhabu.


Mimi nadhani tukubaliane hivi.

1. Serikali haendi mahakamani kwa kuwa haitaki kuanikwa.... (POSITIVE to THEM and NEGATIVE to MWANAKIJIJI and TEAM.

2. Mwanakijiji, Upinzani na wote wenye ajenda zao wanapenda Mambo yaende mahakamani ili waivue nguo Serikali... wapate pa kupatia kura!!! and NOT OTHERWISE... sio uzalendo... wala kupenda sheria zifuatwe.

3.Mwananchi kama mimi Mahakamani hakuna TIJA. Pesa zetu.--> Madawa ya Mifugo, Mbolea, TIB given money for agriculture financing.
 
Napenda kujua kama hotuba yake yote imewekwa hapa JF au nependekeza iwepo sehemu maalum iwepo ,ambapo kutakuwa na hotuba za viongozi wa wa Serikali tu.

Huko itakuwa rahisi kuzifuata na kuzisoma kwa kina, yaani kachumba hako kawe hakuna kujibu wala kureply,sijui nimeeleweka?
 
Kasheshe, mojawapo ya matatizo ya utumishi Tanzania ni haya ya kushindwa kuwa na utaratibu wa kumfukuza mtu at will. Kuna ajira ambazo watu waajiriwe at will akiamua kuacha ana acha bila gharama yoyote na mtu akiamua kumfukuza anamfukuza. Italeta discipline.

Huu woga ati ukimfukuza atakimbilia mahakamani ni woga usio na msingi; Sijapendekeza kitu ambacho hakiko kwenye sheria. Tunaposema kuwa mtu anafanya kazi at the pleasure of the president hata aende mahakamani hana kesi. Leo hii Kikwete akiamua kumtimua Waziri halafu Waziri aende mahakamani ati kaonewa?

Leo hii Rais akimfukuza mwandishi wake au mshauiri wake ambaye yeye amemteua na anafanya kazi at his pleasure akimfukuza huyo mshauri aende mahakamani? labda njozini. Rais asiye na nguvu au uwezo wa kisheria wa kumtimua mtu aliyempa ajira bila kuogopa mahakama ni Rais mvivu na dhaifu. Kama hana nguvu hizo angehakikisha anakuwa nazo. Na my argument ni kuwa anazo.

Angalia ibara hii hii ya Katiba:



Sasa utaona kuwa kuna nafasi ambazo Rais anaweza kuzijaza na nyingine ambazo zinajazwa na vyombo vingine; lakini katika yoyote yale kipengele cha 4 ni muhimu sana. Kuwa Rais hazuiwi na vipengele vya 2 na 3 kudhibiti nidhamu ya "watumishi na utumishi katika serikali ya Jamhuri ya Muungano".

Rudia tena rudia tena kusoma hicho kipengele ikibidi, ulizia wanasheria... nadhani hakina tafsiri uliyosema mheshimiwa mwandishi mwanakijiji!!!
 
Huyu bwana amekuja kuongelea Bungeni mambo ya ubabaishaji tunayoyasikia kila siku kutoka kwa mawaziri wake, afadhali hata angekwenda kuongelea sehemu nyingine. Ametuboa leo.

Nimekata tamaa sana tangu saa tisa alasiri ya leo, Namshukuru Mhe. Spika kwa kuwakilisha mawazo ya wengi waliokuwa wamechoka. Ni matumaini yangu kuwa mtu mzima huyu atakuwa amemwelewa, Vinginevyo, tumekwisha kabisa, uongozi wa nchi hatuna. Rais gani anawaogopa mafisadi?

Huyu kwa vile ameonekana si mmoja wetu lazima ni mmoja wao.Poleni watanzania wenzangu. Mungu atusaidie tufunuliwe akili zetu tuyaone haya na tuchukue hatua ya kuwatolea uvivu papo hapo kama alivyoanza spika leo.
 
Ufisadi wako unaweza kuanikwa huko. Who knows?

Kwi kwi kwi;

Mafisadi mbona ndio mtindo wa maisha wa waTanzania... mshahaa 200,000/- unamiliki magari... na unatumia petrol 300,000/- kwenda kazini ambapo panakupatia 200,000/-

Tatizo lenu ni kunyooshea vidole watu wachache sana... huu ndio mtindo... Muulize Mwenyekiti wa CHADEMA, UDP, NCCR-MAGEURI, TLP...

Heri yangu nakula kajasho kangu... kwa haki na amani.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Tatizo lenu ni kunyooshea vidole watu wachache sana... huu ndio mtindo... Muulize Mwenyekiti wa CHADEMA, UDP, NCCR-MAGEURI, TLP...

Kuna kitu kimevuta hisia zangu hapo. Niwaulize wenye viti wa vyama vya upinzani? CCM safi, au sio? Hapa kidogo nimemkumbuka Mwafrika wa kike aliwahi kusema wewe ni Kilitime. Ukakataa.

Mimi sitakuuliza kama wewe ni CCM unayefisadi nchi hii. Nahofia jibu alilolapata MWk. Yeye alikuumbua. Mimi nakutunzia heshma.
 
Mimi nadhani tukubaliane hivi.


Hatuwezi kukubaliana hivyo, kwa sababu kukubaliana na maoni na hoja dhaifu ni kujidhalilisha. Maoni dhaifu kama ya kwako hayaitaji kukubaliwa bali kupingwa moja kwa moja on the get go!.

1. Serikali haendi mahakamani kwa kuwa haitaki kuanikwa.... (POSITIVE to THEM and NEGATIVE to MWANAKIJIJI and TEAM.

Tatizo unafikiri ni negative kwangu, as a matter ni negative kwao na positive kwangu na kwa timu (as long as in that team Mwanyika, Hosea, na Mwema hawamo.. or anybody else picked by His Excellency).

2. Mwanakijiji, Upinzani na wote wenye ajenda zao wanapenda Mambo yaende mahakamani ili waivue nguo Serikali... wapate pa kupatia kura!!! and NOT OTHERWISE... sio uzalendo... wala kupenda sheria zifuatwe.

Wrong, nataka (sijui wengine) waende mahakamani ili waheshimu sheria na wasiigope. Nataka kutetea utawala wa sheria siyo utawala wa kisheria wa waoga wa sheria!


3.Mwananchi kama mimi Mahakamani hakuna TIJA. Pesa zetu.--> Madawa ya Mifugo, Mbolea, TIB given money for agriculture financing.

Watakuzuga wewe tu. Yaani kweli unaamini kuwa fedha hizo zitaingizwa kwenye kilimo? Utaweza vipi kutofauitisha fedha za EPA na fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya Kilimo?
 
Wananchi, viongozi wampongeza JK
Waandishi Wetu
Daily News; Friday,August 22, 2008 @00:03

Wananchi na viongozi mbalimbali wamempongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa hotuba yake iliyogusa maeneo mengi ambayo majibu yake yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi. Na kati ya hoja zilizowagusa wengi wa wakazi hao waliozungumza na gazeti hili jana ni suala la Muungano, ripoti ya EPA, masuala ya jinsia, tatizo la mafisadi, tatizo la migomo ya mara kwa mara, rushwa na tatizo la uchumi kwa ujumla wa Tanzania.

Kwa upande wa viongozi wa dini, wamemsifu Rais Kikwete kwa kutoa hotuba iliyokonga nyoyo za watu hasa wa maisha ya kati kwa kuzungumza wazi hali ya uchumi ilivyo na malengo ya baadaye. Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Method Kilaini alimshukuru Rais kwa kuzungumza masuala ya Muungano na sasa kinachohitajika ni kujenga nchi na siyo huyu wa kule na yule wa huku.

Kwa kweli mimi binafsi, silisemei Kanisa, ila binafsi nimeifurahia hotuba ya Rais na nina imani sasa kila Mtanzania ameelewa EPA ni nini na lengo la serikali kwa fedha hizo, hasa pale aliposema kwamba zitatumika kwa ajili ya kilimo, nadhani wakulima ni wahitaji zaidi nchini, alisema Askofu Kilaini. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF) Dk. Bohela Lunogela alipongeza hatua hiyo ya kuamuru fedha za EPA zipelekwe kwenye kilimo.

Amefanya vizuri kuzipeleka kwenye kilimo, hili ndilo eneo linalohitaji msukumo ingawa kiasi hiki cha bilioni 133 kinaweza kuonekana kikubwa, lakini hakitoshi kwa kilimo, alisema Dk. Lunogelo kwenye mahojiano na televisheni ya TBC1. Alisema pamoja na fedha hizo kupelekwa kwenye mfuko wa pembejeo, lakini tegemeo kubwa la wakulima ni kuboreshewa huduma za benki kwa ajili ya mikopo na maghala ya kutunzia vyakula.

Kwa upande wao, wanaharakati wa masuala ya jinsia akiwamo Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwakumbuka wanawake hasa kupitia ahadi yake ya kuongeza nafasi zao za uwakilishi bungeni aliyoitoa mwaka 2005.

Alisema wanachokitegemea sasa wanawake ni mchakato huo alioahidi Rais kuwa tayari kwa utekelezaji ifikapo 2010 na kwamba wanatarajia utangazwe na kutoa nafasi kwa wanawake watakaoleta mabadiliko bungeni na si uwezo wao kifedha. Naye mkazi wa Dar es Salaam, Abdul Msangi alisema anaamini kuwa hivi sasa mjadala wa Zanzibar ni nchi ama si nchi, utakuwa umefungwa rasmi kwa sababu Rais Kikwete ameshalizungumzia pamoja na kutoa ufafanuzi ndani ya Bunge.

Sasa tumepata picha halisi juu ya Muungano na wala hatuoni sababu ya Muungano huu kuvunjwa badala yake tushirikiane katika kurekebisha kasoro zilizopo ndani yake ili tusonge mbele, alisema. Rachel Raphael alimpongeza Kikwete kwa kutoa kauli juu ya mgomo wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao wanatarajia kugoma kuanzia Jumatatu.

Emmanuel Tatobi alimpongeza Rais kwa uamuzi wa kufilisi mali za mafisadi na kuongeza kuwa uamuzi huo ni ishara kuwa kweli fedha zilizochukuliwa na mafisadi hao zitarudishwa. Tatobi alisema uamuzi wa serikali wa kutowapeleka mahakamani mafisadi hao, kumeiwezesha serikali kuzipata fedha hizo ambazo labda zingeweza kupotea au kuchukua muda mrefu kuzipata kutokana na utaratibu wa Mahakama.
 
Bila hata kupata ushahidi wa mali zipi za mafisadi zilizofilisiwa na ziko wapi, bila hata kupata majina ya mafisadi waliorudisha pesa walizoiba na idadi iliyorudishwa na kila mmoja wa hao mafisadi na pesa hizo zimewekwa benki ipi.

Mpaka sasa hakuna yeyote serikalini au BoT anayejua kiasi gani kimerudishwa. Kuna wakati tuliambiwa shilingi 60 Bilioni, mara zikawa 53 bilioni sasa hivi hawajui lakini kama kawaida ya Wadanganyika ambao hawataki kuwa wachunguzi wa mambo kwa kina, wameshakurupuka na kutoa sifa kem kem kwa JK kwa kutoa 'hotuba nzuri' au labda gazeti la SIRI KALI liko kazini kufanya vitu vyake ili kumfagilia JK. Bado tuna safari ndefu sana!
 
Inatia aibu kuona Askofu mzima ambaye amesoma lakini anaongea pumba kupita kiasi, kweli hawa maaskofu uchwara hawatakiwi kabisa katika jamii yetu kwa sababu wanachojua ni kujipendekeza tu kwa viongozi wa serikali.
 
Walioiba mabilioni ya EPA wafilisiwa
Cassian Malima, Dodoma
Daily News; Friday,August 22, 2008 @00:01

Serikali imekamata mali zote za wamiliki wa kampuni 13 kati ya 22 zilizothibitika kuhusika na uchotaji wa mabilioni ya shilingi kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Rais Jakaya Kikwete aliliambia Bunge jana.

Alisema licha ya kuzuiwa hata kwa magari wanayomiliki watu hao, pasi zao za kusafiria pia zinashikiliwa wasikimbie nje ya nchi. Licha ya hatua hiyo, Rais Kikwete alisema ameiagiza Benki Kuu (BoT) kufunga akaunti hiyo ambayo kwa mujibu wake ina zaidi ya Sh bilioni 130 na fedha hizo ziwekwe katika mfuko mkuu wa serikali.

"Ikitokea mtu ajitokeze kudai (kutokana na EPA) tutamlipa," alisema Rais na kuiagiza serikali kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya dharura ya malipo kama hayo. Aliwasisitizia wananchi kufahamu kwamba fedha hizo si za umma, ni za watu wa nje ambao hawakupelekewa fedha zao.

Pia ameagiza kwamba fedha zitakapopelekwa serikalini baadhi zitumike kuongeza ruzuku ya mbolea na dawa za mifugo. Alisema fedha nyingine zitapelekwa katika Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) zitumike kutoa mikopo ya kilimo na kama sehemu ya mchakato wa kuanzisha benki ya kilimo.

Katika hotuba yake hiyo bungeni iliyoanza saa 6:17 mchana hadi saa 9:42 alasiri, Rais Kikwete alisema amekubali ombi la timu aliyoiunda Januari mwaka huu kuendelea kufuatilia kampuni hizo na kuziruhusu kuendelea kulipa fedha zilizochukuliwa hadi Oktoba 31, mwaka huu.

Timu hiyo inaongozwa na Mwanasheria Mkuu akishirikiana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). "Ifikapo Novemba mosi asiyelipa… mahakamani, tumewapa fursa ya kutosha," alisema. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, hadi timu aliyoiunda ilipowasilisha ripoti ya uchunguzi wao kwake Jumatatu wiki hii ilikuwa 'imewabana' watuhumiwa hao na kuweza kukusanya Sh bilioni 53.7.

Alisema kwa mujibu wa makubaliano na timu, wadaiwa wengine wanapaswa kulipa fedha zitakazofanya kiasi kilichokusanywa kufikia Sh bilioni 64 ifikapo Oktoba 31, mwaka huu. Rais Kikwete hakuzitaja kampuni ambazo wamiliki wake mali zao zimekamatwa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, Januari mwaka huu alizitaja kampuni hizo kuwa ni Bencon International, VB & Associates, Bina Resorts, Venus Hotel, Njake Hotel & Tours, Maltan Mining, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment, Ndovu Soaps, Navy Cut Tobacco, Changanyikeni Residential na Kagoda Agriculture Ltd.

Rais Kikwete alisema hatua kali zimechukuliwa dhidi ya kampuni hizo 13 baada ya kubainika kwamba zilichota Sh bilioni 90.3 kwa kutumia kumbukumbu, nyaraka na hati za kughushi. Juu ya kampuni tisa zilizosalia, Rais alisema zililipwa Sh bilioni 42.6 ambazo pia inaaminika hazikustahili kulipwa kwa sababu hazikuwa na nyaraka zilizoonyesha stahili za malipo hayo, lakini imekuwa vigumu kuhakiki malipo hayo kutokana na ukosefu wa nyaraka.

Rais alisema kamati yake inasubiri taarifa kutoka kwa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) na Polisi wa nchi ambazo Tanzania ina makubaliano ya kushirikiana nao ili kupata taarifa ya kampuni hizo tisa. Ingawa hakuzitaja, kumbukumbu zinaonyesha kampuni hizo ni G&T International, Excellent Services, Mibane Farm, Liquidity Service, Clayton Marketing, M/S Rashtas, Malegesi Law Chambers, Kiloloma and Brothers na Karnel Ltd.

Rais Kikwete alitumia zaidi ya nusu saa kuzungumzia suala hilo la EPA, akianza kwa kueleza historia nzima ya akaunti hiyo aliyosema iliundwa mwaka 1985 wakati taifa likiwa linakabiliwa na matatizo ya uchumi na ukosefu wa fedha za kigeni. Alisema awali akaunti hiyo ilikuwa ikitunzwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajlii ya kupokea fedha za malipo ya huduma na bidhaa ambazo wafanyabiashara wa Tanzania walikuwa wakinunua kutoka nje.

Kwa kuwa malipo hayo yalifanyika kwa shilingi ya Tanzania na baadaye kukawa na mlundikano kutokana na kutokuwa na fedha za kigeni, akaunti hiyo ilihamishiwa BoT na wakati fulani ilifikia kuwa na akiba ya Sh bilioni 600, alisema. Aliwaambia wabunge waliofurika kumsikiliza na waliokuwa watulivu, kwamba inaonyesha wizi huo uliwezekana kutokana na akaunti hiyo kutofanyiwa ukaguzi kwa miaka kadhaa kwa kuwa haikuwa mali ya serikali.

Rais alisema ni pale kampuni ya ukaguzi ya nje ya Deloitte & Touche ilipoishtukia akaunti hiyo mwaka juzi na kuamua ndipo ulipotokea mvutano na BoT ambayo iliikatalia na kuitimua. Alisema taarifa hizo zilipomfikia aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji alimwagiza aliyekuwa Gavana ukaguzi uendelee kwa kufanywa na Mkaguzi wa Kisheria ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kufanya ukaguzi huo uwe huru, iliteuliwa kampuni ya Ernst and Young ambayo ilithibitisha upotevu wa Sh bilioni 133 katika akaunti ya EPA kwa nyaraka za kughushi. Kampuni hiyo ilitoa mapendekezo kadhaa ambayo Rais alisema yamefanyiwa kazi, ikiwamo uundwaji wa timu iliyomkabidhi ripoti Jumatatu na kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Gavana, Dk. Daud Ballali
 
Kwa nini hawakamatwi wakawekwa ndani? Kulikoni wezi wakapewa muda na kisha kuongezewa ili warudishe walichoiba? Wanaweza wakashirikiana na polisi wakiwa mahabusu.

Serikali kwa nini haiweki majina ya wahusika walioamua kurudisha mabilioni waliyoiba hadharani? Je, katika kiasi hichi mnaweka na mali nyingine zilizofilisiwa kama nyumba na magari? Hizi pesa zimewekwa benki ipi na Watanzania tunaweza kupata uthibitisho toka benki hiyo? mnaficha nini na kwa maslahi ya nani?

Je, ni lini account ya EPA ilikuwa mali ya serikali rasmi? Nini kilitokea mpaka account hiyo kumilikiwa na serikali badala ya wafanyabiashara waliokuwa wanachangia?
 
Asilimia yetu hapa JF tunaopiga makelelele ni ndogo sana kulinganisha na wengi wanaoona kila kitu kiko sawa.

Na JK analijuwa hili fika! JF kazi yetu ni kelele, JK kazi kazi yake ni kuongoza inchi, at the end of the day he holds.
 
Bubu ataka kusema,
Shukran mkuu, hii ndio hotuba yote au kuna zaidi? Hata hivyo mbona nazidi kuchanganyikiwa!...

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kufanya ukaguzi huo uwe huru, iliteuliwa kampuni ya Ernst and Young ambayo ilithibitisha upotevu wa Sh bilioni 133 katika akaunti ya EPA kwa nyaraka za kughushi. Kampuni hiyo ilitoa mapendekezo kadhaa ambayo Rais alisema yamefanyiwa kazi, ikiwamo uundwaji wa timu iliyomkabidhi ripoti Jumatatu na kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Gavana, Dk. Daud Ballali.


Kulingana na kipande hicho cha hotuba hiyo inayohusu EPA ningependa kuelewa kama;-
1. KUGUSHI nyaraka ili kuchukua fedha kisheria ipo ktk Criminal act au?..

2. Hivi Balali alijiuzuru ama ulisimamishwa kazi?..
 
Bubu ataka kusema,
Shukran mkuu, hii ndio hotuba yote au kuna zaidi? Hata hivyo mbona nazidi kuchanganyikiwa!...



Hawa naona wameandika baadhi ya mambo tu katika hotuba hiyo. Labda baadaye tunaweza kuipata hotuba yote hapa ulumbini.
 
Na JK analijuwa hili fika! JF kazi yetu ni kelele, JK kazi kazi yake ni kuongoza inchi, at the end of the day he holds.
JK sidhani kama anaongoza nchi bali anaongozwa na MAFISADI.

Makelele yetu hapa JF ni ya kutaka mabadiliko mbalimbali yafanyike Tanzania ili kuboresha uchumi wa nchi na kuinua kipato cha mtanzania wa kawaida, kuondoa rushwa, kuondoa ufisadi, kulinda haki za watanzania wote.
 
Nina maswali kwa wana JF, naomba nielimishwe.

Kwanini tunaona ni kazi ya rais kuwashitaki walioiba EPA?
Je mwananchi hawezi kushitaki wezi wa mali ya umma?
Je wapinzani au wazalendo wameshindwa vipi kuwashitaki wezi wa EPA?

Naomba kuelimishwa
 
Back
Top Bottom