Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

...hiyo 200bn tunayoambiwa sitashangaa ikageuka 500bn,hakuna sababu ya kutumia pesa zote hizo kwa nchi ya njaa kama yetu,imarisha database ya vyeti vya kuzaliwa kwanza kwa kila mwananchi ili iwe primary identification then driving licence na passport navyo viimarishwe,hizo smart ID ni nzuri ila tatizo kuwaamini hawa mafisadi kwa pesa zote hizo na umaskini wetu tutapata hasara mara mbili,hizo billion 200 mwaga zote kwenye broadband hakikisha kila wilaya inakuwa connected na high speed internet,nyingine weka kwenye miradi ya umeme maana ni 15% tuu ya wananchi wanaopata umeme...tutapunguza umaskini kwa kiasi kikubwa sana,smart ID kwa sasa ni usanii tuu na haitabadilisha chochote kwenye maisha yetu!
 
Kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo maana hata kupima ulazima na umuhimu wa vipaumbele inakuwa shida.....aaaaghhh....

Eti vitapunguza uhalifu? What the...? Unataka kunambia kati ya Marekani na Tanzania ni ipi yenye uhalifu mwingi zaidi? Na ipi yenye mfumo bora wa ku wa trace raia wake? Na unazungumzia uhalifu gani? Udokozi? Ufisadi? Ujambazi? Utapeli? Mauaji ya Albino?

Vitazidisha mapato ya serikali? Hmmmm...really? How so?

Nyani Ngabu ubishi asili yako haipiti siku kama hujabishana humu anyway zilezile za kiafrika I guess you are not serious unafananisha uhalifu Marekani na population ya 300mil over 32mil. ya Tanzania.Na angalia id system zinasaidia kwa kiasi gani kukamata wahalifu........... think twice.

SAHIBA.
 
Okay, basi nitalinganisha Tanzania na jimbo kama Tennessee au Illinois au Michigan....okay?

Okay, au tulinganishe California yenye idadi ya watu inayokaribiana na Tanzania...sawa?

Pia pamoja na kwamba wenzetu na mfumo mzuri wa kufuatilia watu, hayo mambo ya ID au sijui SSN au sijui mi database ya DNA na mambo kama hayo, lakini bado hiyo haijawa deterrent ya uhalifu. Sijawahi kusikia popote zaidi ya kutoka kwako kuwa ID Card inaweza kusaidia kuzuia uhalifu.

Kusaidia kukamata, yes, to a degree lakini kuna mambo mengine pia. Kama ingekuwa hivyo tu basi wala kusingekuwa na cold cases....
 
Jamani:

Marekani vitambulisho vipo kama vile SSN, Kadi ya Udereva, na vitu vingi ambavyo viko linked na information systems ambazo zinawatambua watu.

Vitu vidogo vidogo kama kutambulika ni muhimu na vina saidia katika shughuli nyingi. Sababu kubwa ya wazawa kukosa hata mikopo katika benki zao wenyewe ni kutokuwa na vitambulisho.

Ni nana atakayekupa mkopo bila kukutambua ??? Ndio maji ni kitu muhimu sana, lakini kuna vitu ambavyo watu wanatakiwa wavifanye wenyewe.
 
Nyani Ngabu ubishi asili yako haipiti siku kama hujabishana humu anyway zilezile za kiafrika I guess you are not serious unafananisha uhalifu Marekani na population ya 300mil over 32mil. ya Tanzania.Na angalia id system zinasaidia kwa kiasi gani kukamata wahalifu........... think twice.

SAHIBA.

....bado sioni sababu ya kutumia 200bn kwa smart ID,hata hao wamarekani unaosema wako makini kukamata wahalifu wao hawana na wamekataa smart ID system na still wanatumia birth certificate,driving licences na social security ili kutambua watu wao,hiyo 200bn tukiwa makini bila ufisadi inaweza kupunguza umaskini kwa kiasi kikubwa sana kwa miradi kama ya umeme na broadband!
 
Okay, basi nitalinganisha Tanzania na jimbo kama Tennessee au Illinois au Michigan....okay?

Okay, au tulinganishe California yenye idadi ya watu inayokaribiana na Tanzania...sawa?

Pia pamoja na kwamba wenzetu na mfumo mzuri wa kufuatilia watu, hayo mambo ya ID au sijui SSN au sijui mi database ya DNA na mambo kama hayo, lakini bado hiyo haijawa deterrent ya uhalifu. Sijawahi kusikia popote zaidi ya kutoka kwako kuwa ID Card inaweza kusaidia kuzuia uhalifu.

Kusaidia kukamata, yes, to a degree lakini kuna mambo mengine pia. Kama ingekuwa hivyo tu basi wala kusingekuwa na cold cases....

Tukitumia sababu ya uhalifu ID card sio kizuizi. Kwa upande wangu ni faida kubwa iwapo watanzania wenye uaminifu wakaweza kutumia uamifu wao kama asset ya kuwapatoa mikopo. Nafasi za kazi. Kufanya mitihani na mambo mengi ambayo ni muhimu katika maisha yao.

Na hivyo vyote vinaweza kufanyika iwapo kutakuwa na system ya identification.

Sioni sababu ya mtanzania mwaminifu kukosa mkopo au mpaka atumie hati ya nyumba kupata mkopo wa laki tatu.
 
Asante mkuu zakumi nisaidie kumuelimisha huyu Nyani Ngabu amenivalia jezi ya kijani nafikiri ni yanga huyu hawa ni katika wale waliozivunja zile parking meter kule samora avenue baada ya uhuru wakasema zilikuwa za wakoloni sasa baada ya miaka arobaini wanafunga gari za watu kwa mataruma ya reli tungekuwa na vitambulisho askari anaweka ticket yake anaondoka makutano traffic unalipa fine na kesho yule dereva hapaki gari yake tena pale.
Kitambulisho kimeiingizia city mapato.

kitambulisho kimejenga nidhamu, kitambulisho kimeepusha rushwa kwa yule askari.

kitambulisho kimeipunguzia jiji gharama za kuiajiri ile kampuni ya mataruma ya reli.

Think twice.

SAHIBA.
 
Tukitumia sababu ya uhalifu ID card sio kizuizi. Kwa upande wangu ni faida kubwa iwapo watanzania wenye uaminifu wakaweza kutumia uamifu wao kama asset ya kuwapatoa mikopo. Nafasi za kazi. Kufanya mitihani na mambo mengi ambayo ni muhimu katika maisha yao.

Na hivyo vyote vinaweza kufanyika iwapo kutakuwa na system ya identification.

Sioni sababu ya mtanzania mwaminifu kukosa mkopo au mpaka atumie hati ya nyumba kupata mkopo wa laki tatu.

Sawa lakini utahalalishaje matumizi ya bil.200 ktk mradi wa vitambulisho?
 
Sawa lakini utahalalishaje matumizi ya bil.200 ktk mradi wa vitambulisho?

Don't get me wrong. Sioni sababu ya matumizi ya hizo pesa. Nina expertise katika masuala ya security. Na kwa analysis zangu ID zinaweza kutolewa bila kutumia pesa yoyote hile au kwa maana nyingine bila kuliingizia taifa gharama zozote.

Napenda matumizi ya ID lakini sio kwa gharama hiyo.
 
Naomba matoleo yanayofuata neno "page" libadilishwe kuwa "ukurasa"

Na matoleo yafuatayo Mhariri Mtendaji aondoe "Hoja ya Mwanakijiji" juu ya front page article ya Fred Katunzi.

Mhariri Mtendaji akishamaliza kuhariri anatakiwa ku back off kutoka katika ripoti na makala za waandishi. Toleo zima halina makala ya Mhariri Mtendaji hata moja, sasa "Hoja ya Mwanakijiji" inakujaje?
 
Asante mkuu zakumi nisaidie kumuelimisha huyu Nyani Ngabu amenivalia jezi ya kijani nafikiri ni yanga huyu hawa ni katika wale waliozivunja zile parking meter kule samora avenue baada ya uhuru wakasema zilikuwa za wakoloni sasa baada ya miaka arobaini wanafunga gari za watu kwa mataruma ya reli tungekuwa na vitambulisho askari anaweka ticket yake anaondoka makutano traffic unalipa fine na kesho yule dereva hapaki gari yake tena pale.
Kitambulisho kimeiingizia city mapato...
kitambulisho kimejenga nidhamu ........
kitambulisho kimeepusha rushwa kwa yule askari....
kitambulisho kimeipunguzia jiji gharama za kuiajiri ile kampuni ya mataruma ya reli.

Think twice.

SAHIBA.

Naelewa points zako na vilevile points za Ngabu. Kuna manufaa mengi ya kuwa na vitambulisho.

Lakini nchi yetu ni specialist katika kuwa na miradi iliyo kwenye daraja la Tembo Mweupe. Kwamba unaweka investment ambayo haileti matunda yoyote yale.

Kuna bibi yangu yupo kule kijijini Mgeta. Hajawahi kutoka nje ya kijiji na hana mpango wa kutembelea sehemu yoyote, lakini kuna uwezekano mkubwa gharama za kitambulisho zimemuingiza mtu kama huyu.
 
Hivi wapiga debe wa zoezi hili huko serikalini wamejaribu kujiuliza

1. Utunzaji wa hivi vitambulisho vya smart card kwa 80% ya wananchi wanaoishi vijijini itakuwaje kuzuia uharibifu wa mara kwa mara?

2. Vituo vya kutolea hizi smart card kwa mara ya kwanza na baadaye in case kimeharibika, kimepotea , data is corrupted etc vitakuwa mpaka wilayani au mkoani. Jinsi vituo vitakapokuwa vichache na mbali vitafanya zoezi za replacement kuwa gumu hasa kwa watu wa vijijini kwa kuogopa gharama na usumbufu.

3. Sijasikia elimu yoyote inatolewa kwa wananchi kuhusu mradi huu, manufaa, umuhimu, na kwa nini tuwe nao, zaidi ni majibizano ya wasomi tu....
 
Sawa lakini utahalalishaje matumizi ya bil.200 ktk mradi wa vitambulisho?

Unajua Nyani, katika hilo I see your point. In fact to be honest hata UK hakuna national ID na wananchi katika referendum wamegoma.

Mi nasema in an environment like Bongo where they cannot guarantee the security of my data, sitaki wawe na data zangu mpaka how many kids I have where I live, my bio data in the hands of corrupt tanzanian authorities!
We acha twende kibongobongo... kuna mtu kasema kuna birth certificate, kuna driver's ID (na ndo ID ya Marekani), kuna passport, tuzi-streamline na kuzitumia as ID.

Kuna kadi ya wapiga kura! Loads of ID forms floating in this country and we want to waste money on something that will not work anyway and will have our data up for sale for the next AlQaeda operative anayetaka kufanya uhalifu. Atamhonga mtu hapa atatoa passport based on your personal information, kesho unakuja kukamatwa wewe!

Mzee Mwanakijiji nita-sign your petition any day against this white elephant project!
 
Unajua Nyani, katika hilo I see your point. In fact to be honest hata UK hakuna national ID na wananchi katika referendum wamegoma. Mi nasema in an environment like Bongo where they cannot guarantee the security of my data, sitaki wawe na data zangu mpaka how many kids I have where I live, my bio data in the hands of corrupt tanzanian authorities!
We acha twende kibongobongo... kuna mtu kasema kuna birth certificate, kuna driver's ID (na ndo ID ya Marekani), kuna passport, tuzi-streamline na kuzitumia as ID. Kuna kadi ya wapiga kura! Loads of ID forms floating in this country and we want to waste money on something that will not work anyway and will have our data up for sale for the next AlQaeda operative anayetaka kufanya uhalifu. Atamhonga mtu hapa atatoa passport based on your personal information, kesho unakuja kukamatwa wewe!
Mzee Mwanakijiji nita-sign your petition any day against this white elephant project!

Susuviri:

Sababu za security sio za msingi sana
icon10.gif
. Sababu kubwa hapa ni investment capital inayotumika. Hii ni information system ambayo mara nyingi cost ya implementation ni 20% na ku-maintain ni 80%. Sasa kama unalipa 200bn now, basi kuna uwezekano mkubwa wa kulipa zaidi katika maintanance.
 
Unajua.. mradi wa minara ya benki kuu ulikuwa utumie kiasi cha kama dola milioni kama 200 hivi. Leo hii umevuka na kufikia milioni 369 hivi na bado haujaisha. Sasa kwanini watanzania wanafikiri kuwa mradi wa vitambulisho utatumia dola milioni 200 tu? Ni mradi gani mkubwa ambao umesimama kwenye makadirio yake?

Mmmhhhh.....hapo umelonga mkulu...Kwa staili hii nakuunga mkono..Kama vp tuendlee kutumia vile vitambulisho vya kupigia kura 😀😀😀....Maana piga ua ngoma lazima itaji'double' kama sio kufikia dola 500 million(kutokana na uzoefu wa 'nnji' yetu)
 
Kwa hali technolojia ya Tanzania smart ID card si muafaka. Tunahitaji kwanza kujenga miundo mbinu ya IT na kuwa na database ndio tu-introduce hizi ID. Hili zoezi litaleta matokeo mabaya sana.

By the way kama kwanini wasifanye kwanza kitu kama pilot study itakayohusisha sehemu ndogo ili waone matokeo yake kwanza?
 
...seems hata wabunge wetu hawajashtukia hili changa la macho maana wako kimya,hii kitu ni ya kupingwa kwa nguvu zote,ni gharama kubwa sana kwa nchi maskini kama yetu na ukiangalia vizuri faida zake ni ndogo kuliko hasara,siamni hii ita improve any chance ya mtu kupata mkopo kutoka Bank au kukamata wahalifu....nchi haina hata majina ya mitaa leo unaleta smart ID,ya nini?
 
Madhumuni ya kitambulisho ni kujua ni nani ni nani nchini. Kwa kweli hakuna ulazima wa kuchagua kitambulisho cha bei ya juu sana ambacho thamani yake inazidi kipato cha mwezi cha mtu wa kijijini anayetakiwa kuwa nacho.

Kama ni lazima kuwa nacho, mpaka sasa sijapata sababu ya msingi ya kwanini serikali haijatoa kazi hiyo kwa mpiga chapa wa serikali ambaye angevitengeneza kwa gharama nafuu hapa hapa nchini. Hoja kwamba hakuomba zabuni haina msingi. Hii ni sawa na mtu kuwa na gereji yake na anataka kutengeneza gari yake. Badala ya kutumia gereji yake, anatafuta gereji nyingine yenye bei kubwa na kutengenezea huko wakati gereji yake inauwezo wa kufanya kazi hiyo. Unbelievable...
 
Si nchi inatawaliwa na waluguru. Mluguru anakwenda kuuza mihogo sokoni na akimaliza kuuza anakwenda kwa mchuuzi wa mihogo na ananunua tena mihogo kwa sababu mihogo ya sokoni inanukia kisoko-soko.
 
Back
Top Bottom