Tanzania nchi iliyojaa wanafiki na wanaojali matumbo yao

Hakuna wakala aliyefukuzwa kituo chochote,ila kuna vituo upinzani hawakupeleka mawakala kwa hofu ya kushindwa😃.Mbowe aliwafukuza TBC kwenye mikutano ya cdm ,wangerusha vipi?

Unaweza kunia idadi ya watanznia waliouawa na polisi, Jeshi kipindi cha uchaguzi?
 
Unamdanganya nani? Siku ya uchaguzi Jaji mihayo kamishna wenu wa tume alitembelea jimbo la kawe iTV wakirusha live na alikutana na mawakala wa Chadema walioziwa kuingia vituoni. Haya yalifanyika tanzania nzima, Mara, Mwanza, Kigoma, Songwe , Mbeya na maeneo mengi sana. Kawadanganye huko lumumba
 
Sio mara ya kwanza kwa cdm na Zitto kupeleka mashtaka dhidi ya Rais magufuli huko ICC,wewe upo dunia gani😃
Labda ujiulize wewe mjinga. Hivi mnafikiri humu tumejaa wajinga kama hapo kwenu lumumba??? Weka ushahidi hapa lini tena ICC waliwai kili kupokea malalamiko dhidi ya Tanzania au mtanzania yeyote????
 
Na wewe endelea kuwadaganya wenzako,si ajabu chama kinakufa sababu ya kuwa na wanachama kama wewe
 
Unafiki wao na kujali matumbo yao sasa rasmi unatuangamiza!
"Tanzania nchi iliyojaa wanafiki na wananchi wanaojali matumbo yao."

Nimeisoma mada, lakini mwandishi hakuitendea haki 'heading' ya mada yake; badala yake kachepuka na kusisitiza mambo mengine.

Kichwa hicho cha habari ninakubaliana nacho, na hiyo ndiyo sababu ya matatizo makubwa yanayotukabili sasa kama taifa.
 
Mada imejikita kwenye watu walio karibu na Magufuli ambao wameshindwa kumshauri ukweli na kumwambia ukweli kwa sababu ya unafiki wao na kuogopa kupoteza kazi zao na mishahara yao( kujali matumbo yao)
 
Nasubiri ushahidi wako juu ya lini ICC iliwai pokea malalamiko juu ya Tanzania.
Nami nasubili ushahidi wa askari polisi na jeshi kuhusika kuua raia kipinndi cha kampeni, nipe idadi ya raia walioua na jeshi na polisi.
 
WAPIGA RAMLI MNAWEWESEKA BAADA YA KIPIGO CHA OCTOBER 28.
HAKUNA CHA ICC HAPA UCHAGUZI UMEISHA.
TULIWAONYA WAPINZANI MUACHE UHUNI BUNGENI NA NJE YA BUNGE HAMKUSIKIA SASA NDIO MMEWAJUA WATANZANIA
 
Tunavyo-worship hao wazungu...

Kama watanzania wengi wapo desperate enough kuichomoa CCM kingeshanukishwa bila hata kujali risasi za Tanpol.

Kwa kuwa wengi wape (democracy), tusubiri wengi yawafike shingoni, waamue wenyewe kuuvunja mfumo huu kwa damu au kalamu.

Maana ya taifa huru ni kwamba taifa linaamua lenyewe muelekeo wake. Hata kama linajipeleka kuzimu. Maana ya taifa la kidemokrasia, ni kwamba maamuzi huwa ni ya wengi na wengi hao ndio wenye jukumu la kuwa na huruma kwa wachache (minorities).

Hivyo, 'watanzania wengi' wakiamua kukinukisha kwa damu, hiyo ndio tafsiri ya taifa limeamua. Otherwise, ni watu wachache wanawaamulia watanzania wanachotaka; hakuna tofauti na CCM.

Wanasiasa wawaache hawa hawa majorities wajiamulie watakalo. Kwa mfano, sheria na kanuni 'kandamizi' za uandishi habari zilipigiwa kelele na wanasiasa wa upinzani na wanaharakati binafsi; halafu corporations za habari zikiwa kimya.
Inaonekana kana kwamba wahusika wameridhika, ila wanasiasa ndio wanaona shida.

Waache wananchi wengi wa taifa hili lilo huru waamue wenyewe lini wataamua kutoa ya moyoni, again, kwa upendo au upanga; otherwise inaonyesha hii ni vita ya wanasiasa wa pande mbili wakipigana wao wenyewe kuwaamulia watanzania kipi bora kwao.
 
Tunavyo-worship hao wazungu...

Kama watanzania wengi wapo desperate enough kuichomoa CCM kingeshanukishwa bila hata kujali risasi za Tanpol...
Watanzania hawaitaki Ccm na Hilo liko wazi, ndo mana mawakala wa vyama vya upinzani walizuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura tarehe 28, ndio maana mitandao imezimwa kwa Karibu 2 weeks during and after election na ndo mana watu maweuliwa waliokuwa wakipinga udhalimu..

Hata freedom fighter wa South Africa waliomba msaada nje baada ya movement ya ndani kukwama. Walikuja kukaa Tanzania na maeneo mengi ya Africa.

Sioni shida kwa wapinzani wa Tanzania kuomba msaada nje ya Tanzania maana huko ndo lazima suluhisho la uhakika litapatikana. Kwa wale tunaowategemea kutuletea watalii , kununua korosho zetu, Mbaazi zetu, madini yenu, Michele wetu na mbao zetu.

Hakuna namna sasaivi. Mbinu yeyote halali ya kupambana na ccm na udhalimu wao lazima itumike tu.
 
Tatizo kizazi kile cha mashujaa kinaendea mwishoni.
Kikiisha kizaz cha lika la akina magufuli kizazi.kinachofuata ni cha hovyo kupita.

Haiwezekani vijana wanakua fuata upepo,wakishawekwa kwenya ka wadhifa fulani anajisahau kabisa,kiburi chao majivuno kwao kinachofanyika hakuna.
Hovyo kabisa.
 

Nazidi kuelewa kwa nini Nyerere alisema kati ya maadui wakubwa wa Tanzania ni pamoja na ujinga...

Ni ujinga uliokithiri mtu kusimama na kutoa visingizio vyepesi kuwa maandamano hayakufanikiwa kwa sabb ya polisi...

Ni kweli Mkuu, ukimsikiliza Lissu vizuri, 100% anaamini turn out ya watu kuandama ndiyo ingeamua kufanikiwa kwa maandamano na si zuio la polisi...

Nje ya Lissu, Dada mpendwa Sarungi alitoa takwimu ya uwiano kati ya wananchi na jeshi, akijaribu kuonyesha hatuna jeshi lenye uwezo wa kuzuia wananchi...

Hata Binti Hellen Kijo alionyesha masikitiko dhidi ya Watanzania kwa nini hawakuandamana na sabb za msingi kwa mujibu wake zilikuwepo...

Lakini still hawa wanaojinasibu kuwa ni wakereketwa wa upinzani wana miss this point...

Nashindwa kuelewa upinzani unawezaje kutusua kama kiini cha tatizo tu hawakijui au wanakipuuza?
 
Mada imejikita kwenye watu walio karibu na Magufuli ambao wameshindwa kumshauri ukweli na kumwambia ukweli kwa sababu ya unafiki wao na kuogopa kupoteza kazi zao na mishahara yao( kujali matumbo yao)
Kichwa cha habari kilichotumika kiliwahusisha waTanzania, ( raia wake wengi) kuwa wanafiki, jambo amabalo ninakubaliana nalo. Kwa hiyo nilitegemea mada ijikite kuelezea kinagaubaga tabia hii ya waTanzania walio wengi, na sio hao wachache uliowalenga hapa.

Na kumbuka, hawa sio lazima wawe ndani ya chama cha CCM, hata kule upinzani wapo wengi tu, ndio maana unapoona viongozi wao wanapobinywa, hawa wanafiki hawanyanyui hata kidole kuwatetea viongozi wao.
Hata sisi wengine tusiokuwa na vyama, hala hiyo ipo sana kote nchini.

Mkuu wangu 'Lord' nadhani umetumia 'heading pana sana ikiwa inajumuisha, sio kwa makosa, ila nadhani hapo katikati ya kujieleza ukajikuta unasahau 'ujumla' wa hiyo 'heading' uliyotumia.
 
Umeandika vyema, hasa kule juu, ingawaje hapa chini sikuelewa unamaanisha nini.

Ngoja nikupe mfano pengine utakaoonyesha sisi waTanzania tulivyo tofauti sana na pengine ndiyo sababu ya haya yanayotusibu.

Pale Kenya, ukimgusa Raila Odinga kwa aina yoyote tegemea 'reaction' toka kwa wafuasi wake. Ndiyo maana, hata huko nyuma ilipotakiwa apewe kibano kama wanachokipata hapa akina Mbowe, hakuna aliyethubutu kufamfanyia kwa sababu walielewa kitakachotokea sio kizuri.

Hapa akina Mbowe wanaweza kuhangaishwa vyovyote iwapendezavyo watawala bila ya kuwa na hofu ya kitakachotokea kwa wafuasi wao. Usidhani huko CCM kuko tofauti. Leo hii hawa mabosi wanaotupeleka hati hati ikitokea wakawa ndio wanaopewa mbinyo, usitegemee kuwa kuna watu huko CCM watakaofanya lolote; tena usishangae ukakuta wengi wao ndio wakawa washangiliaji wakuu! Huu ndio unafiki ambao mleta mada alitakiwa aujengee hoja, lakini bahati mbaya kaishia kuvungavunga tu hii mada yake.

Na wewe hapa hujaeleza sababu za unafiki huu tulionao waTanzania, pamoja na kumweka Bi Kijo bila ya kutaja na kutoa ufafanuzi wa alichokisema yeye.

Ninakubaliana kuhusu kisingizio cha polisi sio sababu kubwa inayofanya watu wasiamue kuchukua uamzi wa kukataa kama wanaona wanayofanyiwa hayafai. Hakuna polisi wa kuzuia watu waliodhamiria kukataa kuburuzwa na kunyimwa haki.

Kinachoweza kuelezwa ni kwamba viongozi wa upinzani hawajafanya mipango mizuri ya kuwaongoza watu kukataa dhulma. Kwa mfano: hivi vyama vya upinzani vingekuwa vimejiandaa kukata na kuzuia uchafuzi wa uchaguzi na kuweka mipango na kuwaanda wananchi kukataa dhulma hiyo katika vituo vyote walikoondolewa wakala wao nchi nzima na kuzuia kuingizwa kwa karatasi zilizochafua kura za wananchi; huu ungekuwa mwanzo mzuri wa kuwahamasisha wananchi na ingewarahishia wananchi kufanya kazi hiyo bila ya maumivu yoyote toka kwa hao polisi, kwa sababu hakuna polisi wa kutosha kila sehemu ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…