balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,771
- 14,294
Hii siyo yangu nimekupakulia tuu humuhumu jfJenga hoja usirushe shutuma hewani bila mpangilio, tatizo wewe unarusha shutuma hujengi hoja, unatajataja majina tu bila vina wa hoja. Hakuna nchi yoyote duniani isiyo na sheria na taratibu, tunataka nchi iongozwe kwa sheria na taratibu zilizopo, nchi itakayowweza kufuata sheria na taratibu kwa mujibu wa katiba waliyojiwekea ndiyo tunasema ni nchi bora.
Sasa sijui nianza na yupi kwa sababu unataja watu ovyo ovyo bila mpangilio. Ngoja nianze na Manji, manji ameshutumiwa na makosa mengi tu, kuanzia matumizi ya dawa za kulevya ambapo vipime vya mkojo vya mkemia mkuu vimethibitisha sio maneno ya mtaani, Pili kukutwa na mihuri na nguo za jeshi, bado hizi zote ni tuhuma, utaratibu tuliojiwekea katika katiba yetu ni kwamba mtuhumiwa ni laxima apelekwe mahakamani ndiyo mahakama itaamua kama anakesi ya kujibu ama hapana, sasa katika suala la Manji wewe tatizo lako lipo wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app