Tanzania Premier League: Kuna ulazima wa klabu moja wapo (Simba au Yanga) iondoke Dar na kuhamia Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka

Inter, juve, Madrid, Barcelona na nyinginezo zote zinakuwa pale zilipoanzishwa, utaanzaje kuhamisha Sima au Yanga kwenye makao makuu yake.
Nani atalipa gharama za kuwaweka nje ya Dar kuanzia wachezaji hadi watumishi.
Nakubaliana na yule aliyekwambia hujui chochote kuhusu mpira.
 
Kwani lazima mechi ya Yanga (ikiwa nyumbani) na Mwadui FC ichezwe Dar? Kwani haiwezi kuchezwa katika mkoa ambao haujafanikiwa kupeleka timu ligi kuu?
Hii itakua sio fair kwa yanga au nini maana ya mechi ya nyumbani na mechi ya ugenini? Yani Mwadui akiwa mwenyeji acheze kwake ila Yanga mechi yake ihamishwe au unataka kuaminisha nn sijaelewa.

Mfumo wa mpira wa miguu ulimwenguni kote kwenye ligi kuna mechi za nyumbani na za ugenini kipi haswa special kwa simba au yanga mpaka wasiwe na home game?
 
Kuwahamisha sio tatizo kama wakiridhia na wakiamua hivyo, Gharama sio sababu kama pesa zipo...mbona serikali wakiwemo watumishi wake wananahamia Dodoma?

Sema tu hakuna timu hapo itakubali kirahisi
 
Kuwahamisha sio tatizo kama wakiridhia na wakiamua hivyo, Gharama sio sababu kama pesa zipo...mbona serikali wakiwemo watumishi wake wananahamia Dodoma?

Sema tu hakuna timu hapo itakubali kirahisi
Sio kila kitu ni siasa, sababu ya serikali kuhamia dodoma ni kuwa katikati ya nchi ili kuweza kutoa huduma kirahisi.

Ila kwa maendeleo ya sasa ya sayansi na teknologia hizo sababu zilikuwa zimepitwa na wakati.

Huwezi kuiondotoa team kwenye base fun yake sasa hivi Simba wana viwanja vya maxoezi Bunju pia wana eneo wanaloweza kujenga viwanja huko, yanga wana eneo kigamboni kwa kifupi ni hoja isiyo na mashiko na siyo hoja ya mtu anayefatilia mpira.
 
Kabla ya kujiuliza ya Simba na Yanga kuhama Dar, jiulize pia kwanini hatuna uwanja mzuri kama wa taifa nje ya Dar? hata wa kuingiza tuu watu elfu 30. Mbona timu ya taifa pia kila siku inacheza Dar tuu? yakiwezekana hayo basi hata kuhama simba au yanga Dar itawezekana
 
Wakati Azam inaanzishwa ningejua kiwango walichopanga kukiwekeza kwenye mpira ninhewashauri waweke mkoani....hapa namaanisha wangetengeneza mashabiki wao wengi kuliko pale dar ambapo watu wanaweza kama jibu siyo A basi lazima iwe ni B
 
Simba hawezi kuhama Dar kumbuka ameshaanza uwekezaji wa Viwanja na hostel
 
Yanga na Simba zote mbili zilianzishwa na Muzungu, kwa kifupi kama Muzungu hana mkono hakuna kitu kinafanikiwa hapa kwetu, kulingana na uzoefu wangu, na siyo Yanga na Simba tu hata angalia Coco Beach ndiyo Beach pekee ya maana Dar Mji uliojengwa ukingoni mwa Bahari na Coco ilitengwa na Mzungu, huko kwingine kote watu wamejenga kwenye fukwe, kwa nini watu watoke Mbagala na sehemu nyingine za Dar waende Coco beach kufwata ufukwe wakati huko kote Bahari ipo karibu?
 
Umeshaenda beach za kigamboni
 
Mashabiki wa YANGA ambao ni CCM wao ndio wahamie CHAO , kuna uwanja mkubwa unajengwa huko , mpira utakuwa na ladha.
 
Mkuu, ina maana wewe haujiamini bila mzungu?...

Siyo swala la mimi, ni swala na uhaliasia na ukweli uliopo, huko Mikoani unakokuongelea kulikuwa na Timu nzuri tu, Mwanza kulikuwa na timu hata Tanga nao walikuwa na African sports na Coastal union, Iringa, Songea kote huko sasa ziko wapi, isitoshe hata hizi Yanga na Simba naweza kwenda mbali kusema kwamba zinanawili na kushamili sababu ya Wahindi, ukiondaoa akina Mo, Manji Azam & co. siajabu hakuna kitu kitabakia na ndio maana Mo ni kama Mungu kwa baadhi ya watu, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…