Tanzania Premier League: Kuna ulazima wa klabu moja wapo (Simba au Yanga) iondoke Dar na kuhamia Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka

Tanzania Premier League: Kuna ulazima wa klabu moja wapo (Simba au Yanga) iondoke Dar na kuhamia Arusha au Mwanza ili kuongeza ladha ya mchezo wa soka

Unajuwa sio dhambi kupenda Simba na Yanga tatizo kubwa nchi hii ni washabiki wa miji mingine kidogo kuna miaka ya nyuma kulikuwa kama mfano Mwanza ukisikia Pamba, Coastal, Reli ya Moro au Tukuyu hata CDA hizi team zilikuwa zinapata support kubwa katika mikoa yao na hii ilileta upinzani. Ukisikia mechi Pamba na Yanga au Simba hii ni big game Tanzania au hata team za Zanzibar ulikuwa ukisikia Small Simba, Miembeni, Malindi au Kikwajuni ni hatari. Tatizo limeanzia hapa hizi team hazipati support kutoka kwa wenyeji chukulia mfano kwa wenzetu mfano Spain, Real na Barca na uhakika hata Spain watu wote wana unazi na team hizi ila mapenzi yao kwa team zao wanaonesha kwa wazi haiwezi kwenda Real Sevilla halafu ukute wakazi wa pale wanashangilia Real hakuna au EPL huwezi kukuta mtu Stoke city anacheza na Man halafu mji wa Stoke wavae jezi za Man hakuna hata kama moyoni wana support Man lakini ikicheza na team ya mji wake full support mji wao.
Washabiki wamiji mingine sio dhambi pendeni Simba na Yanga sana tu lakini inapokuja kucheza na vijana wenu simameni na vijana wenu team zenu mbaya zaidi hata viongozi wa kiserikali utasikia mimi Simba au Yanga sawa sio mbaya wote tumezaliwa tunapenda hizi team kwa ukubwa wao hakuna wa kukataa ila simama sema kama mbunge wa Kagera sema mimi Kagera Sugar kama Tanga support Coastal au African union tulete ushindani. Kuna mtu kawahi kuona Dortmund wanavaa jezi ya Bayern.
Unajua kufafanua aisee
 
Kabisa, zinadumaza soka la Tanzania. Chukulia mfano klabu kama Azam fc ndio utapata jibu mkuu.. Azam pamoja na uwekezaji wao mkubwa, lakini haina matokeo mazuri. ..



🇦🇷🇦🇷🇦🇷🔥🔥
Sasa mkuu matatizo ya Azam (kutokufanikiwa kwake) yana uhusiano upi na Simba/Yanga?
 
Back
Top Bottom