Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Kuna kitu kinaitwa Opras haina tofauti na performance appraisalSijuwi mfumo wa Tanzania upoje. Hizo "performance appraisal" kwa Tanzania anazijaza nani?
Mfano nchi niliyokuwepo kuna "performance appraisal" lakini inajazwa na "Private inspecting consultants". (Factor) kigezo cha kwanza kabisa ni katika kila kazi kuna kitu kinaitwa "fundamentals "za hiyo kazi. Inspector ndicho kitu cha kwanza anatazama. Asiyefata "fundamentals" za hiyo kazi anarudishwa akaisomee tena hiyo kazi (akiwa kazini), Akirudishwa huko ni automatically "entry level pay" yake inashuka kwa nusu nzima, inakuwa ni ya mwanafunzi wa kazi.
Bado haiondoi ukweli tz ukiharibu hapa unahamishiwa pale, Mchechu alifanya madudu nhc leo mama kamrudisha,Usilete ujinga uliosomeshwa na Walimu wajinga, unaweza jirekebisha.
Nilifikiri una uzoevu katika nchi mbalimbali zisizoendelea !!Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.
Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.
Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.
Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.
Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.
Miaka ya nyuma kwenye reforms zilizopendekezwa kwa serikali za mitaa hii kitu ilianzishwa na walikuwa wanaita OPRAS (open reviews appraisal system kama sijakosea) na wakaleta forms zinazotakiwa kujazwa every December ukionyesha your work plan kwa mwaka mzima, idadi ya siku za kazi, resources needed etc... Ikifika Novemba mfanyakazi na bosi wake wanapitia work plan kuona kipi kimefanyika na kipi hskijafanyika and why, na unapewa ratings/scores... Nilishuhudia baada ya mwaka tuu ukatupwa kuleeeeKweli kabisa, mfumo mzima wa kuendesha nchi unatakiwa upinduliwe kabisa.
Serikali inatakiwa iwe nyembamba sana na iwe ni "policy makers, facilitators and inspectors" tu.
Amelisema hili Prof AssadKweli kabisa. Ni mfumo ambao hata tuhangaike vipi na takwimu hautotupandishia uchumi kwa haraka. Ukichukulia kuwa Serikali ndio moja ya waajiri wakubwa sana Tanzania na nnauhakika over 90% ya waajiriwa serikalini ni underperformers.
Wengi wanaokimbilia kazi za serikalini ni wazembe na wabadhirifu.
Yaani ukae miaka 10 huku kazi yako ni kucheza karata kwenye pc au kwenye simu kazini halafu upandishwe cheo?Unamshauri nani?
Na ni kazi gani hizo ambazo uta monitor utendaji wa kila mtu?
Nikupe mfano Wizara ya mambo ya ndani inapandisha vyeo kwa mtindo hii miwili moja Elimu pili muda wako kazini haina mingine.
Mtu wa kidato cha nne asiye na fani yoyote anapata cheo kwa muda wa miaka mitatu hadi kumi anapata cheo. Kwa mwenye elimu ya zaidi ya form 4 au fani ni faida zaidi hii wizara performance ni nyumbani kwenu kwa maarabu huko
Kuna NGOs huku nchini huo ndiyo utaratibu wao na mikataba ya kazi una renew kila mwakaHata mimi. Nimeupenda. Naunga mkono hoja. [emoji1754]
Sure Mkuu. Nakubaliana na wewe 100%. 🤝🏽Kuna NGOs huku nchini huo ndiyo utaratibu wao na mikataba ya kazi una renew kila mwaka
Tosha sana. Pamoja na kuwa ni kipimo kidogo lakini kina nguvu sana. Hasa vile vya biometrics i.e fingerprints.Kusaini saa moja na nusu na kutoka saa tisa na nusu ni performance tosha
Sasa kwenye ofisi hiyo wa kwanza angeondoka huyo mwenye majukumu ya kuhakikisha hivyo vidude kufanya kazi. Kwani kuna "backups" za umeme kila namna, tena hizo "biometric attendance systems" nyingi hata vi battery vya remote tu vinafaa kwa backup. Tena siku hizi si lazima hata uweke vidole, unapita kwenye entrance tu vinakupiga na picha na kama haijakusoma hata mlango haufunguki, na hata mkiingia mlangoni kwa fujo, basi vitawapiga wote, havibabaiki.Tosha sana. Pamoja na kuwa ni kipimo kidogo lakini kina nguvu sana. Hasa vile vya biometrics i.e fingerprints.
Chakushangaza vilifungwa baadhi ya Sekta, vikaundiwa zengwe umeme ukawa unakatika Asubuhi muda wa kuingia na mwishowe vikachomolewa waya vikaharibiwa. Sasa ni 'Ngoma Isambe' 'Kama Kawa... Kama Dawa'.
Kofia Oyeee!!!
Mauzauza Oyeee!!!
Ni wazi kuwa "measures" na nini cha kufanya kinajulikana, tatizo linakuja ni nani wa kumvika paka kengele?Miaka ya nyuma kwenye reforms zilizopendekezwa kwa serikali za mitaa hii kitu ilianzishwa na walikuwa wanaita OPRAS (open reviews appraisal system kama sijakosea) na wakaleta forms zinazotakiwa kujazwa every December ukionyesha your work plan kwa mwaka mzima, idadi ya siku za kazi, resources needed etc... Ikifika Novemba mfanyakazi na bosi wake wanapitia work plan kuona kipi kimefanyika na kipi hskijafanyika and why, na unapewa ratings/scores... Nilishuhudia baada ya mwaka tuu ukatupwa kuleeee
Sijawahi kuzisikia hizo, nijuazo ni hizi, kama yetu, zinazoendelea na zilizoendelea.Nilifikiri una uzoevu katika nchi mbalimbali zisizoendelea !!
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kwa mfumo ulivyo rais akiwa mzembe atomatikale na wao wanakuwa wazembe, vilevile hakuna maala panapomtakata mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa kuwajibika pale mkoa wake au wila yake inapofanya vibaya, ni lini umesikia mkuu wa wilaya au mkoa amemkemea mkurugenzi wa halmashauri? Ukiona hiyo imetokea jua mkurugenzi aligoma kupeleka fungu.Unalosema linaweza kuwa kweli na linaweza kuwa si kweli. Umetumia kipimo kipi kumuona kuwa Rais ni mzembe.
Niuonavyo mfumo wa Urais Tanzani na madaraka aliyonayo Rais, hawezi kabisa kuwa mzembe, huo muda wa uzembe atautoa wapi? Sema wale wenye kumsaidia Rais ndio wanakuwa wazembe namba moja, hususan mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa tasisi na mashirikaya kiserikali/ Duh. Mlolongo ni mrefu sana.
Rais hana muda wa kuwa mzembe na Rais pekee bila kuwa mfumo thabiti wenye kueleweka hawezi uwa yeye inspector wa kila mtu.Kwa mfumo ulivyo rais akiwa mzembe atomatikale na wao wanakuwa wazembe, vilevile hakuna maala panapomtakata mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa kuwajibika pale mkoa wake au wila yake inapofanya vibaya, ni lini umesikia mkuu wa wilaya au mkoa amemkemea mkurugenzi wa halmashauri? Ukiona hiyo imetokea jua mkurugenzi aligoma kupeleka fungu.
HAKUNA.Sasa kwenye ofisi hiyo wa kwanza angeondoka huyo mwenye majukumu ya kuhakikisha hivyo vidude kufanya kazi. Kwani kuna "backups" za umeme kila namna, tena hizo "biometric attendance systems" nyingi hata vi battery vya remote tu vinafaa kwa backup. Tena siku hizi si lazima hata uweke vidole, unapita kwenye entrance tu vinakupiga na picha na kama haijakusoma hata mlango haufunguki, na hata mkiingia mlangoni kwa fujo, basi vitawapiga wote, havibabaiki.
Tatizo ni hilo la kulindiana madhambi, ukute "manager" anashirikiana na mlinzi kufanya dhambi, nani wa kumvika paka kengele?
Ni kweli. Tatizo ni KUBWA SANA.Rais hana muda wa kuwa mzembe na Rais pekee bila kuwa mfumo thabiti wenye kueleweka hawezi uwa yeye inspector wa kila mtu.
Tatizo letu naamini lipo kwenye mfumo wa elimu yetu kuanzia chekechea. Tumejazwa ujinga kuwa elimu ni kujuwa kusoma na kuandika tu. Ndiyo maana nasisitiza, hivi vipimo vya ubora vianzie mashuleni. Tukifanikiwa kupanguwa na kuwa na Walimu wenye kujielewa na kuelewa ni nini maana ya ubora, tutakuwa tumemaliza tatizo kwa asilimia nyingi sana.
Tatizo tulilonalo ni kubwa lakini linatibika.