Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Hizo sio wasifanye kazi. Pia sio sababu za kutofanyiwa tathmini ya kina. Tathmini ya kina itabaini uozo uko wapi na pia itakuwa ni mkombozi wa wafanya kazi. Kuliko sasa wajanja wachache hawaishi kukaa vikao vya kulipana pesa za bure.
Hakuna mtu asiyefanya kazi kwa kina. Ukweli ni kwamba watu wanafanya Kazi wanavyoweza.

UKiwa Daktari unasikiliza wagonjwa 200 kwa wiki, siyo kwamba hutawasikiliza ila huwezi kiwasikiliza kwa ufanisi unatakiwa.

Na siyo kwamba serikali haijui tatizo kubwa ni Nini.

Na ndio maana ukienda kwenye vikao vyao, hawataki kabisa kuambiwa changamoto. Wanachotaka kusikia Ni kwamba, wewe utafanyaje kutatua hayo matatizo.

Pamoja na kusukuma kibabe ili Mambo yasonge hivyo hivyo kwa kulazimisha
 
Sisi madereva wa halmashauri za wilaya ni uchafu tu.Gari ikifika muda wa matengenezo,basi itakaa gereji mwaka mzima.Sasa hapo utanipimaje kwa mfano na kosa ni la mwajiri mwenyewe?.
Mimi nawashangaa sana wanavyoandika wakati wengi wao wanalishwa maneno tu kuwa wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi na ni wavivu na wapigaji. Sijui inategemea Sekta na Sekta lakini wengine unakuta wanaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 2 usiku almost everyday na hakuna chochote cha ziada wanacholipwa.
 
Hakuna mtu asiyefanya kazi kwa kina. Ukweli ni kwamba watu wanafanya Kazi wanavyoweza.

UKiwa Daktari unasikiliza wagonjwa 200 kwa wiki, siyo kwamba hutawasikiliza ila huwezi kiwasikiliza kwa ufanisi unatakiwa.

Na siyo kwamba serikali haijui tatizo kubwa ni Nini.

Na ndio maana ukienda kwenye vikao vyao, hawataki kabisa kuambiwa changamoto. Wanachotaka kusikia Ni kwamba, wewe utafanyaje kutatua hayo matatizo.

Pamoja na kusukuma kibabe ili Mambo yasonge hivyo hivyo kwa kulazimisha
Nimesoma huu uzi watu wana very negative perception na civil servants lakini hawajui changamoto wanazokumbana nazo.
 
Kwani wanafuatwa majumbani kwao ili wapewe kazi? Zi wanaziomba wenyewe? Si wanaomba wao tena kwa kuzigombania? Wakubaliane na masharti ya KPI
Kwa hiyo mishahara kiduchu hata wanacho deliver ni kikubwa sana.......vinginevyo huduma za umma zinaweza kuzorota zaidi....badala ya kupandisha mishahara ya watumishi mnakimbilia kujificha kwenye KPI, poor you!
 
Nimesoma huu uzi watu wana very negative perception na civil servants lakini hawajui changamoto wanazokumbana nazo.
Asilimia kubwa siyo Watumishi. Na unavyojua kawaida ya watanzania wengi ni CHUKI inayoambatana na WIVU.

Halafu Kuna watu huwa wanadhani kila anayefanya kazi serikalini hajawahi kufanya kazi sekta binafsi.
 
Mimi nawashangaa sana wanavyoandika wakati wengi wao wanalishwa maneno tu kuwa wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi na ni wavivu na wapigaji. Sijui inategemea Sekta na Sekta lakini wengine unakuta wanaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 2 usiku almost everyday na hakuna chochote cha ziada wanacholipwa.
Haya watu wametoka nyumbani kwa, wameenda kusimamia zoezi la USAFI siku ya Muungano Ni Nani kawalipa?

Ishtoshe Watumishi WANAJITOLEA mnooo.

Ukisema kila kitu kifanyike kwa haki, serikali ndio itakayokwama.

Mfano, Kuna jamaa yangu yeye kwa kazi take alitakiwa kusimamia kata moja. Lakini kwasababu watu Hakuna anasimamia Tarafa nzima peke yake, na wakati huo huo Hana usafiri Wala pesa za usafiri anazopewa.

Unapigiwa simu hata SAA 12 Jioni kwenda kufanya kazi na Hakuna atakayekulipa.
 
Wazo zuri,ila changamoto nyingi kwa mfano walimu,manesi na madaktari wa vijijini wana mzigo mzito sn kuliko wa mjini.
 
Kabla ya kuzungumzia kwa wafanyakazi Anza na serikali iperform kabla ya kuongeza tozo na kodi
 
Sawa kabisa mradi mfumo ufumwe kwa mtazamo mpana (broader perspective) ya tathmini (evaluation) ya nguvu kazi. Kila nafasi ya kazi iwe na tathmini ya misingi (fundamentals), malengo, nidhamu, miiko, mafunzo endelevu kazini, nukta chanya na hasi (positive and negative points). Aaah mlolongo wa vipimo (measures) ni mrefu sana na inabidi ufatwe kimadhubuti (strictly).

Of course utekelezaji wa tathmini ya wafanyakazi kwa mtazamo mpana ya kila muda (periodical) fulani ina gharama (costly) zake kubwa lakini ikifanywa kwa misingi yenye makali (stringent fundamentals) kwa wanao tathminiwa na wanaotathmini itazaa matunda ndani ya miezi 12 mpka 24. Gharama zitajilipa maradufu kwa ufanisi wa muda mrefu utakao patikana.

Na mfumo huo utaifanya serikali kuwa ni kweli mtoa huduma kwa wateja wake(raia).

Wale wakubwa wa serikalini watakaopenda niwape ushauri wa kina kuhusu huu mpango wanitafute inbox, nipo tayari kuutoa ujuzi wangu bure kwa serikali yangu. Na mashirika binafsi wanaweza pia kunifata inbox lakini kwa mashirika kutakuwa na malipo, tena wakumbuke, huduma zangu siyo rahisi na non negotiable.

Natumai watakutafuta na/au kufanyia kazi ushauri wako.
 
Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.

Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.

Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.
I second you. Mimi niliwahi kufanya kazi mahalo Fulani. GM alikua mkaburu wa south Africa, ilikuwa Ili upande mshahara ni ufanye kazi na kilikuwa na mtihani kabisa. Ukipass unapandishwa mshahara. Ilikuwa ni kaz kaz na kusoma

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Maajabu! Hivi inakuwaje watu wanapinga hata mawazo chanya yanayoweza kuleta mabadiliko.

Definitely, to impliment changes, force must be applied.
Wewe umeona hapo kuna wazo?
FRDDzymX0AASLx1.jpeg
 
fikilia mwalimu wa mathematics 1 shule nzima ya kata ,cheo hawezi pata kwa ukilaza wa watoto kwenye ilo somo
Ni vifikra vidogo dogo tu ila vya msingi sana hili bibi limechemka pakubwa
 
Mimi nawashangaa sana wanavyoandika wakati wengi wao wanalishwa maneno tu kuwa wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi na ni wavivu na wapigaji. Sijui inategemea Sekta na Sekta lakini wengine unakuta wanaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 2 usiku almost everyday na hakuna chochote cha ziada wanacholipwa.
Mkuu katika sehemu inayoongoza kuwafanyisha kazi watumishi bila huruma,ni halmashauri za wilaya.
 
Unamshauri nani?

Na ni kazi gani hizo ambazo uta monitor utendaji wa kila mtu?

Nikupe mfano Wizara ya mambo ya ndani inapandisha vyeo kwa mtindo hii miwili moja Elimu pili muda wako kazini haina mingine.

Mtu wa kidato cha nne asiye na fani yoyote anapata cheo kwa muda wa miaka mitatu hadi kumi anapata cheo. Kwa mwenye elimu ya zaidi ya form 4 au fani ni faida zaidi hii wizara performance ni nyumbani kwenu kwa maarabu huko
Unamaanisha nini "nyumbani kwenu na kwa maarabu huko"?

Wewe unaonesha ni poyoyo na mzembe, hauna zaidi.
 
Bi Faiza nakuunga mkono kwa asilimia zote

Tena mimi huwa natamani hata mchakato wa kuajiri waalimu ziingizwe interviews, haiwezekani graduates wengi mtaani lakini kigezo bado ni degree!!

Mwisho wa siku waalimu wanaochaguliwa wengine ni tia maji tia maji na wakishaingia hawafanyiwi review yoyote hata wakifelisha consistently.

Huko kwenye elimu ndio haswa palitakiwa pafumuliwe na paboreshwe sana tena sana. Tunazalisha taifa la failures kwa kuwaacha failures ndiyo wawe Waalimu. Inasikitisha sana.
 
Huko kwenye elimu ndio haswa palitakiwa pafumuliwe na paboreshwe sana tena sana. Tunazalisha taifa la failures kwa kuwaacha failures ndiyo wawe Waalimu. Inasikitisha sana.
Failures wanakuwa walimu wapi?
 
Mimi nawashangaa sana wanavyoandika wakati wengi wao wanalishwa maneno tu kuwa wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi na ni wavivu na wapigaji. Sijui inategemea Sekta na Sekta lakini wengine unakuta wanaingia saa 1 asubuhi na kutoka saa 2 usiku almost everyday na hakuna chochote cha ziada wanacholipwa.
Hiyo ya "wengine" kufanya na "wengone" kutokufanya ndiyo vipimi vitabaini.

Kufanya kazi kwa muda mrefu hakumaanishi kuwa huyo anaeifanya hiyo kazi ndiye anafanya sana. Utakuta kazi ya masaa mawili mtu anaifanya masaa 12, utasema huyo ndiye mfanya kazi sana au mzembe sana? Fikiri.
 
Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.

Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.

Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.
Uko 100% correct lakini kuna nyongeza aina 2 kuna general increase hii ina base na report ya BOT on inflation lakini ni lazima kuwe na performance appraisal hii ni process za ndani na hii based na performance ndio unacho ongelea. Shida ni kuwa na system ya haki ili tusije kupeana nyongeza based na urafiki, mapenzi au sababu zingine ila kukiwa na system yenye kumpa mtu haki bila kujali unampenda au humpendi ila kila mtu anaona huyu ana stahili. Mimi nimefanya kazi kwenye kampuni namna hiyo ilikuwa kuna range 0-10% na ikija ile report unaweza kuta umepata 2% na Manager wako anaongea na wewe tunakupa 2 sababu moja, mbili, tatu kwa hiyo mategemeo yetu mwakani haya mapungufu uyafanyie kazi kwa uwazi kabisa yuko anaondoka na 10% na wako zero kabisa. Lazima hata yule wa zero atalalamika na kujiona alikuwa anastahili apate 10 ila ataambiwa hujapewa sababu labda time keeping yako, attitude yako, una warning mwaka huu, kazi zako humalizi kwa wakati atalalamika mwisho wa siku itamuuma na kujituma mwakani apate level nzuri. changamoto ni kuwa na system fair na process fair basi.
 
Back
Top Bottom