Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.
Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.
Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.
Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.
Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.
Sijajua Kama unazungumzia hili ukiwa na maslahi nalo, Kama mdau au unajaribu tu kumtetea Rais Samia. Nauliza hili kwasababu Kuna watu ambao siyo Watumishi ( just a bunch of stupid ashholes) ambao kwao mtumishi akiteseka au kudhalilishwa ndio Furaha yao.
Kwa hili, hata ukipita mtaani utagundua kiwa watu wanamzungumzia vibaya Rais Samia kwasababu hadhalilishi Watumishi, kuonea na matajiri pia.
Binafsi, Ni supporter mkubwa sana wa Rais Samia na ndio maana Mimi simlaumu kwa lolote kuhusu hili suala.
Kwanza Samia anajitahidi mnooo.
Ndani ya muda mfupi, Rais Samia amepandisha watu madaraja, Amelia annual increaments na kuajiri watu wengi tu, kitu ambacho Magu hakufanya ndani ya Miaka 6.
Rais Samia amewarudisha kazini darasa la Saba, na ametaka vyeti feki wapewe makato yao. Hili Hakuna mtu ambaye siyo mtumishi analipenda.
Watanzania wengi Wana Chuki sana na wivu Dhidi ya Watumishi na matajiri, na ndio maana akitokea Mwanasiasa anawadhalilisha anaonekana Jembe sana.
Turudi kwenye mada yako.
Ukweli mchungu ni kwamba, Mishahara ya wafanyakazi hasa wa serikali kuu na Mitaa bado Ni midogo sana. Hulu wakipewa majukukumu makubwa kuliko wanavyostahili kupewa.
Mfumo wa kupima utendaji kazi wa Mtumishi upo, kwa maana ya OPRAS lakini sometimes unajazwa tu kwasababu Mara nyingi watu wanafanya Kazi nyingi kuliko mkataba wao, wanatoa pesa zao mifukoni kazi ziende.
Nakupa mifano michache.
Mtu ameajiriwa Kama Daktari, amefika kazini amekuta Kuna Daktari mmoja na yeye Ni wa Pili, Kituo cha Afya au hospital zinafanya kazi masaa 24.
Stahiki ya Mtumishi Ni kufanya kazi 9 na mfano kea Daktari KUSIKILIZA watu 4 kwa siku. Hapo utafanyaje kazi?
Mtumishi huyo Hana housing allowance, nauli Wala chochote.
Mtu fulani ni Bwana let's assume, anafika kituo Cha kazi, Hana nyumba, Hakuna housing allowance Wala nauli. Muda huo Wilaya nzima wako 10. Anapewa Tarafa nzima!!! Atafanyaje kazi.
Mwalimu anaajiriwa kufundisha some la Hesabu au physics anafika shule anakutafuta yupo peke yake. Shule haina nyumba, Hana housing allowance Wala chochote.
Unaajiriwa Kama Mtendaji wa kata au. Kijiji, ( Happ nitoe mfano halisi ). Kuna kata kubwa fulani huku ipo karibu na Mpakani. Umeingia kazini, umefanya kazi, umetembeq sana kwa miguu, huna nyumba Wala chochote. Umerudi nyumbani baada ya muda wako wa kazi kuisha. SAA 10 Jioni unapigiwa simu Wamasai kutoka Kenya wameingiza mifugo yao kuvamia mashambani ya watu.
Hapo inabidi uchukue Boda Boda kwa pesa zako mfukoni ukafanye kazi ya serikali.
Na experience hii ninayosema ndio inawakuta Watumishi kila siku. Muda huo huo Mshahara wako Ni TGS B ( Tsh 410,000 kea mwezi hapo hujakatwa PAYE, NHIF, Chama Cha wafanyakazi, na PSSSF).
Hii ndio hali HALISI.