FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #61
Hayo yafungulie uzi wa mada yake.. Hapa mada ni namna ya kuongeza mishahara na vyeo.Umetazama upande mmoja wa shilingi, serikali yenyewe nayo itengeneze mazingira mazuri ya kazi kwa watumishi wake, kwamfano ;
Kabla ya kuwalaumu watumishi, ipo haja serikali ijjitazame je imetimiza wajibu wake kwa watumishii wake katika kila eneo la kazi?
- Vitendea kazi ni duni sana katiika maeneo mengi ya kazi kiasi kwamba kama mfanyakazi angetakiwa kumaliza kazi ndani ya saa moja, basi anatumia masaa mawili au matatu kwakuwa vifaa vya kazi ni duni
- Huduma nyingi za kiutumishi ziko hafifu sana katika maeneo ya kazi, kwamfano, mtumishi anakaa mbali na sehemu ya kazi, usafiri ni shida, kama anatumia usafiri wa bus la ofisi muda mwingi bus linachelewa kufika kituoni kuwachukua wafanyakazi na kuwarudisha kwasababu nyingi tu ikiwemo foleni, ubovu wa bus, kukosekana kwa mafuta nk, hata kwa wale wanaotumia usafiri wa mabasi ya biashara, huko ndiyo usiseme.
- Watumishi hawapewi nyumba za kuishi karibu na kazini walipo, matokeo yake wanapanga nyumba, kodi inakuwa kubwa, wanalazimika kwenda kupanga au kujenga vyumba viwili au vitatu mbali kabisa kwenye nafuu ya bei ya vyumba au viwanja, unategemea mtumishi wa namna hiyo atakuwa na perfomance kazini? Labda uwe boss, una usafiri wa kupewa na ofisi au nafasi yako nzuri una uwezo wa kujaza mafuta kwenye gari lako.
- Serikali haitoi nauli wala communication allowance kwa watumishi wa kada ya chini, hii inawapunguzia uwezo wa utendaji kazi watumishi wake, yapo mashirika binafsi yanatoa huduma hizi kwa watumishi wao na mambo yanakwenda vizuri, lakini ikiwa mtumishi hapewi subsidy ya vitu kama hivyo matokeo yake anatumia mshahara wake kuisaidia serikali kufanya mawasiliano na wakuu wake na pia kwenda na kurudi kazini, wakati mwingine anatumia nauli yake kwenda kufuatilia masuala ya ofisi kwasababu ofisi haina fungu la nauli wala simu.
Hakuna aliyelaumiwa hapa. Kusema watu wana underperform siyo kulaumu bali vigezo vyao vikiainishwa halafu hujawapa vitendea kazi watakuwa na haki ya kuachana na hiyo kazi, kwanini ufanye kazi sehemu ambayo haikupi vitendea kazi? utakuwa juha au haufahamu "fundamentals" za kazi yako.
Mfano wewe fundi mekanika uambiwe tengeneza magari bila spana? Ukikubali si wewe ndiye juha au mzembe, hakuna zaidi.