Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Rais kwa nafasi yake ni Mwajiriwa nambari moja.

Yeye ni Boss.

Yeye ni Msemaji wa mwisho katika Masuala mengi na mbalimbali ya Kiserikali, Kisheria na mengineyo.

Yeye anatazamiwa au naweza kusema tunamtizama matendo, mienendo na hasa utendaji kazi wake ili na sisi tujipimie kama ni kutembea au kukimbia.

Anaposhindwa au hao wanaomzunguka wanaposhindwa pamoja nae kuhusu jambo fulani katika uchangamoto wake na Suluhu kwa macho ya wazi bila kupepesa inaonesha jambo lenyewe linawezekana basi hatuna budi kumuona Mzembe.
Rais wa Tanzania (yeyote awaye) hana muda kabisa wa kuwa mzembe.

Mfano Nyerere, hakuwa mzembe kabisa lakini alishindwa kabisa kuuinua uchumi wa Tanzania kwa miaka 23 au zaidi aliyotawala, matokeo kang'atuka nchi ikiwa masikini hohehahe. Naamini tatizo kubwa ni watendaji na utendaji, Rais sio mtendaji, Rais ni facilitator. Kumbuka hilo.
 
Unalosema linaweza kuwa kweli na linaweza kuwa si kweli. Umetumia kipimo kipi kumuona kuwa Rais ni mzembe.

Niuonavyo mfumo wa Urais Tanzani na madaraka aliyonayo Rais, hawezi kabisa kuwa mzembe, huo muda wa uzembe atautoa wapi? Sema wale wenye kumsaidia Rais ndio wanakuwa wazembe namba moja, hususan mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa tasisi na mashirikaya kiserikali/ Duh. Mlolongo ni mrefu sana.
"...hawezi kabisa kuwa mzembe..."

Mfumo wa Urais au Cheo cha Urais ni sawa na kupewa swali 1 katika Mtihani na kupewa Majibu sahihi ya kuchagua mengi 3, 5, 10 au zaidi au pungufu huku ukitakiwa kwa Cheo na nafasi uliyonayo ni wewe pekee ndiye unayepaswa kuchagua jibu sahihi zaidi kuliko yote japo yote ni majibu.

Kazi za Washauri ni kutoa Mapendekezo yaliyo sahihi zaidi huku Wasaidizi ikiwa ni kutekeleza kulingana na maelekezo.
 
Unalosema linaweza kuwa kweli na linaweza kuwa si kweli. Umetumia kipimo kipi kumuona kuwa Rais ni mzembe.

Niuonavyo mfumo wa Urais Tanzani na madaraka aliyonayo Rais, hawezi kabisa kuwa mzembe, huo muda wa uzembe atautoa wapi? Sema wale wenye kumsaidia Rais ndio wanakuwa wazembe namba moja, hususan mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa tasisi na mashirikaya kiserikali/ Duh. Mlolongo ni mrefu sana.
Mtumishi amefanya uzembe katika Idara yake/ Wizara na wewe kama Rais unampa nafasi nyingine tena na tena kwasababu kwa akili yako unaona hakuna mwingine atayeiweza nafasi hiyo!!
 
"...hawezi kabisa kuwa mzembe..."

Mfumo wa Urais au Cheo cha Urais ni sawa na kupewa swali 1 katika Mtihani na kupewa Majibu sahihi ya kuchagua mengi 3, 5, 10 au zaidi au pungufu huku ukitakiwa kwa Cheo na nafasi uliyonayo ni wewe pekee ndiye unayepaswa kuchagua jibu sahihi zaidi kuliko yeyote japo yote ni majibu.

Kazi za Washauri ni kutoa Mapendekezo yaliyo sahihi zaidi huku Wasaidizi ikiwa ni kutekeleza kulingana na maelekezo.
Rais wa Tanzania(yeyote awaye) siyo mtendaji, ni "facilitator", maamuzi yoyote atakayotoa itategemea na watendaji wa hayo maamuzi. Hilo lipo wazi kabisa.
 
Huu utaratibu ndio unaotumika huku mbele,juhudi zako ndio zitakufanya uongezwe mshahara,

Huwezi kufanya kazi ile ile na kwa njia ile ile kwa miaka 5 halafu useme una experience ya hiyo kazi kwa miaka 5 wakati u are doing the same thing in a same way! Hakuna improvement yeyote toka kwako!

Povu ruksa.
 
Ndiyo hivyo meku, hata mimi nimeupenda sana huu uzi na kwa kuwa mleta mada FaizaFoxy ni ameshapata uzoefu nje ya nchi haya mambo alioyainisha yana misingi mikubwa sana kukuza uchumi wetu,

Leo katika pitapita yangu mitandaoni nimegundua GDP 2022/2023 ya kenya na Tanzania ya kenya ipo vizuri sana na inaendelea kufanya vizuri tangu 2021 sasa kama uchumi haupandishwi na wafanyakazi hizo hela za kuweka nyongeza ya mishahara inatoka wapi
Ni ngumu na hela za kuongeza hazitatoka au kuongezwa. Tuendelee kujadiliana labda JAWABU lipo hapa.
 
Lichama linaiba kura miaka nenda rudi halileti maendeleo vs rasilimali mkilichalenji linauwa na kuteka watu kwanini msianze kuliondoa lichama la hivi kabla hamjaenda kwa walimu na watumishi wanyonge?
Kuliondoa LICHAMA linahitajika LICHAMA lingine kubwa zaidi na lenye nguvu na uwezo wa kuliondoa na kama halipo basi hili LICHAMA litaendelea tu, hakuna namna.
 
Hapo nakubaliana na wewe, kwani wanasiasa hata wanapokaguliwa "administration" zao na CAG hakuna anaepata hati safi.

Mimi nahisi kwanza CAG awe huru na asiwajibike kwa bunge wala Rais. Apewe na meno ya kung'ata.
Apewe na nani sasa!?

Sasa ndiyo ujue kwanini watu hawaruhusiwi kufuga mnyama SIMBA [emoji881].
 
Hapo wapiga kura wanajiuliza, nmbadala wa "lichama" hili, kuna "lichama" lipi lengine lenye maana?

Chama kipi Tanzania amabacho kina hati safi kwa ukaguzi wa "portion" tu ya a"dministration" unaofanywa na CAG?

Hapa tunaongelea "performance" hatuongelei siasa, kwa sababu naamini Tanzania wana siasa wenye nia hasa ya kuleta mabadiliko kwa wananchi ni wachache sana, 90% wa ya wanasiasa wapo kwenye siasa kwa kuwa ni njia ya mkato ya kujineemesha, hususan bunge.
Hakika.[emoji1430]
 
Mtumishi amefanya uzembe katika Idara yake/ Wizara na wewe kama Rais unampa nafasi nyingine tena na tena kwasababu kwa akili yako unaona hakuna mwingine atayeiweza nafasi hiyo!!
Hapana si kweli. Tupe mfano hai, hapa hatuongelei ushabilki.

Watanzania tusifikirie kuwa Rais yuko pale anafanya miujiza. Rais pia anategemea wataalaam wa kila nyanja wamshauri na watendaji watende, sasa ikiwa watendaji wenyewe hawjaweka vigezo vya utendaji wa kila kazi na vipimi vyake vya kuwa hapa, hiki huyu anakiweza, mshahara wake upande hivi a huyu hawezi ashushwe hivi. Unategemea lipi katika hali kama hiyo?

Mwarubaini ni watendaji waanze kuwekewa vipimo na "indepent consultants" na wawe "fundamentalists" kwenye fani zao. Vipimo vijadiliwe kama inavyojadiliwa budjet (siongelei vipimo vijadiliwe bungeni) na mpaka consultants wajirihishe kuwa, mgfani hai, "receptionist wa idara fulani "fundamentals" za kai zake ni hizi, performance yake ikidhi haya, kuanzia dress code, muda wa kazi kuingia na kutoka, kanuni za kazi zake, kama hajakutwa reception hatua zipi, akikutwa kakaa anaongea na simu au anakula ofisini, hatua ni hizi. Ofisi yake ikiwa "inanuka ishuzi" hatua za kuvhukuliwa ni hizi. Hivyo hivy kwa nafasi zote za kazi. Anaekiuka japo moja ya jilo basi hana kuongezwa mshahara wala cheo na akirudia hili hilo mara kadhaa basi nafasi hiyo haimfai. Yakiwepo hayo lazima tutie adabu.
 
Rais wa Tanzania (yeyote awaye) hana muda kabisa wa kuwa mzembe.

Mfano Nyerere, hakuwa mzembe kabisa lakini alishindwa kabisa kuuinua uchumi wa Tanzania kwa miaka 23 au zaidi aliyotawala, matokeo kang'atuka nchi ikiwa masikini hohehahe. Naamini tatizo kubwa ni watendaji na utendaji, Rais sio mtendaji, Rais ni facilitator. Kumbuka hilo.
Samahani naomba maana ya "facilitator" kwa jinsi unavyoitafsiri wewe?
 
Kwa jinsi ninavyoilewa mimi au niseme kutoka Gugo.

What Is a Facilitator?
A facilitator plans, guides and manages a group event to meet its goals.

To facilitate effectively, you must be objective and focus on the "group process." That is, the ways that groups work together to perform tasks, make decisions and solve problems. [1] Good facilitation involves being impartial and steering the group so that its ideas and solutions flow.
 
Hapana si kweli. Tupe mfano hai, hapa hatuongelei ushabilki.

Watanzania tusifikirie kuwa Rais yuko pale anafanya miujiza. Rais pia anategemea wataalaam wa kila nyanja wamshauri na watendaji watende, sasa ikiwa watendaji wenyewe hawjaweka vigezo vya utendaji wa kila kazi na vipimi vyake vya kuwa hapa, hiki huyu anakiweza, mshahara wake upande hivi a huyu hawezi ashushwe hivi. Unategemea lipi katika hali kama hiyo?

Mwarubaini ni watendaji waanze kuwekewa vipimo na "indepent consultants" na wawe "fundamentalists" kwenye fani zao. Vipimo vijadiliwe kama inavyojadiliwa budjet (siongelei vipimo vijadiliwe bungeni) na mpaka consultants wajirihishe kuwa, mgfani hai, "receptionist wa idara fulani "fundamentals" za kai zake ni hizi, performance yake ikidhi haya, kuanzia dress code, muda wa kazi kuingia na kutoka, kanuni za kazi zake, kama hajakutwa reception hatua zipi, akikutwa kakaa anaongea na simu au anakula ofisini, hatua ni hizi. Ofisi yake ikiwa "inanuka ishuzi" hatua za kuvhukuliwa ni hizi. Hivyo hivy kwa nafasi zote za kazi. Anaekiuka japo moja ya jilo basi hana kuongezwa mshahara wala cheo na akirudia hili hilo mara kadhaa basi nafasi hiyo haimfai. Yakiwepo hayo lazima tutie adabu.
Siwezi kumtaja jina ila Mama kabla ya kumuapisha alimwambia nimekupa tena ili ukajirekebishe na kufanya vizuri.

Jamaa akainuka 'akasujudu' kisha akakaa.
 
Siwezi kumtaja jina ila Mama kabla ya kumuapisha alimwambia nimekupa tena ili ukajirekebishe na kufanya vizuri.

Jamaa akainuka 'akasujudu' kisha akakaa.
Elewa kuwa huu uzi haukulenga "kusaka wachawi", huu uzi umelenga kushauri namna ya mfumo unaotumika sasa hivi kupandisha watu mishahara na vyeo.

Kwa ufupi, tunachoongelea hapa ni namna ya kupandisha mishahara na vyeo, isiwe kwa mfumo uliopo sasa bali ubadilishwe na kuwa "performance based".

Hayo ulioleta wewe ni "kusaka wachawi". Uzi haujelenga huko kabisa, tujikite kwenye mada. Tukianza kusaka wachawi tutaondoka kwenye mada. Ukisoma vizuri post namba moja imeshasema kuwa zaidi ya 90% ya wafanyakazi wa Tanzania, hususan serikalini, ni under performers.
 
Samahani naomba maana ya "facilitator" kwa jinsi unavyoitafsiri wewe?
Sijatafsiri kabisa maana ya "facilitator", nimeliweka hilo neno kama lilivyo. Kama hauielewi maana ya "facilitator", nakushauri ingia kwenye "dictionary" au uliza wenyeuzoefu wa kutafsiri, nimekosa neno sahihi la Kiswahili ndiyo maana nikaliweka kama lilivyo. Siku nikilipata neno sahihi kwa Kiswahili ntafanya editing nilipoliweka neno hilo. Kwa sasa utaniwia radhi.
 
Kwa hiyo watendaji wa chini ndio walimlazikisha Nyerere kupigana vita Msumbiji, Uganda na Zimbabwe mpaka akasahu kujenga nchi yake?
Sipo huko kabisa. Nipo kwenye namna bora ya kupandisha mishahara na vyeo.

Nyerere nilitolea mfano wa kuwa msimamizi mkuu wa nchi na akashindwa kuunda mfumo mzuri wa kubaini utendaji mbovu uliopelekea nchi ikawa masikini wa mwisho duniani. na ndio, kwa bahati nzuri au mbaya, unaotumika mpaka leo hii.

Tusitegemee muujiza kutoka kwa Rais, yeyote awaye, ikiwa hatuna mifumo thabiti ya namna ya kuongezeana mishahara na vyeo kwa watumishi wa serikalini. Tutabaki kila kukicha kungoja huruma ya Rais.

Nnaamini kukiwa kuna mfumo thabiti hata Rais atakuwa hana tena kazi ya kuingilia haya mishahara na vyeo.
 
Apewe na nani sasa!?

Sasa ndiyo ujue kwanini watu hawaruhusiwi kufuga mnyama SIMBA [emoji881].
Ndiyo tunashauri hivi, wenye kumpa au watakubali au watakataa lakini "message sent".
 
Soma ibara ya 23 utapata jibu. Acha ujuaji usio kuwa na tija. Kima cha chini hakina sababu ya kuwepo na vigezo ni suala la kuwa na mshahara unaokidhi mahitaji kwa watumishi. Katiba ipo wazi ni kuwa na just renumeration.
Hujajibu swali nililokuuliza. Sasa wewe mjuaji lijibu kwanza swali hilo halafu uendelee na ujuwaji wako. Linakushinda nini kujibu? nakuongeze swali lingine hapa chini...

Hiyo katiba iliandika wapi kuwa kupandishwa mishahara na vyeo mpaka kutegemee huruma ya Rais?

Wewe itakuwa katika wale wfanyakazi wazembe ambae hutaki "performance" yako ipimwe. Endelea kusubiri huruma ya Rais.
 
Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Umetazama upande mmoja wa shilingi, serikali yenyewe nayo itengeneze mazingira mazuri ya kazi kwa watumishi wake, kwamfano ;
  1. Vitendea kazi ni duni sana katiika maeneo mengi ya kazi kiasi kwamba kama mfanyakazi angetakiwa kumaliza kazi ndani ya saa moja, basi anatumia masaa mawili au matatu kwakuwa vifaa vya kazi ni duni
  2. Huduma nyingi za kiutumishi ziko hafifu sana katika maeneo ya kazi, kwamfano, mtumishi anakaa mbali na sehemu ya kazi, usafiri ni shida, kama anatumia usafiri wa bus la ofisi muda mwingi bus linachelewa kufika kituoni kuwachukua wafanyakazi na kuwarudisha kwasababu nyingi tu ikiwemo foleni, ubovu wa bus, kukosekana kwa mafuta nk, hata kwa wale wanaotumia usafiri wa mabasi ya biashara, huko ndiyo usiseme.
  3. Watumishi hawapewi nyumba za kuishi karibu na kazini walipo, matokeo yake wanapanga nyumba, kodi inakuwa kubwa, wanalazimika kwenda kupanga au kujenga vyumba viwili au vitatu mbali kabisa kwenye nafuu ya bei ya vyumba au viwanja, unategemea mtumishi wa namna hiyo atakuwa na perfomance kazini? Labda uwe boss, una usafiri wa kupewa na ofisi au nafasi yako nzuri una uwezo wa kujaza mafuta kwenye gari lako.
  4. Serikali haitoi nauli wala communication allowance kwa watumishi wa kada ya chini, hii inawapunguzia uwezo wa utendaji kazi watumishi wake, yapo mashirika binafsi yanatoa huduma hizi kwa watumishi wao na mambo yanakwenda vizuri, lakini ikiwa mtumishi hapewi subsidy ya vitu kama hivyo matokeo yake anatumia mshahara wake kuisaidia serikali kufanya mawasiliano na wakuu wake na pia kwenda na kurudi kazini, wakati mwingine anatumia nauli yake kwenda kufuatilia masuala ya ofisi kwasababu ofisi haina fungu la nauli wala simu.
Kabla ya kuwalaumu watumishi, ipo haja serikali ijjitazame je imetimiza wajibu wake kwa watumishii wake katika kila eneo la kazi?
 
Back
Top Bottom