Tanzania tukipunguza idadi ya vyama vya siasa kutoka 26 hadi 4 itapendeza?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Jf team,

Salaàm!

Binafsi sioni haja ya kuwa na vyama vya siasa lukuki hapa nchini. Na huenda uwepo wa vyama lukuki ni chanzo cha matumizi ya fedha za umma kuwa makubwa kupitia ruzuku.

Nashauri:-
1. Tuone iwapo itapendeza kupunguza vyama hivyo toka idadi ya sasa 26+ na vibakie 3 au 4 tu.

2. Vyama vinavyoweza kubaki viwe CCM, CDM, ACT na Umoja. Hapa tutaokoa ruzuku zinazotumika vibaya bila sababu.
 
Punguza mikoa, ibaki 20,punguza ma waziri wabaki 17,punguza ma Jimbo/wa bunge wabaki 100,futa ondoa cheo cha mkuu wa mkoa, na ma vyeo mengine ya, hovyo kama mkurugenzi wa, utamaduni wa, wilaya, nk
 
Vyama inatakiwa visizidi vitano. Vyama vingi inakuwa kama ligi ya mpira haijulikani hii nchi ina ugumu kiasi gani mpaka kuwepo muunganiko wa mawazo tofauti ya kutosha vyama 26.

1. Chama kisicho na kiti bungeni kifutwe.

2. Chama kisicho na wanachama walau laki moja nchi nzima kifutwe (sababu wengi huwa mashabiki ila kuwa wanachama hai ni vigumu, idadi ya 100k ni kipimo cha wastani).

3. Chama kisichoshiriki chaguzi chenyewe kila uchaguzi eti kinaunga mkono chama kingine kifutwe kikaungane uko moja kwa moja.
 
Uwepo wa vyama vingi ni mtaji kwa chama tawala CCM. Maana kwa miaka nenda utaratibu huu umekuwa ukiwasaidia kwenye kupandikiza mamluki wao kwenye hivyo vyama vingine kwa lengo la kudhoofisha nguvu ya upinzani nchini.

Na ndiyo maana kuna baadhi ya vyama huonekana nyakati za uchaguzi tu. Uchaguzi ikipita, na vyenyewe vinapotea.
Binafsi nilitamani uwepo wa vyama viwili tu vikuu kama ilivyo kwa Wamarekani. Na hivyo wananchi wawe na uhuru wa kuchagua chama wakioendacho, kuongoza.
 
Punguza mikoa, ibaki 20,punguza ma waziri wabaki 17,punguza ma Jimbo/wa bunge wabaki 100,futa ondoa cheo cha mkuu wa mkoa, na ma vyeo mengine ya, hovyo kama mkurugenzi wa, utamaduni wa, wilaya, nk
Welldone mkuu, paza sana sauti kuhusu hili, serikali yetu ni kubwa mno!,mawaziri 15 tu wanatosha, mikoa 20 tu inatosha, wilayani abakie Mbunge na DED, the rest no uchafu, na uchafu mwingine unaonuka vibaya ni msajili wa vyama, futilia mbali uozo huu,political parties zikajisajili kwa NEC maana ndio wenye uchaguzi
 
Huna hoja upuuzwe.

Vyama vyingi vya upinzani Tanzania ni wasaka tonge..

Hakuna upinzani wa kwl Tanzania.,,
 
Hivyo vingine ni vyama rafiki na hao wa jembe na nyundo!
 
📌📌📌📌🔨🔨🔨🔨🔨🔨
""""Chama kisichoshiriki chaguzi chenyewe kila uchaguzi eti kinaunga mkono chama kingine kifutwe kikaungane uko moja kwa moja.""""
 
CCCM ni chama HEWA,

Hakijawahi sajiliwa popote.
 
Chama ni CCM na hayo mengine ni mapandikizi yake.
 
Umasikini ukipungua Tz, kuna uwezekano vyama pia vikapungua.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Punguza mikoa, ibaki 20,punguza ma waziri wabaki 17,punguza ma Jimbo/wa bunge wabaki 100,futa ondoa cheo cha mkuu wa mkoa, na ma vyeo mengine ya, hovyo kama mkurugenzi wa, utamaduni wa, wilaya, nk
Fanya hivi wabunge wasipewe mishahara, ifutwe. Wakienda bungeni wawe wanalipwa posho ya kujikimu (night allowance) kwa rate ya serikali. Usafiri wapande bus/ndege kulingana na anapotoka na wakifika wanarudishiwa nauli zao. Vikao muhimu tuu ndiyo watakuwa wanakuja Dodoma kama kupitisha bajeti, vikao vingine watafanya kwa zoom meeting wakiwa majimboni mwao. Hii ikifanya miaka 2 tuu watajichuja wenyewe, wale wabunge maslahi wote watakimbia na watabaki wale wenye wito tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…