Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Nashukuru sana Mkuu.
Nakumbuka miaka ya 1990 hivi sehemu ambazo zilikuwa na viwanda vidogo na vile vya kati vilikuwa zimechangamka sana kulinganisha na sasa hivi. Wale waliokulia sehemu zenye Ginery (viwanda vya kuchakata mazao yatokanayo na pamba ikiwemo mafuta ya pamba), wanaweza kushuhudia hili. Viwanda alivyojenga Mwl. vilisaidia sana nchi kutokuwa na matumizi makubwa sana ya fedha za kigeni katika kuagiza bidhaa toka nje ya nchi. Nchi yetu ilijitegemea kwa mambo mengi madogo madogo tofauti na ilivyo sasa. Tulizalisha mafuta ya kula, sabuni, nguo (Mwatex, Mutex), hapa hapa kwetu.
Maisha enzi hizo yalikuwa na "ladha" tofauti na ilivyo sasa.
 
China wamefanya hivyo na wamepiga hatua.

Mambo mengi hutegemea political will ili yaende.

Sisi hatuna viongozi wa aina ya China na Russia.

Yaani viongozi mabeberu lakini wazalendo, hao hatuna.
China ili fanya mabadiliko kadhaa ya kisera kwa ukomunisti wao naweza ita mabadiliko makubwa.

Kwa kiasi kikubwa ukomunisti wa mwanzo wa China na huu wa sasa wenye sifa za kichina una mabadiliko kadhaa.

Nyerere aligoma kufanya mabadiliko kwenye fikra zake kuhusu ujamaa wake ndio maana aling'atuka.
 
Ndiyo Mkuu.
Waafrika wengi kwa asili tulikuwa wajamaa
Kwa sababu tulikuwa tunaishi kimakundi jamii ndogo ndogo.

Unafikiri jamii kubwa kama taifa linaweza ishi mfumo wa kale bila mabadiliko ya usasa ?
 
Unataka turudi enzi za jumapili
Mwisho kutumia magari binafsi
Ni saa 12 jioni....[emoji1]

Ova
 
China wamefanya hivyo na wamepiga hatua.

Mambo mengi hutegemea political will ili yaende.

Sisi hatuna viongozi wa aina ya China na Russia.

Yaani viongozi mabeberu lakini wazalendo, hao hatuna.
Russia haina mfumo wa ujamaa wala ukomunisti kuanguka kwa U.S.S.R kuliangusha kila kitu
 
Maisha ni yale yale,exactly unaweza kuwa na mimali mingi lakini ukawa unaishi maisha yasiyokuwa na furaha

Ova
 
Nathubutu kusema wewe Pascal Mayalla ni "genius ". Una uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kupembua mambo.
Nina imani siku moja utatufaa sana sehemu mojawapo serikalini endapo tukipata viongozi wazalendo.
Asante sana, kwa umri wangu niliofikia, ni over and above kuteuliwa!. Mtu kulitumikia taifa na kuwatumikia Watanzania, sio lazima uteuliwe, haya maandiko yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa", ninayoandika humu na kwenye magazeti ni huduma tosha kwa Taifa na kwa Watanzania, and soon, kipindi kitaingia kwenye mainstream media
View: https://youtu.be/b67jqx0GWd8?si=dJMLlehgMKg5Ua5M na kitakuwa moto kama kile kipindi changu cha Kiti Moto
P
 
Kabisa kabisa ! Sisi wengine tulikuwepo wakati ule na sasa pia bado tupo we knew and we know the whole truth !!
Hatujalishwa matango pori sisi !!
Kukaa foleni ugawaji kusubiria,bidhaa
Sukari nk [emoji1]

Ova
 
Vita baridi vimekuwepo toka kutamatika kwa vita vya pili na vilikuwa vya pande mbili U.S.A VS U.S.S.R, Ubepari Vs Ukomunisti.

U.S.S.R walipambana kuangusha ubepari sehemu yoyote duniani na U.S.A walipambana kusimika ubepari sehemu yoyote duniani.

U.S.A alitumia ubabe wa kiuchumi na kijeshi kunyong'onyesha wakomunisti sehemu yoyote duniani na Russia alitumia pesa na silaha kufadhili mapinduzi ya wakomunisti dhidi ya ubepari sehemu mbalimbali duniani.

Vita baridi vilikuwa vya pande mbili U.S.A na U.S.S.R sio upande mmoja pekee
 
Wewe ndio huna akili na ikiwezekana una matope kabisa,badlands ya kusema athali za ujamaa katika kipindi chake wewe unaleta athali za ujamaa baada ya mabeberu kuwapiga pini juu ya kuendesha Nchi kwa sera ya Ujamaa.
Kwa hio unadhani tukianza ujamaa saizi hatutapigwa pini?
Kama unapenda sana ujamaa hamia North Korea
 
Ujamaa unatendeka vipi kwenye hizo nchi ulizo taja ?

Na tafsiri ya ujamaa kwa Nyerere ilikuwa ipi ?
 
Ulisoma ripoti ya mwanzo baada ya kuanza utekelezaji wa Azimio la Arusha matokeo yake yalikuwa yapi ?
 
Kufeli kwa ujamaa kunaanzia mbali sana kabla ya kufika kwenye USA na washikaji zake,

Uzalisha ndani ya nchi tu ulikuwa mdogo,
Tulishindwa kuzalisha Sabuni, sukari, mafuta na hata chumvi ya kutosha wakati tuna bahari kubwa, na hapo USA alitutesa? Mwinyi anadai UDA ilikuwa inakufa kabisa, ufanisi ulikuwa chini ya sifuri, napo USA ? Nyerere alipiga marufuku TV na computer 💻 kwa raia wake wasipate kujua yanayoendelea nje, na pia wasipate kufunguka kifikra, nayo tulaumu USA,
USA alikuja tu kupiga msumari wa mwisho kwenye jeneza, ila ujamaa ulijizika wenyewe, hata USA asingeingilia, ujamaa ulikuwa unafeli, sera kama vijiji vya ujamaa, maduka ya ushirika, ni sera ambazo no way huku duniani zitafanikiwa, hata ufanyaje hutoboi


Ujamaa unafeli kwa sababu unajengwa kwenye misingi ya kuleana watu wavivu na wenye nguvu wote kuwakandamiza
 
...1980 uchumi ulianza kwenda Kombo ....mara kwanza JKN aliomba kutoka 1983.....wapambe kina Butiku wakagoma....1985 akasema siombi tena ushauri akatoka....alishaona ujamaa sio njia pekee tena kumiliki na kukuza uchumi...kama tulivyolaririshwa.....wewe unachosema hukielewii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…