- Thread starter
- #61
Nashukuru sana Mkuu.Mto hoja wewe ni Mwamba sana,tumerudi nyuma mara 1000 na sababu kuu ni moja veranda vyote vilivyojengwa na kufanya kazi katika kuishi sera ya ubepari vilibinafisihwa na wajanja wachache wakanufaika na badaye vilikufa-na matatizo ya kiuchumi kama kukosekana kwa ajili yakaanzia hapo.
Nakumbuka miaka ya 1990 hivi sehemu ambazo zilikuwa na viwanda vidogo na vile vya kati vilikuwa zimechangamka sana kulinganisha na sasa hivi. Wale waliokulia sehemu zenye Ginery (viwanda vya kuchakata mazao yatokanayo na pamba ikiwemo mafuta ya pamba), wanaweza kushuhudia hili. Viwanda alivyojenga Mwl. vilisaidia sana nchi kutokuwa na matumizi makubwa sana ya fedha za kigeni katika kuagiza bidhaa toka nje ya nchi. Nchi yetu ilijitegemea kwa mambo mengi madogo madogo tofauti na ilivyo sasa. Tulizalisha mafuta ya kula, sabuni, nguo (Mwatex, Mutex), hapa hapa kwetu.
Maisha enzi hizo yalikuwa na "ladha" tofauti na ilivyo sasa.