Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Ujamaa/Ukomunisti ni LAANA kubwa sana hapa duniani.
Chini ya Sera, Fikra na Falsafa ya Ujamaa/Ukomunisti, inaamini kwamba Raia wote ktk nchi ni MATEKA wa Mwenyekiti. Katika msingi huu, kamwe raia hamuwezi kuwa na maendeleo na wala hamuwezi kuishi kwa furaha na amani, badala yake raia wataishi kama wapo jehanamu.
 
Mwalimu alikataa kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania kama alivyotakiwa kufanya na IMF na World Bank ili Nchi ikopeshwe pesa !
Hivyo akaamua ni bora ang’atuke kuliko ageuke jiwe kwa kukubali masharti ya wakubwa wa Dunia !!
 
Kama hata wasaidizi wake wa karibu hawakuuelewa huo ujamaa hata raia pia ilikuwa ni haki vile vile kutomuelewa.
 
Ujamaa unatendeka vipi kwenye hizo nchi ulizo taja ?

Na tafsiri ya ujamaa kwa Nyerere ilikuwa ipi ?
Namna bora kabisa ya utafiti ni participant observation. Ukiweza fika Japan au Slovenia au Ujerumani/Israel/Sweden; ongea nao, ishi nao, ona namna usoshalist ulivyo.
Sio kila kitu utaelewa kwa google au vitabu. Kuona na kuishi ni kupata real experience ya nini kinaendelea.
 
Kumbe ulikuwa unawaza Kama Mimi👇.
Kuna mda huyu bro anazinguaga kinyama.
Kiufupi huwa tupo smart,ila ila ninapowaza kuhusu siasa za chama chake na kufumbia baadhi ya Mambo ya hovyo na kusifia baadhi ya vitu ambavyo ni ukakasi kwa watu wengine huwa naumia Sana.
 
Umeshindwa kuelezea
 
Uzuri ni kwamba you will never be. Utabaki kuwa rais wa keyboard.
 
Ujamaa uko kinyume na asili ya binadamu ndiyo maana kote duniani umeshindikana ku impelement.

Ujamaa ni kugawana umasikini miongoni mwa jamii., kufanya matajiri wawe masikini na masikini wawe masikini zaidi
 
Mimi nawaza tu,mahali pa kuanzia ni kusafisha wasomi wanasiasa kwa damu na moto.
Hawa tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kutawala na wakatumia fursa hii kutuuza kwa matajiri wahuni wa ndani na nje.Wakatulazimisha tuwe na elimu inayotufanya watumwa wa wanasiasa na matajiri.
Nchi ikishatakaswa,ndipo tunaanza upya na akili mpya kama vile ndio kwanza tumepata uhuru
 
Kuna Mambo mazuri ya ujamaa na mabaya, hata ubepari una Mambo mazuri na yasiyofaa. Tatizo ni pale tulipovunja azimio la Arusha na kuwaruhusu viongozi kuwa wafanyabiashara. Hapo Kila kiongozi akiingia anawaza namna ya kupata Mali na njia rahisi ya kutajirika ni kupitia siasa.
 
Ujamaa umeshakufa toka miaka ya tisini baada ya kujunjika USSR na ukuta wa berlin. Nchi zilizokuwa namba moja katika ujamaa(China na Russia) leo hii ndo zinazozalisha mabilionea wa kibepari. Kosa letu ni bado tupo kijamaa ambapo serikali inapewa mamlaka kubwa. Lakini hao viongozi wa serikali hawana vigezo na sifa za kupewa haya mamlaka makubwa ya nchi. Tunatakiwa tuige nchi zilizoendelea kwa kuzipa vigezo kampuni na sekta binafsi. Tukiwapa sekta binafsi kipaumbele kwa kuwapa masharti ya kuwa na mazingira mazuri ya kazi. Na kutoa ajira kwa kiasi fulani tutafika mbali sana. Hii nchi magazeti yamejaa siasa, burudani na michezo. Tanzania iwape wawekezaji mazingira yaliyo bora kuliko. Unawapa tu masharti kuajiri watu 10000, halafu halipi hata senti ya kodi. Wewe kama serikali unapata hela kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Unakuta katika nchi yetu tuna mabilionea wa dola wameajiri watu bila bima ya afya wala mikataba na bado wanapata upendeleo wa kodi. System haitakiwi kumpa kipaumbele raisi na viongozi wa serikali. Mfumo inabidi upendelee kampuni na sekta binafsi. Huku ujerumani miji ambayo viwanda vipyo viwanda ndo vinasimamia maendeleo kwa asilimia kuda. Ukifika makao makuu ya Audi katika mji wa Ingolstadt. Audi ndo imejenga Uwanja wa mipira, Mall kubwa ya Westpark, Arena ya michezo mbali mbali. Pia Audi inandaa matamasha mbali mbali wanamuziki wanakuja kwa udhamini wao. Ukiwapa kipaumbele viongozi wa serikali katika media wanatumia hela za kodi ambazo ni za kwako wewe mwananchi. Lakini unapoipa kipaumbele sekta binafsi hawawezi kukuangusha maana wanalazimika kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinapatikana ili kuimarisha uzalishaji wao. Tungekuwa na sekta binafsi imara haya mafuriko ya Hanang makampuni mengi yangefika na ku solve matatizo. Lakini serikali inafika pale kufanya PR badala ya kusolve. Na hata kama wakitaka ku solve haya matatizo kuna maofisa wanataka kupiga hela na sio kusaidia. Huu ni mtazamo wangu kutokana na nilichoexperience.
 
UJAMAA NI MUHIMU SAANA
 
Uchumi wa kibepari sidhani kama unazuia serikali kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo ya nchi, ujamaa ni umasikini na kwa kiasi kikubwa ndio unaotuchelewesha, hata hizo nchi zilizoendelea kwa ujamaa kama China na Urusi hazina ujamaa huo tunaoutaka sisi
 
Yaani uturudishe kwenye ujamaa??? Hv unajua hata wachina wenyewe ujamaa umebakia kwenye makaratasi??? Mpk mchonga anaachia madaraka ni kutokana na kufeli kwa siasa za ujamaa
 
Ni ngumu Sana kumchomoa Mtakatifu Nyerere kwenye hii laana ya dhulma, yeye ndie alieasisi chama hichi kisha akawepo hadi kinapevuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…