John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Ujamaa/Ukomunisti ni LAANA kubwa sana hapa duniani.Amani iwe nanyi nyote.
Kwa wale wazee wenzangu mtakubaliana na mimi kwamba Tanzania ingekuwa mbali zaidi kimaendeleo endapo ingeendelea na mfumo wa Ujamaa chini ya chama kimoja kuliko ilivyo sasa.
Uchumi wetu ulianza kuyumba mara tu awamu ya pili chini ya Mzee Ruksa, Alhaji Ali Hassani Mwinyi ilipoingia madarakani na kuusaliti Ujamaa wa Hayati Mwl. JKN.
Hadi kufikia mwaka 1987, uchumi wa Tanzania ulikuwa unaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Hii ina maana uchumi wetu ulikuwa mkubwa kuliko hata wa Kenya ambayo ndiyo kinara kwa kuwa na uchumi mkubwa katika ukanda huu kwa sasa!
Miaka ya 1990 tulipokubaliana na mambo ya kipuuzi kama nchi, tukapoteana kabisa na hali yetu haijatengamaa mpaka kesho. Fedha yetu inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka huku kukiwa na pengo kubwa sana kati ya wenye nacho na wasionacho.
Hivyo ushauri wangu ni serikali kufanya kila linalowezekana kuturudisha katika mfumo wetu wa Ujamaa; Sera inayotutofautisha sisi na majirani zetu. Hii itasaidia kuleta ustawi kwa wote na kutuondolea kero ya kuwa na viongozi wezi na vibaka waliojificha kwa mavazi ya uongozi.
Asalaam Aleykum.
Chini ya Sera, Fikra na Falsafa ya Ujamaa/Ukomunisti, inaamini kwamba Raia wote ktk nchi ni MATEKA wa Mwenyekiti. Katika msingi huu, kamwe raia hamuwezi kuwa na maendeleo na wala hamuwezi kuishi kwa furaha na amani, badala yake raia wataishi kama wapo jehanamu.