Mkuu mambo kama haya unatukwaza baadhi ya watu.
Tunahisi unataka kutuingiza matatizoni tu tukiweka baadhi ya yanayo endelea huku mitaani kwetu.
Walichosema USA kama alivyo eleza
Kiranga kwa mujibu wa BBC world kinawezekana sana kina ukweli flani.
Hapa nilipo kwenye jiji kuu la kibiashara la nchi flani ndani ya bara la giza kuna hospital jirani ya taasisi binafsi. Mtu mmoja ndani kwetu alikuwa anataka kwenda kupata matibabu hiyo sehemu, jirani yetu akamwambia ndugu usiende hapo. Wale wauguzi wa hiyo hospital rafiki zangu walikuja jana hapa kwangu wakaniambia chonde chonde rafiki yetu kama hauumwi sana usiende hospitalini kwetu, kuna wagonjwa wawili wa COVID-19. Wao (hospital) walipiga simu namba maalum waje wachukuliwe lakini jamaa hawakuja.
Wakachukua hatua kuwapeleka wenyewe hospital flani ya serikali yenye kupokea kesi hizo wakakataliwa na kuambiwa wagonjwa wamejaa hawapokei wapya. Wagonjwa wakarudi nao kwenye hospital yao binafsi ndogo tu hapa mtaani.
Disclaimer: Samahani kwa kuweka habari ya nchi toka bara la giza wakati wewe na
Kiranga mnazungumzia hali ya DAR, siku nyingine nitakuwa makini kutochanganya habari. Nilijikuta tu nafananisha hali ya hii sehemu niliyosema na huko mnakozungumzia ndiyo maana nikaweka hapa huu mfano.
Makazi yangu ni hapa hapa panaposifika kuwa ugonjwa umeshamili. Kazi zangu nafanyia maeneo mbalimbali hapa mjini. Leo kkoo, kesho masaki, mtondogoo temeke. nk. Sijakutana kabisa na mgojwa au msiba unaohusika na covid moja kwa moja.
Kuna mambo mawili nayaona. La Kwanza, ugonjwa upo lakini hauna madhara km tuliyoyasikia kwa wenzetu huko Asia, Marekani na Ulaya. Kwa huku unawadhuru wenye maradhi mengine. Sukari, HIV, nk. Hasa wenye umri mkubwa.
La pili ugonjwa upo ila uambukizanaji wake tulidanganywa. Sio kwakugusana na mgonjwa wala kugusa alipogusa mgonjwa.
Ingelikuwa maambukizi yake ni km walivyobainisha WHO watu wa hali ya chini tungeisha. Anzia masokoni, kwenye mabar, boda boda
Tena hawa ndio wangeisha sana. Ukiwapigia muda wowote unamgojwa wanambeba bila hiyana hadi hospital.
Mwisho tufuate maelekezo ya wataalam. Vaa barakoa, nawa mikono na tujitahidi kukaa mbali mbali.