Usimsahau na
Kiranga
Ila niliwahi Kumuliza Head Of Psu Wa Sasa Wambura, Why Mnakuwa na tited security Sana Kwa Wakuu Wa Nchi, Akasema Wanataka Wao [emoji1][emoji1][emoji1]
Kwa nchi kama Marekani, rais kulindwa na walinzi wengi, hususan wanaoonekana waziwazi wameshika silaha kubwa za moto, ni suala la aibu.
Viongozi wanataka kuonesha picha ya kwamba Marekani ni nchi ya demokrasia, viongozi wana imani sana na usalama wao bila ya ulinzi mkali, wanapendwa na watu.
Hii dhana ina tija kwa kiwango fulani, lakini ikizidishwa ina madhara yake. Mfano mmoja ni mauaji ya rais John F. Kennedy, yaliyowezekana kufanyika kirahisi kwa sababu rais alikuwa kwenye gari ya wazi, kwa sababu alitaka kuwaona wananchi na wananchi wamuone, bila ya ulinzi mkubwa sana.Inasemekana walinzi wake walimshauri asipande gari la wazi, lakini rais Kennedy alikataa, akiamini hakuna tatizo la kiusalama.
Kwa kawaida marais wa Marekani wanahusisha ulinzi mkubwa, hususan wa silaha nzito zinazoonekana wazi, kuwa ni tabia za tawala za kijeshi, za kidikteta, zisizo na demokrasia, ambazo hazijiamini na zinapenda kutisha wananchi.
Binafsi sikupendelea muonekano wa kijeshi ulioanza kuingia serikalini kipindi cha Magufuli, kiasi cha kwamba si tu ulinzi wa rais ulikuwa kijeshi zaidi na walinzi kubeba silaha kubwa za moto, bali pia hata rais mwenyewe, ambaye si mtawala wa kijeshi, alipenda kuvaa magwanda ya kijeshi.
Sijawahi kumuona rais mwingine yeyote wa Tanzania kavaa magwanda ya jeshi bila kuwa vitani. Hata Kikwete ambaye alikuwa mwanajeshi.
Kuna picha chache tu za Nyerere amevaa kijeshi, hususan kimgambo, hususan wakati wa vita vya Kagera au operesheni maalum za kijeshi.
Marais walielewa kanuni ya "civilian leadership/ control of the military".
Uongozi wa kidemokrasia wa kiraia unaongoza jeshi, na taswira inayotolewa na uongozi inatakiwa kuwa ya uongozi wa kiraia.
Si wa kijeshi.
en.wikipedia.org