Nadhani hoja kubwa si ulinzi imara, ni ulinzi wa kitaalamu. Hao Marais wa Marekani ambako waliopita wengi wameuawa kuna 'intelligence' ya maana kwanza kabla kiongozi hajafika na wakati akiwa katika eneo
Nyerere alikuwa katika hatari kubwa sana nyakati za ukombozi ukizingatia akina Mondlane waliuawa hapa nchini
Ulinzi wa Nyerere ulikuwa wa kisayansi kiasi kwamba hakuwa anazungukwa na maaskari na bunduki bali usalama ulishapitiwa kabla na baada ya kufika eneo. Utakumbuka'' intelligence'' yetu ilivyokuwa nyakati hizi
Inashangaza sana , sijui kwanini alikuwa na ulinzi wa namna ile.
Ulinzi wa kuzungukwa na mabunduki na makundi ya watu ni wa karne ya 18. Ni ulinzi wa kijima sana.
Anwar Saadat aliuawa katikati ya kundi la Walinzi. Ndivyo ilivyokuwa kwa viongozi wengi miaka ya nyuma
Zama za teknolojia matumizi ya akili ni muhimu sana kuliko uwepo wa makundi yenye mibunduki
Jamaa alikuwa ana exaggerate kila kitu , alitaka tu kuonekana ni mtu special sana duniani.
Hakukuwa na sababu ya Helikopta ikiwa alisimama hovyo barabarani na kuhutubia.
Katika vitu vinavyokera ni Protokali ya kuhutubia. JPM alibadilisha namna kiongozi anavyotoa hotuba
Siku hizi kila anayesimama anaanza kuwatambua wageni waliopo. Ni makosa makubwa sana
Viongozi waliopo wanatambuliwa mara moja wakati wa kuanza kwa shughuli.
Viongozi wanaofuata wanamtambua mgeni rasmi kwa kumu address 'Mh Rais' au VP au PM
Rais anatambulishwa uwepo wa viongozi, si kazi ya Rais kuwatambua kwasababu walishatambuliwa
Nyerere, Mwinyi, Mkapa walianza hotuba kwa kutambua mwenyeji wa shughuli.
Hakuna sababu ya kusoma majina ya kila kiongozi katika jukwaa kuu
Halafu Rais atambue viongozi wakuu kwa makundi.
Mfano akimtambua waziri mkuu tayari ameshtambua uwepo wa Mawaziri.
Ukimtambua CDF umeshatambua vyombo vya ulinzi na usalama. Hakuna sababu ya kutambua TISS,Polisi n.k.
Wanaoandaa hotuba ya Rais waliangalie hili. Rais anatambua mwenyeji kisha viongozi kwa ujumla wao na wananchi. Si kazi ya Rais kutaja kila mtu aliyekuwepo. Hili alianzisha JPM na sasa linaendelea bila kujua kuna tatizo
Pascal Mayalla