Tanzania tuna tatizo la wataalamu

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Ukiongea na wananchi wa kawaida wana lalamika kuna wasomi wengi sana hawana kazi. Ukiongea na wataalamu wanalalamika hakuna watu wa kutosha wenye ujuzi na taaluma za kazi. Kuna Mtanzania Dr Mushi alifanya PHD yake kwenye hili na link ya kitabu chake iko hapo. Je ni kweli kuna tatizo la wataalamu? Na tufanye nini kutatua hili tatizo

Pascal Mayalla Zitto

Nimeona hii kuhusu kenya

Kitabu kiko amazon
Amazon product ASIN 0739165550
 
Wataalamu mimi naona tunao lakini njia sahihi za kuwatumia ndio changamoto kubwa ktk nchi yetu, mfano mdogo tu tuna stesheni ngapi zilizo andaliwa kwaajili ya utafiti wa mbegu bora za kilimo/mifugo? ujenzi gani mkubwa tulioufanya hapa nchini wataalamu wetu wakapewa nafasi watumikie ujuzi wao? wapewe nafasi, wajivunie taaluma zao hapo tutajivunia wataalamu wa nchi yetu.
 
Elimu,elimu,elimuu.

Wataalam tunao Ila asilimia kubwa utaalam wao upo kwenye vyeti na sio skills,elimu yetu ni yakukariri(darasani) zaidi kuliko vitendo. Angalia miradi mingi iliyosimamiwa na wataalam wetu life span yake ikoje na bajeti yake ya utekelezaji wa miradi.

Kama kweli tunahitaji kubadilika tuanze kubadili mitaala yetu kwanzia ngazi ya awali,tupate watu sahihi watakao jifungia kutuandalia mitaala mipya itakayo endana na ulimwengu wa sasa.

Mwisho zitungwe sheria kali zitakazo wakafunga vifungo na adhabu pale watendaji wanapovurunda au kuhujumu miradi,taifa limeharibika sanaa upigaji now kimekuwa kitu cha kujivunia,yaan daraja la billion 5 tunaambiwa billion 70 na watu wanaona poa tu.
 
Kauli za mabeberu hizi zenye lengo la kutunyongesha.

Kuna Mtanzania ambaye kafanye PHD yake na uchunguzi kwa zaidi ya miaka 3 naye ni beberu nunua kitabu chake halafu tueleze hapa ni nini hasa sio cha kweli. Tusipende kutokujituma na majibu rahisi rahisi tu hili ndilo tatizo letu! Kila kitu mabeberu🤔
 
Kuna Mtanzania ambaye kafanye PHD yake na uchunguzi kwa zaidi ya miaka 3
Hawa wala usiwaamini mkuu. Wamekopi na kupesti maneno ya mabeberu ili waipate hiyo unayoiita PhD.

Wenye PhD wako wengi nchi hii lkn hawana tija yoyote kwenye hili taifa zaidi ya kumiliki karatasi ngumu wanazoziita vyeti.
 
Ktabu ni takataka ni theory kibao kama unasoma majarida ya nje utajua tu...Hapa bongo hao PhD ni kama afya tu kama utaendlea kusoma mpaka uzeeni utapata tu.. article nyingi hta lugha unajua ni copy and paste na kuunganisha idea hata Yale maneno unaona togolani mavura anatweet kule twitter ni ideas za vitabu kama hujui.
 
Hakuna mwenye PhD wala professorial rank nchi hii. Ndiyo maana tangu dunia kuumbwa hata kijiti cha kuchokonolea meno au kiwembe hakijawahi kutengenezwa hapa nchini.

Au hata dawa ya chooni au kidonge cha kuua mende.

Bure kabisa
 
😂😂😂😂
 
Unamaliza chuo unakuja pata kazi baada ya miaka 5. Hapo umeshafanya kila aina ya kazi kuanzia boda boda mpaka ukuli lazima elimu i expire

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mwenye PhD wala professorial rank nchi hii. Ndiyo maana tangu dunia kuumbwa hata kijiti cha kuchokonolea meno au kiwembe hakijawahi kutengenezwa hapa nchini.

Au hata dawa ya chooni au kidonge cha kuua mende.

Bure kabisa
Unatuonea mkuu, kwamba nchi yetu bure kabisa

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mwenye PhD wala professorial rank nchi hii. Ndiyo maana tangu dunia kuumbwa hata kijiti cha kuchokonolea meno au kiwembe hakijawahi kutengenezwa hapa nchini.
Mkuu, Kwani kutengeneza vitu kama toothpicks, wembe.. lazima umiliki PhD?!
Kama we umeona hiyo fursa kwanini usitengeneze?
 
Watalaamu wanatengezwa nadhani hakuna sera ya kuendeleza watu katika nafasi mbalimbali zilizopo.
 
Mkuu, Kwani kutengeneza vitu kama toothpicks, wembe.. lazima umiliki PhD?!
Kama we umeona hiyo fursa kwanini usitengeneze?
Watu wanazani mambo yanaishia kwenye kutengeneza tu. Kuna kuiuza hyo product na kupata revenue hapo ndo pana mtihani.

Jiulize Jamii forum imeanzishwa 2006, Facebook imeanzishwa 2004, na instagram imeanzishwa 2010.

Jaribu kuangalia jinsi hyo mitandao ilivo kua na kuendelea mpaja sasa hivi. Na angalia tunavo strugle na JF.

Maendeleo hayaishii kwenye ujuzi tu kuna kitu kinaitwa Sera, kama hakuna sera wezeshi hakuna kitu kitaenda smooth.

"If the policy aren't good the agriculture cannot be right"

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Hawa wala usiwaamini mkuu. Wamekopi na kupesti maneno ya mabeberu ili waipate hiyo unayoiita PhD.

Wenye PhD wako wengi nchi hii lkn hawana tija yoyote kwenye hili taifa zaidi ya kumiliki karatasi ngumu wanazoziita vyeti.

Huu mtandao wa hoja sio vihoja. Tuletee data zako ni wapi hasa haukubaliani nao kama huna data tunashauri uwende page ya udaku au mapenzi “sexless”
 
Mkuu, Kwani kutengeneza vitu kama toothpicks, wembe.. lazima umiliki PhD?!
Kama we umeona hiyo fursa kwanini usitengeneze?
Nilitegemea wasomi wawe wa kwanza kuiona fursa hii. Msomi ni mtu anaueyatawala mazingira na changammoto zake.

Lkn ndiyo wanaoongoza kulia lia kuhusu ajira. Wakati ndugu na jamaa zao waliowaacha bijijini wakipambana kimya.

Haya ni maajabu yanayosubiriwa kuwekwa kwenye kitabu cha Guinness
 
Huu mtandao wa hoja sio vihoja. Tuletee data zako ni wapi hasa haukubaliani nao kama huna data tunashauri uwende page ya udaku au mapenzi “sexless”
Unachokitaza hata wewe hujakifanya. Nilitarajia wewe msomi ungetuwekea takwimu hapa ili sisi akina Sexless tuondokane na hii dhana ama fikra potofu.

Wasomi gani nyie mnaojitambulisha kwa majina yenu kuanzia na Dr. tu badala ya kujitambulisha kwa umuhimu wa kazi zenu kwenye jamii?

Bure kabisa.
 
Ingawa chapisho lake ni la muda mrefu ,lakin tatizo hilo lipo na ni kubwa sana.Tatizo hilo linasababishwa na serikali kutowapatia mafunzo kwa vitendo watumishi wake wengi.Mfano madaktari wengi wa Tanzania wamesoma kwa Kiasi kidogo sana.Jaribu kupata ajali uone au Jaribu kuugua mqgonjwao Kama figo uone.Bado utaona madaktari wetu walioshindwa kutoa uduma zinazotakiwa kutokana na kwamba wamesoma kidogo sana.
 
Takwimu zipo kwenye kitabu acha uvivu kasome. Vijana wa siku hizo uvivu mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…