Tanzania tunatarajia kuzalisha MW 5,000 mwaka 2025

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Leo katika hafla ya utiaji saini mikataba yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.9 ya kuongeza usambazaji wa umeme kwa wananchi na maeneo ya kimkakati. Waziri wa Nishati January Makamba alisema Serikali inamkakati wa kuongeza uzalishaji umeme "Tunaposema tunazalisha umeme wa Megawati 1,700 na tunaona unatosha hautoshi, ni kwamba tu haujawafikia wahitaji. Ukiwafikia wahitaji umeme tulionao ni mdogo mno"

Hivyo Serikali imejipanga kuzalisha umeme MW 5,000 ifikapo 2025 amesema "Tutafika Megawati 5,000 mwaka 2025, itakuwa ni zaidi ya mara tatu ya umeme uliopo leo."

Umeme utaenda kufufua fursa nyingi zaidi vijijini kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha vijiji vyote Tanzania vinaendelea.
 
Kuna harufu ya samaki aliyeoza kwa rushwa hapa. USSR
 
Safi sana,inamaana ndani ya miaka ya Rais Samia ukiacha bwawa la Nyerere ataingiza kwenye Gridi megawatt zingine 1000.

Safi sana sio Jiwe maika yote anaimba habari za Stiglaz
 
UWONGO UWONGO.
Uongo tena ,wivu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Muwe na akili megawatt 5,000 zitatoka huku,

Za Sasa 1600,
Nyerere 2115,
New 1300 kutoka gas na vyqnzo vinginevyo kama upepo,joto Ardhi nk
 
Ifikapo 2025 Tanzania itakua kama Ulaya kila kona umeme Mungu ampe maisha marefu Rais wetu aendelee kuupiga mwingi
 
Hizi hadithi zilianza kusikika tangu Mubongo akiwa waziri
 
Leo katika hafla ya utiaji saini mikataba yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.9 ya kuongeza usambazaji wa umeme kwa wananchi na maeneo ya kimkakati. Waziri wa Nishati January Makamba alisema Serikali inamkakati wa kuongeza uzalishaji umeme "Tunaposema tunazalisha umeme wa Megawati 1,700 na tunaona unatosha hautoshi, ni kwamba tu haujawafikia wahitaji. Ukiwafikia wahitaji umeme tulionao ni mdogo mno"

Hivyo Serikali imejipanga kuzalisha umeme MW 5,000 ifikapo 2025 amesema "Tutafika Megawati 5,000 mwaka 2025, itakuwa ni zaidi ya mara tatu ya umeme uliopo leo."

Umeme utaenda kufufua fursa nyingi zaidi vijijini kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha vijiji vyote Tanzania vinaendelea.
Huyu jamaa amepofushwa kabisa na tamaa ya upigaji haoni kitu kingine chochote tena ndani ya akili zake..

Hiyo Megawati 5,000 ifikapo 2025 imeshindiliwa akilini mwake kama maandishi ya msahafu, wala hawezi tena kuchambua chochote juu ya uhitaji huo kwa wakati huo!
Hii yote ni kutegemea kwamba vikampuni vyao vya mfukoni vikiwategemea watu toka nje watakuja kuwanyonga waTanzania kwa bei mbovu za mikataba watakazoingia nao katika uzalishaji wa umeme wa bei mbaya, huku wakitumia raslimali zetu, kama jua , upepo na gesi.

Hili kundi la viongozi hawa ni maadui wakubwa wa nchi hii.
 
..isijekuwa ni IPTL nyingine.
Chini ya hawa watu, tegemea zaidi ya IPTL; changanya humo na hao wa gesi waliotutia adabu hivi karibuni mahakamani.

Hii wizara chini ya Makamba na Bodi yake, sijui kama tutasalimika.
 
Uongo tena ,wivu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Muwe na akili megawatt 5,000 zitatoka huku,

Za Sasa 1600,
Nyerere 2115,
New 1300 kutoka gas na vyqnzo vinginevyo kama upepo,joto Ardhi nk
Sasa hizo 1,300 mpya, ndizo zitakazotuletea shida kubwa, kwa sababu zote ni kutoka kwa vikampuni vya mifukoni vya hao hao akina Makamba, na mikataba yao ya kutuuzia hizo 1300 ndizo zitakazotunyonga kwa bei zao mbaya kabisa.

Ukitaka kujua uhujumu huu unaopangwa na hawa watu, usiende mbali; nenda tu hapo jirani yetu Kaskazini.

KenGen wanazalisha na kuuza umeme kwa bei ya chini kabisa; lakini unapochanganya na bei za hao wazalishaji wengine wenye vikampuni vyao, umeme unakuwa ni wa ghali sana.
Hivi karibuni walipoambiwa wapunguze bei, wakagoma na serikali ikaufyata!
 
Leo katika hafla ya utiaji saini mikataba yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.9 ya kuongeza usambazaji wa umeme kwa wananchi na maeneo ya kimkakati. Waziri wa Nishati January Makamba alisema Serikali inamkakati wa kuongeza uzalishaji umeme "Tunaposema tunazalisha umeme wa Megawati 1,700 na tunaona unatosha hautoshi, ni kwamba tu haujawafikia wahitaji. Ukiwafikia wahitaji umeme tulionao ni mdogo mno"

Hivyo Serikali imejipanga kuzalisha umeme MW 5,000 ifikapo 2025 amesema "Tutafika Megawati 5,000 mwaka 2025, itakuwa ni zaidi ya mara tatu ya umeme uliopo leo."

Umeme utaenda kufufua fursa nyingi zaidi vijijini kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha vijiji vyote Tanzania vinaendelea.
Uongo
 
Back
Top Bottom