Usishangae kuona hivyo. Tambua yakuwa USD ndio means of exchange ya biashara na miamala ya kimataifa. Dollar economy ndiyo inatawala dunia, hakuna TZS, ¥, €, £, Yuan, Russian rubble etc. BOT wanasimamia miamala yote na miamala ya kitaifa inatakiwa itumie TZS, ila miamala ya kimataifa lazima tutumie USD na BOT hawawezi kulazimisha matumizi ya TZS katika miamala ya kimataifa. Hii ni kwasababu ya dollar economy/ dollar supremacy.
Warusi wenyewe wanaangaika kuipiku dollar economy baada ya kuwa wanawekewa vikwazo Mara kwa Mara pia wanapotumia USD wanaimarisha zaidi fedha ya marekani. wamejitahidi ila wapi, na Unaijua urusi ni taifa kubwa kiuchumi, kijeshi, kiteknolojia nk... ila hawawezi kuondoa dollar supremacy sasa wewe unataka tuiondoe eti kwa sababu hatutumii bidhaa nyingi kutoka marekani, unafikiri tutaweza???
Huku TZS inaporomoka thamani kila siku ingawa BOT wanajitahidi kusimamia matumizi ya shilling katika miamala ya ndani. Ila bado wafanyabiashara wanapendelea USD kwasababu inanguvu na inaimarika kila siku kuliko TZS. Bado ukienda kwenye mabenk ukiweka fixed deposit kwa fedha ya kigeni hususani UK pounds, Euro, USD unapata interest kubwa kuliko kuweka kwa TZS ndo maana kuna watu wanasema TZS ni fedha ya madafu . Kwahiyo usishangae kuona watu wanapenda USD.