Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

Mkuu wakati unatupa nasaa sio mbaya ukatupa na connection pia mtaani hali sio shwari kutoboa bila kushikwa mkono ni mtiti
 
Cha ajabu sana ni kwamba matajiri wote duniani wamejiajiri, sijawahi kusikia tajiri aliyeajiriwa serikalini... [emoji23] [emoji23]
Matajiri wa duniani Hawajajiajiri... Wameajiri watu. Know the difference.

Kuna tofauti kati ya Kujiajiri na Kuajiri wengine wakufanyie kazi. Mada inazungumzia Waliojiajiri vs Waajiriwa, haizungumzii walioajiri watu.
 
Wewe unayefungua biashara mpaka jumamosi na jumapili ili uuze uingize hela na muajiriwa anayepumzika weekend nzima, nani yupo kwenye slavery machine?
Soma ulichoandika.
Inaonesha unawaza weekend tu hapo ulipo.
 
Saana yaani serikalini haijalishi upo wapi ila kuna mseleleko sana pia kuna uhakika wa mambo tofauti na kujiari.. na ndio maana kupata kazi huko ni mtiti mwingine
Hicho unachoita mselekeko kiuhalisia ni kwamba watu huko ni wazembe, hawafanyi kazi kwa ufanisi, wezi na wategeaji. Ikitokea serikali ikaja na mfumo mpya wa watu kufanya kazi kwa masaa na clear daily targets, kuajiri kwa sifa na elimu stahiki, basi ujue wengi watakimbia na kufukuzwa kazi. Sasa hivi mtu anaingia kazini saa 1.30 asubuhi anawahi kusaini kitabu but ukifuatilia muda productive alioutumia kwa siku pengine 2 hrs tuu...
 
Kujiajiri inahtaji roho ngumu Sana , juhudi na uvumilivu , ni kweli Kwa miaka 15 ya Kwanza aliyeajiriwa atakula bingo Ila baada ya hapo hampati aliyejiajiri hata robo Labda aliyejiajiri awe Fala
Hivi watanzania milioni zaidi ya 60 wanaweza kweli kuajiriwa na serikali?? Hivi unajua mpaka sasa watanzania walioajiriwa na serikali hawazidi hata milioni 3??
 
[emoji23] [emoji23] na ukiongezea huwa wanajisahau sana na kubweteka wakiwa kazini...
 
Hata aliyeajiriwa anakua pia. Kuna annual increment (japo ni ndogo), kuna kupanda cheo.. kuna kuhama taasisi kuhamia taasisi inayolipa zaidi etc.
Wakati naanza kazi serikalini huko Morogoro watu kama akina Aziz Abood walikuwa wakiuza duka na baba yao, akina Makundi (BM) walikuwa maduka ya kawaida kabisa, na wengine wengi tuu... Lakini nikiangalia walipo sasa daaah aiseeee.. Ila hata biashara au kujiajiri kama huna nudhamu hutoboi...
 
Hawa walio ajiriwa serikalini ni wanyonyaji wakubwa. Ndio maana bado Tanzania kuna umasikini mkubwa. Sababu wakulima, wafanya biashara wakubwa na wadogo, hata wanaosota bila kipato wote wanakamuliwa na hawa waajiriwa serikalini.
Ufanisi hakuna, ndio kizuizi cha maendeleo, rushwa mbele, na bado kila leo wanalia nyongeza na kupandishwa vyeo.
 
Aliyejiajiri akumwa utamuonea huruma hata Bima ya Afya hana

πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Ukiwasikia sasa mtaani maisha yakiwapiga
1. Kuajiriwa ni utumwa
2. Kuajiriwa unakosa uhuru- wakati anaamja saa kumi na moja asubuhi anarudi saa nne usiku- kuna uhuru gani hapa

Hawajiulizi Nikki wa Pili akiona wivu kwa wanaaheria wanapiga michongo ya pesa ndefu huku yeye alisoma masters ya sociology kakosa ajira alianza nyimbo za kuwananga walioajiriwa akaja na wimbo wa

  • Mimi sitaki kuajiriwa
  • Sitaki kutumwa natama kujituma
  • Sitaki kazi, sitaki kuajiriwa

Alipopata upenyo wa DC hakugeuka nyuma na music akatupa kule.

We huoni Mtoto waMjini na michongo yake kaamua kuwa mtumishi wa Umma Ms Jokate?

Chawa woote wanatafuta ajira serikalini.
90% workforce Tanzania ni walojiajiri kwenye kilimo, machinga, chips, dagaa na samaki, bodaboda na mitumba wamechoka vibaya mno.
 
Kanuni ni ile ile tu kama huwezi kuperfom kwa nidhani ukiwa umeajiriwa hutopata hiyo nidhamu ukiwa umajiajiri never.
 
Ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…