Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Hakimu Mfawidhi, Kwa hapa Tanzania na hali ilipofikia sidhani kama mwezi wa tano maambukizi yatapungua, ndio kwanza yatazidi zaidi sababu hakukuwa na hakuna hatua madhubuti.

Mitaani watu wamekaa kiboya sana bila tahadhari wanacheza pool, kunywa pombe na kutembeleana hovyo, kula hovyo njiani na kwenye daladala mtu bado anakula mahindi ya kuchoma!

Huo mwezi wa tano vifo ndio vinaweza kuwa vingi zaidi tusipochukua hatua.
 
Sibonike, Idadi ya 54 ndo idadi nzima ya wa athirika wote nchini Uganda sisi tumewapata siku moja wenzetu wako lock-down hi wiki ya tatu na wameongezewa wiki tatu zingine wakati sisi bado tunadunda tuko bize kusali duh......' now who is fooling who'?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_3703.JPG


Huku Zanzibar mitaa inaanza kuisha mana kila cku takwimu za mitaa mipya wagonjwa wa ndan na ni sehem za walala hoi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
I trully believe chanzo cha maambukizi kusambaa hapa Tanzania yanatokana na PSV vehicles--hasa z mikoani--almost 200 buses zinatoka Dar heading mikoani kila siku.

Assume kila bus ina muathirika mmoja,na kila bus linabeba watu 50max. by chance--wakaambukizwa watu wawili tu kwenye kila bus--ina maana waathirika wapya 100 kwa siku moja.

And the chain continues--Tutaishaaa--DAB azuie movement ya mabasi ya mikoani.
Watu wakae makwao--mizunguko ipungue.

Wale wanaotoa tiba mbadala nao huu ndio wakati wa kuonyesha makeke yao--it's very possible Dawa ipo hapa hapa kwetu.

Mshana Jr ,Unaijua Sokonoi(Dawa ya kimasai?),pia zile wanazofukizwaga kule upareni--tusaidiane tupone.
 
Endeleeni kusali huku mkijazana Bar,misikitini,kanisani,sokoni,mitaani,kwenye daladala. Mtakufa tutarithi ardhi zenu tule maisha .
 
Ukitoa shule na vinyozi kila kitu kinaendelea, baadhi ya sehemu wamepunguza masaa ya kazi. Mawazo yangu, dunia nzima inaua sisimizi kwa nyundo.
kwa nini mzee??.club na mabaa yapo wazi? kama yapo wazi basi inaonekana huko corona sio issue kubwa kihivyo

Hittin Blunts and Bustin Nuts
 
Kama Taifa tumeamua kumuamini Mungu na kuchukua tahadhari zilizo ndani ya uwezo wetu ili kuepusha majanga mengine mimi nikiwa kama muunini ninaye amini uwepo wa Mungu kupitia haya maombi ya siku tatu ambayo Mh. Raisi ametuomba tufunge na kusali naimani Mungu atatuonekania muda sio mrefu.

Mungu hajawahi shindwa na kamwe hatoshindwa, tuchukue tahadhari tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima tuoshe mikono yetu kisha tumwache Mungu ajidhihirishe.
 
We,,,huu ugonjwa unatesa,,Kuna watu wanakaa hata mwezi,wanahangaika nao tu,,
Hivi mwanaFA alipona?
 
Piga pini Dar hamna kutoka wala kuingia (ingawa wao wenyewe km nilazima waendelee na hicho kinachoitwa kuchapa kazi ndani ya dar yao).

Piga pini zanzibar(hamna kutoka wala kuingia) ikiwezekana lockdown kabisa wafe kwa njaa huko ndani).

Hii miji miwili imeshakuwa kitovu cha korona kitaathiri nchi nzima kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.
Tupe wiki mbili,utafurahi
 
Kuna maambukizi ya weekend ya pasaka ndiyo yatavunja rekodi,,,huu ugonjwa haubagui dini ,umri wala jinsia japo wanaume tunakufa zaidi . Naombea hata viongozi wetu wakuu walipe bei ya huu ugonjwa .
 
Kama Taifa tumeamua kumuamini Mungu na kuchukua tahadhari zilizo ndani ya uwezo wetu ili kuepusha majanga mengine mimi nikiwa kama muunini ninaye amini uwepo wa Mungu kupitia haya maombi ya siku tatu ambayo Mh. Raisi ametuomba tufunge na kusali naimani Mungu atatuonekania muda sio mrefu.

Mungu hajawahi shindwa na kamwe hatoshindwa, tuchukue tahadhari tuepuke mikusanyiko isiyo ya lazima tuoshe mikono yetu kisha tumwache Mungu ajidhihirishe.
Kuna siasa hapa inafanyika in the name of prayers.

Ufahamu na maarifa ndio nguvu ya msaada anayoitumia Mungu kufanya kazi zaidi katika majira na kipindi tunachokiishi ili kukabili changamoto zinazotuzunguka.

Himizo hili la kufunga na kuomba likiambatana na maamuzi ya kiimani yanayotokana na maarifa na uzoefu juu ya njia ya kujikinga na janga hili la dunia as medical emergency, hakika litafaa sana:

Haingii akilini Kama tunahitaji msaada wa Mungu hali Yale yaliyo ndani ya uwezo wetu hatutaki kuyafanyia maamzi.

Mbona bado tunaruhusu safari za mikoani?

Mbona bado tunaruhusu Bar, hotel, kumbi za starehe kuendelea na shughuri Kama kawaida?
Mbona hakuna udhibiti katika usafiri wa umma (public transport)?

Mbona hakuna hatua za kuzuia makusanyiko hasa katika maeneo ya biashara hasa masoko, minada na supermarket?

Mbona makusanyiko ya kiibada bado tunaruhusu?

Mbona tumeshindwa kufanya total lock down?

Kama hatua za social distance zinetushinda hakuna namna tunaweza kuhepuka athali za janaga hili.

Tukiruhusu maambukizi yaendelee kwa sehemu kubwa ya population lazima tuwe na uhakika gharama walizolipa mahala pengine duniani vikiwemo vifo vyetu sis, ndg na jamaa zetu lazima vitatokea tu.

Najua tutachagua kuvitangaza au lah ila kikombe hiki tutakinywea.

NOTE:

Moja ya maombi yetu iwe kumuombea Rais wetu na viongozi wa serikali ,Mungu awape ujasiri wa kufanya maamuzi magumu ili kulinda maisha ya watanzania.

Kutoogopa hofu ya lock down hiyo pia ni sehemu ya imani thabiti.

Mungu atupe ujasiri na maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom