Safi sana kwa wakuu wote mliotuletea
picha nzuri zenye mvuto hasa zikitukumbusha
kipindi hicho Nchi ilikuwaje?

Japo picha zote na miaka uliyoweka nilikuwa
sijazaliwa lakini nimejifunza kitu kwamba
enzi hizo kulikuwa hakuna ubaguzi wa
wenye nacho na wasio kuwa nacho.

Nimeangalia hapo hasa hayo magari sijui
yalikuwa ya aina yake.
 

.....Aiseee kumbe wazee wetu na vijana mlifaidi sana maisha wakati wa ujana wenu,maana mji msafi,hamna ghasia wala fujo wala vibaka kama tuonavyo sasa,mijini tumejazana zogo tupu hata wasichana walikua warembo na wanajiheshimu kuliko wa sasa.kulikiua hamna mafisadi kila mtu alikua anaipenda Nchi yake,naomba hizo enzi zirudi ingawa si rahisi
 
Wabongo wa Dar Es Saaam wakiwa na pembe za ndovu mwaka 1880

 
Hawa ni wafungwa wa kike wakiwa wamefungwa kwa minyororo wakifanya kazi za jamii (community work) za kusafisha barabara Dar Es Salaam mwaka 1890. Haijulikani walikuwa wamefanya makosa gani mpaka kufungwa gerezani. Picha kwa hisana ya Library of Congress.

 
Henry Stanley akisalimiana na Dr. David Livingstone kwenye kijiji kimoja Ujiji mwaka 1872. Wasaidizi wa Stanley wamesima upande wa kushoto na mmoja wao katikati akiwa amebeba bendera ya Marekani. Livingstone amesimama upande wa kulia akiwa pamoja na waarabu na wanavijiji kwa nyuma kidogo. Picha kwa hisani ya Library of Congress.


 


Hili ni bango lilitengenzwa na kupigwa picha mwaka 1918. Linaonyesha portrait ya Gavana wa Tanganyika Schnee (kuanzia 1912 hadi 1918) pamoja na nakala ya barua aliyoaindika kwa Kijerumani akitoa amri ya kutokomeza Uislamu kwenye bara la Afrika.

Kwenye bango hilo utaona picha mbili za Fort Mosi, sijui zilipigwa Moshi, Tanganyika?, sehemu ambayo Waingereza waliikuta barua hiyo ya Gavana Schnee.

Hiyo lugha ya Kichina kwenye bango inafafanua mpango na shughuli za Mjerumani katika kukandamiza uislamu Afrika.

Pia kwenye bango hilo kuna barua iliyoandikwa na Mmarekani Vice Consul akiwa Nanking, ikifafanua kuwa bango hilo lilisambazwa na Kamati ya Propaganda ya Kiingereza na lilikusudiwa kuwapa tahadhari waislamu wa Kichina kuhusiana na uongo na usaliti wa Mjerumani. Picha na maelezo kwa hisani ya Library of Congress. cc. FaizaFoxy
 
Hapa ni njiani karibia na Mount Meru kuelekea Arusha kama ilivyoonekana mwaka 1936.

Enzi hizo locals wa anga hizo walikuwa na kitu kinachotwa "Sunday Beer Party" kama wanavyoonekana kwenye picha.

Sijui kama bado huu utamaduni upo. cc. Arushaone, PakaJimmy

Picha kwa hisani ya Maktaba ya Congress.


 
Msichana wa Longido akiwa amejipamba masikioni, shingoni, na mikononi mwaka 1936.


 
Mount Meru mwaka 1936. Umebadilika au bado upo vile vile?

 
Kuelekea Ngorongoro Crater mwaka 1936



Ngorongoro crater
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…