Tanzania ya enzi hizo katika picha
Safi sana kwa wakuu wote mliotuletea
picha nzuri zenye mvuto hasa zikitukumbusha
kipindi hicho Nchi ilikuwaje?

Japo picha zote na miaka uliyoweka nilikuwa
sijazaliwa lakini nimejifunza kitu kwamba
enzi hizo kulikuwa hakuna ubaguzi wa
wenye nacho na wasio kuwa nacho.

Nimeangalia hapo hasa hayo magari sijui
yalikuwa ya aina yake.
 
View attachment 74223
Hapa Ni Tanzania Elimu Supply(TES) Enzi Hizo 1947

View attachment 74224
Mabasi ya Ekarusi Kumbakumba kwa nyuma Azania Front

View attachment 74225
Tanganyika Parkers Enzi Hizo 60s

View attachment 74226
Salender Bridge 1960s

View attachment 74227
Dar-Es-Salaaam 1975 Hiyooooo!!!

View attachment 74228
Seaview-Mawingu House 1960

View attachment 74229
Arusha-Clock Tower 1966

View attachment 74230
Dodoma City Center 1974

View attachment 74231
Bukoba City Center 1972

View attachment 74232
Jengo La CCM Likiwa Linajengwa Enzi Hizo

View attachment 74233
Korogwe Hotel

View attachment 74234
Same Hotel

View attachment 74235
Musoma 1960

View attachment 74236
Handeni Bomani Enzi Hizo

View attachment 74237
Shule Ya secondary Kisutu 1975

View attachment 74238
Iyunga Secondary 1966

Tupia Nyingine na wewe kama Unazo za Enzi Hizo za Popote pale ndani ya Tanzania::::Kumbukumbu ya Miaka 51 ya Uhuru::09 Dec 2012

.....Aiseee kumbe wazee wetu na vijana mlifaidi sana maisha wakati wa ujana wenu,maana mji msafi,hamna ghasia wala fujo wala vibaka kama tuonavyo sasa,mijini tumejazana zogo tupu hata wasichana walikua warembo na wanajiheshimu kuliko wa sasa.kulikiua hamna mafisadi kila mtu alikua anaipenda Nchi yake,naomba hizo enzi zirudi ingawa si rahisi
 
Dar es salaam harbour 1955
4551437928_d1b44bbd18_o.jpg

Daaaaar ilikua enzi hizo check green hyo!!! Son of Alaska umetisha kwa exclusive photos!! Miaka 52 ya Uhuru maisha magumu,ufisadi wa kutisha,wezi ndio watawala!!
 
Last edited by a moderator:
Wabongo wa Dar Es Saaam wakiwa na pembe za ndovu mwaka 1880

3c02973r.jpg
 
Hawa ni wafungwa wa kike wakiwa wamefungwa kwa minyororo wakifanya kazi za jamii (community work) za kusafisha barabara Dar Es Salaam mwaka 1890. Haijulikani walikuwa wamefanya makosa gani mpaka kufungwa gerezani. Picha kwa hisana ya Library of Congress.

3b38289r.jpg
 
Henry Stanley akisalimiana na Dr. David Livingstone kwenye kijiji kimoja Ujiji mwaka 1872. Wasaidizi wa Stanley wamesima upande wa kushoto na mmoja wao katikati akiwa amebeba bendera ya Marekani. Livingstone amesimama upande wa kulia akiwa pamoja na waarabu na wanavijiji kwa nyuma kidogo. Picha kwa hisani ya Library of Congress.


18647r.jpg
 
3g11304r.jpg


Hili ni bango lilitengenzwa na kupigwa picha mwaka 1918. Linaonyesha portrait ya Gavana wa Tanganyika Schnee (kuanzia 1912 hadi 1918) pamoja na nakala ya barua aliyoaindika kwa Kijerumani akitoa amri ya kutokomeza Uislamu kwenye bara la Afrika.

Kwenye bango hilo utaona picha mbili za Fort Mosi, sijui zilipigwa Moshi, Tanganyika?, sehemu ambayo Waingereza waliikuta barua hiyo ya Gavana Schnee.

Hiyo lugha ya Kichina kwenye bango inafafanua mpango na shughuli za Mjerumani katika kukandamiza uislamu Afrika.

Pia kwenye bango hilo kuna barua iliyoandikwa na Mmarekani Vice Consul akiwa Nanking, ikifafanua kuwa bango hilo lilisambazwa na Kamati ya Propaganda ya Kiingereza na lilikusudiwa kuwapa tahadhari waislamu wa Kichina kuhusiana na uongo na usaliti wa Mjerumani. Picha na maelezo kwa hisani ya Library of Congress. cc. FaizaFoxy
 
Hapa ni njiani karibia na Mount Meru kuelekea Arusha kama ilivyoonekana mwaka 1936.

Enzi hizo locals wa anga hizo walikuwa na kitu kinachotwa "Sunday Beer Party" kama wanavyoonekana kwenye picha.

Sijui kama bado huu utamaduni upo. cc. Arushaone, PakaJimmy

Picha kwa hisani ya Maktaba ya Congress.


00409r.jpg
 
Msichana wa Longido akiwa amejipamba masikioni, shingoni, na mikononi mwaka 1936.


00419r.jpg
 
Mount Meru mwaka 1936. Umebadilika au bado upo vile vile?

00408r.jpg
 
Kuelekea Ngorongoro Crater mwaka 1936

17743r.jpg


Ngorongoro crater
17747r.jpg
 
Back
Top Bottom