Naaam naam, na mimi nachelea kusema mtaji wa msukule wa kisiasa ni watu wa aina yako.
Tuanzie hapa umeona wapi wewe umetoka kuzaliwa ukajikongoja hadi miaka 10, halafu unataka upate balekhe hapo hapo, unataka upate mke hapo hapo, unataka na uitwe baba hapo hapo, haiwezekani la hasha haiwezekani.
Jambo usilolijua litakusumbua, nasema hivi kwa maana hii, ni ukweli usiopingika Tanzania tuna rasilimali nyingi sana ambazo kwa namna moja ama nyingine zingaliweza kutusaidiea kupiga hatua moja kwenda nyingine. Lakini huwezi ukakurupuka kutamani kutumia rasilimali hizo kama hujaimarika kifikra na kiteknolojia, hapo unapopatolea mfano Kenya angalia leo hii wamewahi kufanikisha kujenga SGR, je wanafaidika nayo? Ndio maana nikasema huwezi ukalazimisha kuitwa baba, wakati hata bado hujabalekhe.
Tanzania ni nchi yenye upekee wake, tulianza kujiimarisha kwanza kutokea kwenye msingi wenye tija ili tutakapoanza kuchanja mbuga basi watu wetu na mifumo yetu iwe na uwezo thabiti wa kuhimili kasi ya maendeleo, ndio maana tumekuwa na mfumo wetu wa kimapinduzi ya uchumi na kiuongozi tofautisha na nchi nyingine hapa barani Afrika na dunia kwa ujumla.
Nadiriki kusema Tanzania ndio nchi pekee duniani iliyoweza kubeba taswira halisi ya maana ya maendeleo, ya kuwa maendeleo ni mchakato.
Mimi nitaichagua CCM, na Nitamchagua Magufuli.