Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

mbona hawa "hawakuanza" wakati wa Magufuli; na sidhani kama kuna serikali duniani imefanikiwa kuwaondoa hawa... wengine imechukua miongo kadhaa kuwafikia (rejea mfano wa Cambodia na Chile)...

..Tatizo ktk Tanzania ya Magufuli " wasiojulikana " walikuwa wanaenenda utadhani wametumwa na kupewa upako toka magogoni au lumumba.
 
Watashangaa sana Mwana mama atakapoanza kusimama mwenyewe bila kujiegemeza kwa yeyote.

Kwanza tayari ni kama amekwishaanza njia yake, kwa maamuzi machache anayofanya sasa hivi.

Hebu fikiria lugha yetu adhimu ya Kiswahili, yeye tayari kasema tofauti na yule aliyekuwa hataki kabisa kusikiliza kitu juu ya lugha nyingine mbali ya Kiswahili, kwa sababu zake mwenyewe.

Mwalimu Nyerere hakukataa lugha nyingine, pamoja na kwamba alikijenga sana Kiswahili.
 
Na pia tupo wengine tunaoamini kuwa JPM rip alimweka Kakoko bandarini ili kudhibiti uingizaji wa makontena ya magendo na utoroshaji wa makontena yenye rasilimali.

Pia ATCL kupata hasara ya bilioni 60 sasa hivi kutoka shilingi bilioni hadi 200 miaka ya nyuma inaonyesha kuwa kulianza kuwa na dalili za mabadiliko kimapato.

Usisahau tangu miaka ya nyuma ATCL ina madeni ya landing fee kutoka viwanja vya ndege vingi tu duniani kiasi cha kutishiwa kuzuiwa ndege hizo pale zitapotua kwenye viwanja hivyo, vile vya London vikiwa ni mojawapo.

Tatizo hapa ni mkakati uleule wa kutaka kuionyesha mabaya pekee upande wa JPM bila kuonyesha mazuri pia na kwa wapinzani kushindwa kuwaelimisha baadhi ya wananchi wa kawaida ambao siku zote ni wajinga.

Ujinga wao ni kwa maana kwamba wao hufuata tu upepo na kusahahu kujiongeza kifikra.

Sasa, ikiwa Kakoko ataondolewa bandarini mimi nimependekeza mheshimiwa raisi amteue mwanajeshi aongoze TPA ili kuleta nidhamu mahali hapo na mapato yaendelee kuingia na kuziingizwe makontena ya magendo wala kutoroshwa makontena yenye rasilimali.

Pili, ili serikali isiendelee kupata hasara ni bora kuziuza ndege zote na kurudisha fedha ambazo zitaelekezwa kwenye maeneo mengine kama Afya na Elimu.

Maana akili za mtanzania na mwafrika twazifahamu wenyewe.
 
Ndio angalizo langu; yaani watamgeuka huyu hadi wataanza kukumbushia zama za Jiwe; kama walivyokuja kumkumbuka JK...
Mzee Mwanakijiji, kwa kumbukumbu tu April 17, 2018, niliandika hivi, nanukuu..,

Mimi sikumpigia kura Rais Magufuli katika uchaguzi wa 2015 kwa sababu ambazo nilizieleza wazi wazi toka hata kabla ya kampeni za Urais kuanza rasmi mwaka huo. Kwa kifupi, kwa historia yake kiuongozi na kiutendaji katika nafasi mbali mbali serikalini kwa muda wa miaka karibia 20, sikuweza kushawishika kwamba anazo sifa mbili, hekima na busara, zinazohitajika kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Alipokuja kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka 2015 sikufarijika, niliona kama vile Watanzania wenzangu wamenisaliti. Lakini, tofauti na wengi, nilifanya uamuzi wa kumpa nafasi na kwa muda wa siku 100 (miezi mitatu) nilikaa pembeni nikifuatilia kwa makini sana utendaji wake kwa tumaini kwamba labda msimamo wangu wa awali juu yake haukuwa sahihi.

Katika hiyo miezi mitatu ambayo nilijiepusha hata kuchangia ndani ya hili jamvi letu la JF, nilijaribu na kujitahidi sana nikubaliane na sifa alizokuwa akipewa na watu waliomuona kama mwokozi wa wanyonge. Nasikitika sana kusema kuwa jitihada zangu zote katika kumkubali hazikuweza kuzaa matunda na
imani yangu kwake ilipungua kadiri siku zilivyosogea na hivi sasa imetoweka kabisa.

Mwisho wa kunukuu... Mzee Mwanakijiji, nimetoa huo ufafanuzi kwa lengo moja tu la kukutoa hofu kwamba kwa namna ile ile nilivyompa Magufuli siku 100, hivyo hivyo nitafanya kwa Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan na hivyo hivyo nilifanya kwa Jakaya Mrisho Kiwete. Naamini muda huo unatosha kabisa kumpima kiongozi yeyote na kujua mwelekeo wake kiuongozi kama anafaa au hafai...akifaa nitamuunga mkono na asipofaa mawe ni yale yale.

Binafsi sina imani na CCM kwa sababu naamini adui wa taifa hili ni CCM...CCM imezeeka, imechoka na inaongoza kwa mazoea, ujanja ujanja na hila hivyo mabadiliko ni muhimu na lazima. Bahati mbaya kwa upinzani wangu huo dhidi ya CCM, wengi wanautafsiri kwamba mimi ni Chadema, hapana wanakosea, mimi ni mpinzani wa uongozi mbovu usio na busara wala hekima kama nilivyoshuhudia kwa marehemu John Pombe Magufuli.

Magufuli hata Katiba aliyoapa kuiheshimu, kuitetea na kuilinda hakuona umuhimu wake na CCM ikafumba macho na ikakubaliana naye hadi kufikia kukiri kwamba nia ya maendeleo inazidi umuhimu wa kufuata sheria. Kama Mh. Rais Samia Suluhu Hassan naye atafuata nyayo za mtangulizi wake ajue amefeli, kapimwa na kakutwa hatoshi na hivyo tutamwandama kama tulivyomwandama John Pombe Magufuli na tulivyomwandama Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Mkulu, wewe unaijua sana nchi yako Tanzania. Huwa kinachobadilika ni Rais, sio chama wala sio mfumo. Kila Rais ana utashi wake na haiba yake. Haitokei wakafanana. Mara nyingi wanakinzana sana. Pima mwenyewe ulivyokuwa ukimchukulia Kikwete na baadaye Magufuli - chma kilekile. Halafu ingawa ni mara ya kwanza mabadiliko ya aina hii kutokea, namini unafahamu kuwa hakuna Rais wa Tanzania anayelazimika kufuata ajenda ya aliyemtangulia.

Hebu ona hizi move tu: Majaliwa alihangaika na wakurugenzi wa Idara huko TPA huku pembeni yake akiwepo DG na Katibu Mkuu wa Wizara wanakodoa macho tu. Mama. Mh. Samia kasema mantiki inataka DG naye awekwe pembeni kupisha uchunguzi. Audit ya ATCL imesomwa bila kurembwa, Mrundikano wa kesi feki mahakamani umehojiwa, ubabaishaji wa majukumu ya TAKUKURU umekosolewa, nk. Na hapa ni mwanzo tu wa mabadiliko ya msingi. Bado tu unaishi kwa matumaini kuwa Mama Samia anaendeleza awamu ya Magufuli?

Usipoteze muda kujibu wapinzani. Hao ndio kazi yao. Watamchochea Mama afanye wanayoyatarajia. Akianza kui-consolidate CCM kujiandaa na 2025 watarejea kumshambulia kwa kukandamiza upinzani n.k. It's all part of the usual merry-go-around. Sijui kama wewe bado utakuwa mnazi wa CCM wakati huo.
 
Ni kweli Samia ni ccm lakini katu hawezi kuchukua Tabia na mwenendo wa Magufuli , Samia hatoivunja Ilani ya ccm wala hataiweka ccm mfukoni
 
Chama kilekile.

Ilani ileile.

Katiba ileile.

Watu ni walewale kasoro mmoja tu.

I am sober. I am managing my expectations.

Sitegemei tofauti kubwa.

At least, no significant and immediate changes are likely!
 
Mzee Mwanakijiji,
Kwa maoni yangu nadhani kuwa kama waAfrika wa nchi zingine walivyodhani Magufuli ni "mtakatifu, Mzalendo, Mpigania Haki za Kiuchumi za waAfrika, Asiyependa Ufujaji wa Pesa za Umma, kinara wa Maendeleo ya Vitu badala ya Maendeleo ya Watu" ukweli ni kwamba si hivyo walivyokuwa wanamfikiria.

Na waTanzania baada ya Magufuli kuwa mwendazake RIP, sasa wanapata nafasi ya kuona mapungufu yake makubwa yaliyokuwa yanasemwa ambayo kwa miaka mitano yalibatizwa kuwa ni uvumi wa mawakala wa mabeberu waliopo Tanzania wasio wazalendo.

Maendeleo ya Vitu ilikuwa ni mwamvuli na chombo cha kipropaganda wa kuficha ubadhilifu mkubwa, kukandamiza demokrasia, ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu na kukandamiza uhuru wa kupata na kupashana habari.

Kufungwa kwa mwamvuli wa huu wa kuficha mapungufu wa Magufuli RIP ndiyo mwisho wa agenda zake zote na mpaka kufika 2025 kila kilichokuwa 'cha Magufuli' kama ambavyo hatua na agenda zilizokuwa zimebinafsishwa kwamba si CCM wala Serikali kinafanya bali ni mtu mmoja ndiyo alibebaba kila kitu , basi hivyo vyote vitakuwa vimezikwa pamoja na Magufuli.

Maono ya Mzee B.W Mkapa (RIP) yanatimia, Sasa serikali mpya itaachana na agenda ambazo chama na serikali haikuziamini ni zake na wakamwachia Magufuli (RIP) azibebe mwenyewe. Kazi ya Mola haina makosa, sasa ni nafasi kwa kile wanachama halisi wa CCM, mawaziri na wataalamu serikalini kutekeleza wanachoamini kupitia maridhiano yenye hoja-shawishi shirikishi na kwa pamoja kukitekeleza kile walichokubaliana kwa umoja wao. Na hii ndiyo maana halisi ya uwepo wa chama cha siasa, na chama hujijenga kwa hoja, agenda na ilani za ushawishi mpana ulio shirikishi kutimiza malengo, mfano ya muda mrefu 2025 - 2030 na zaidi.

5 Jul 2018
MKAPA AMKOSOA VIKALI MAWAZIRI WA JPM ''Apinga utumiaji wa neno MIMI MIMI badaa ya Serikali ya CCM"
 

Fanya utafiti kidogo juu ya hali ya aviation industry duniani kabla hujaihukumu ATCL. Airlines zote zinapumulia machine!
 
Sema nyinyi mafisadi na wauza madawa ndiyo mlikuwa mnaishi na wasiwasi kwa matendo yenu. Lakini kumbuka bado serikali ileile inaendelea ukirudia makosa yako unaenda na maji. Angali video clip hapa chini uone watz walivyomuaga Jemedari wetu kama wangekuwa hawana amani wangemuaga hivi??

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…