Charles Mandela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 2,752
- 2,282
SIMBA ni wenyeji wa asilia wanaopatikana mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA. Hawa wenyeji wa hii mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA huwa wanaitwa SIMBA au MWASHITA kwa jina lingine.simba na chui kivip, fafanua
Wakazi wa hii mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA ndio waliosalia bila ya kuguswa kwenye lile sakata la ubinafsishaji kwa waliojilimbikizia mali na ukwasi uliotokana na vyama vya ushirika.
Vyama vya ushirika vilivyokuwa vinapatikana kwenye hii mikoa husika vilikuwa ni - chama cha ushirika cha MWANZA kilichokuwa kinaitwa NCU, chama cha ushirika cha SHINYANGA kilichokuwa kinaitwa SHIRECU na chama cha ushirika cha TABORA kilichokuwa kinaitwa WETCU.
Kama unavyofahamu, waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika ndio waliokuwa na ukwasi kipindi hicho na wengine bado wana ukwasi mpaka leo hii kutokana na sababu niliyoitaja hapo juu ya HAYATI MWALIMU kuwaacha bila ya kuwagusa wale waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA.
Huu ulikuwa ni mkakati wa kisiasa wa HAYATI MWALIMU kuandaa ngome yake ya kisiasa kwa kuandaa upinzani wake mwenyewe.
Na CHUI ni wenyeji wa mkoa wa MARA au kwa jina lingine wanaitwa SERENGETI au kwa jina lingine wanaitwa RAMA [ Hii RAMA imetokana na neno MARA baada ya kuligeuza kinyume ] au kwa jina lingine wanaitwa RAMADHANI.
Mara nyingi hili jina la CHUI huwa hawalitumii sana ili kuficha uhalisia wake. Mara nyingi huwa wanatumia majina ya SERENGETI au RAMADHANI yaani RAMA.
Na kitu kingine ambacho jamii huwa inafichwa ni kuwa - hawa MWASHITA yaani SIMBA ndio huwa wanaongoza kwa idadi kubwa ya watu wakifuatiwa na CHUI yaani SERENGETI au kwa jina lingine wanaitwa RAMADHANI au RAMA yaani MARA na huwa sio WACHAGA wala WANYAKYUSA.
Narudia tena - kitu kingine ambacho jamii huwa inafichwa ni kuwa, hawa MWASHITA yaani SIMBA ndio huwa wanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wakifuatiwa na CHUI yaani SERENGETI au kwa jina lingine wanaitwa RAMADHANI au RAMA yaani MARA na sio WACHAGA wala WANYAKYUSA.
Sasa hii inatokana na nini? Mkoa wa MARA una makabila zaidi ya kumi [ 10 ] na HAYATI MWALIMU alifanikiwa kuyaunganisha makabila yote na kuwa na dhana ya kisiasa iliyo moja. Na kilichofuatia baada ya hapo ni kujenga ngome ya kisiasa kwa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA.
Sasa kwanini hawa wenyeji wa mkoa wa MARA waitwe CHUI na hawa wenyeji wa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA yaani MWASHITA waitwe SIMBA?
Je, wenyeji wa mikoa mingine wanaitwa majina gani?
Na ni nani aliyehusika kuipa majina ya wanyama mikoa pamoja na kanda za TANZANIA?
Majibu yake ni haya - kwa swali la kwanza. Wenyeji wa mkoa wa MARA wanaitwa CHUI ni kwa sababu sifa za mnyama CHUI ndio walizonazo wenyeji wa mkoa wa MARA, hali kadhalika wenyeji wa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA wanaitwa SIMBA ni kwa sababu sifa za mnyama SIMBA ndio walizonazo wenyeji wa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA.
Majibu kwa swali la pili kuhusu wenyeji wa mikoa mingine wanaitwa majina gani? Kwa kutumia RAMANI hapo juu, wenyeji wa mikoa ya KAGERA, KIGOMA na RUKWA huwa wanaitwa KIBOKO na wenyeji wa mikoa ya MBEYA, IRINGA na MOROGORO huwa wanaitwa KIFARU na wenyeji wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO huwa wanaitwa NYATI na wenyeji wa mikoa ya RUVUMA, MTWARA na LINDI huwa wanaitwa TEMBO. Mengine sio vizuri kumalizia mikoa iliyobaki kwa sababu ya unyeti wake.
Majibu kwa swali la tatu - kuhusu ni nani aliyehusika kuipa majina ya wanyama mikoa pamoja na kanda za TANZANIA? Jibu, ni kuwa tangu utawala wa WAJERUMANI walipofika na kuitawala TANGANYIKA waligawanya makabila kwa kutumia SIFA za wanyama wa porini walioakisi tabia za watu wa kabila fulani.
Nadhani hapa umeelewa! Turudi kwenye maada husika sasa - kwanini HAYATI MWALIMU aliigeuza hii mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO kuwa ni "BATTLE GROUND" yaani "UWANJA WA VITA" kati ya SIMBA na CHUI.
Hawa wenyeji wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO yaani NYATI walikuwa na vuguvugu la kudai UHURU wao tangu kipindi cha ukoloni. Hali ambayo ilikuja kuchanganya na joto la mabadiliko ya kisiasa kupanda zaidi baada ya kifo cha utata cha aliyekuwa WAZIRI MKUU wa kipindi hicho, EDWARD MORINGE SOKOINE mwaka 1984.
Ifahamike kuwa siasa za TANU na ASP zilifanyika mikoa ya PWANI pamoja na ZANZIBAR. Lakini baada muungano wa vyama vya siasa vya TANU na ASP na kuunda chama cha CHAMA CHA MAPINDUZI, yaani CCM. Siasa zote za CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM zilifanyika TABORA na sio DODOMA kama watanzania wengi wanavyofikiria.
Baada ya mwaka 1977, siasa zote na maamuzi yote ya CHAMA CHA MAPINDUZI, yaani CCM yalifanyika TABORA, pale DODOMA yaani CHIMWAGA ilikuwa ni kupitisha maamuzi yaliyokwishafanyika na kuamuliwa TABORA.
Nadhani mpaka leo ndivyo inavyofanyika hivyo, pale WHITE HOUSE [ DODOMA ] ni makao makuu ya CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM na TABORA ndio makao makuu ya intelijensia ya CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM.
Kwahiyo, kupitia intelijensia ya CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM [ sio TISS wala sio NSA ] waliwawezesha kiuchumi hawa wenyeji wa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA kupitia mazao ya kibiashara yaliyokuwa yanapatikana kwa wingi kipindi hicho. Mazao hayo ya biashara ni PAMBA pamoja na TUMBAKU.
Kilichofanyika ni SIASA ya kuua hivi vyama vya ushirika kwa kufilisi na kufunga wahujumu uchumi waliokuwa wakifanya kazi kwenye hivi vyama vya ushirika na kuwaacha wale waliokuwa watumishi wote wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU. Hii yote ilifanyika kwa baraka zote za HAYATI MWALIMU.
Sasa kipindi cha vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa kupanda, HAYATI MWALIMU aling'atuka kwenye nafasi ya urais na kumuachia nafasi ya urais ALLY HASSAN MWINYI. Lakini HAYATI MWALIMU aliendelea kuwa mwenyekiti wa CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM mpaka pale hali ya kisiasa ilipotulia na kumuachia hiyo nafasi ya uenyekiti wa chama, ndugu ALLY HASSAN MWINYI. Hii yote ilifanyika mwaka 1990.
Lakini mbinu iliyotumika kuzima vuguvugu la kisiasa kwa kipindi hicho ilikuwa ni "HARSH" kidogo. Kuna watu wengine waliuawa! Kuna watu wengine walifungwa kifungo cha maisha! Kuna watu wengine walifilisiwa! Kuna watu wengine walilawitiwa, kubakwa, kubanwa makorodani na kuharibiwa maumbile ya uzazi kwa jinsia zote za kike na kiume!
Mbinu nyingine iliyotumika kuzima vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa ni KUHAMIA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO kwa wakati huo. Sasa hivi hii mikoa inajumuisha MANYARA, ARUSHA na KILIMANJARO. Hii mbinu ndio inayoitwa "BATTLE GROUND" au "UWANJA WA VITA".
Watu wengi kutoka mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA yaani SIMBA walihamia mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO na kushika sekta zote za kiuchumi. Na waliofanikisha hili kwa upande wa SIMBA ni waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU.
Kwa upande wa MARA yaani CHUI au kwa jina lingine SERENGETI au RAMADHANI yaani RAMA walihamia mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO na kushika sekta zote za kiuchumi. Na aliyefanikisha hili kwa upande wa CHUI alikuwa ni HAYATI MWALIMU mwenyewe. HAYATI MWALIMU alikuwa akiwapa mitaji ya kibiashara kwa wale waliokuwa wafanyabiashara na kuwapa nafasi za kuhamia kwa wale waliokuwa watumishi wa SERIKALI ikijumuisha sekta za JESHI LA WANANCHI, POLISI, MAGEREZA, UHAMIAJI na IDARA YA MAHAKAMA.
Sasa kwa upande wa SIMBA waliokuwa wakihamia mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO na kubadilisha majina yao ya asili na kuakisi majina ya asili ya ARUSHA na KILIMANJARO walikuwa wakipata msaada wa FEDHA kutoka kwa hawa waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU.
Hawa SIMBA ndio walioanzisha baadhi ya vijiji kule KILIMANJARO na kuakisi majina ya asili ya huko. Moja ya vijiji hivyo maarufu ni BOMANG'OMBE. Hawa wenyeji wote wa BOMANG'OMBE ni SIMBA kutoka SHINYANGA waliokuwa wakipata msaada wote kutoka kwa waliokuwa wafanyakazi wa SHIRECU. Vijiji vingine ni SIRI, sio vyema kusema yote hadharani.
Na kwa upande wa CHUI ni vivyo hivyo, hawa RAMADHANI yaani RAMA au kwa jina lingine SERENGETI ndio wanavyofanya kwa CHUI waliohamia mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO. Kuna vijiji vipo ambavyo hawa CHUI walihamia na kuakisi majina ya asili ya huko.
Kwa upande wa SIMBA yaani MWASHITA [ MWANZA, SHINYANGA na TABORA ] wameenda mbali zaidi hadi kuwapatia ajira kwenye makumpuni ya kibiashara yanayomilikiwa na SIMBA. Ilifanyika hivyo ili kushikilia sekta zote za kiuchumi zilizopo mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
Ndio maana watu wengi wanashangaa TIGO kuwa na wafanyakazi wengi kutoka mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO. Hao ni SIMBA yaani WASUKUMA walioakisi majina yenye asili ya mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO ambao wazazi wao walihamia huko kipindi cha vuguvugu la kisiasa.
Na ndio hao wafanyakazi wa makampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo ya KILIMANJARO EXPRESS, ARUSHA EXPRESS, DAR EXPRESS, MGHAMBA INTERTRADE LTD, NBS Co. LTD, HAPPY NATION, ISAMILO, NYEHUNGE, ZUBERI, KISESA, TANZANITE, BEST LINE, CHAMPION, AL SAEDY, ABC, SAULI, BUTI LA ZUNGU, SPIDER, SIMBA MTOTO, TASHRIFF, TAQWA, FALCON, ADVENTURE, SARATOGA, ALLY'S, SHERATON, RED BELT, AHMEED, NAAMAN'S, KIAZI KITAMU, MACHAME INVESTMENT, KISBO, KIBO SAFARI, ASANTE RABI, NGASERE, HAI EXPRESS, ROMBO EXPRESS, RAHA LEO na TAHMEED.
Na ndio hao wamiliki na wafanyakazi wa hoteli nyingi za kitalii zinazopatikana mikoa ya MANYARA, ARUSHA na KILIMANJARO.
Na kuna timu ya mpira wa miguu inayoshiriki ligi kuu, MTIBWA SUGAR FC inaweza kuhamia mkoa wa ARUSHA au KILIMANJARO. Hii ikiwa ni muendelezo wa kushika sekta zote za kiuchumi zinazopatikana mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
Hii yote ilifanyika kwa baraka za HAYATI MWALIMU baada ya kuwawezesha kiuchumi hawa wenyeji wa mikoa ya MWANZA, SHINYANGA na TABORA.
Hiyo ndio "BATTLE GROUND" yaani "UWANJA WA VITA" iliyoasisiwa na HAYATI MWALIMU mwenyewe. Kwahiyo kuanzia leo inabidi ufahamu kuwa sio kila mtu anayeitwa MANKA ni MCHAGA au sio kila mtu anayeitwa SUMARI ni MMERU au sio kila mtu anayeitwa TLUWAY ni MUIRAK [ 😂😂😂 ].
Raia mmoja kati ya raia wanne waopatikana mkoa wa KILIMANJARO ni SIMBA yaani MWASHITA. Iko vivyo hivyo hata kwa mkoa wa ARUSHA, raia mmoja kati ya raia wanne waopatikana mkoa wa ARUSHA ni SIMBA yaani MWASHITA.
Ndio hao unawaona WASAFI FM na WASAFI TV wakina TILLYA [ 😁😁😁 ] pamoja KISS FM zote za KENYA, TANZANIA na RWANDA. Ndio hao wote unaowaona kwenye makumpuni ya SIMBA ilhali wao wana majina ya asili ya mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
Nadhani pia kuna mradi ambao utakuja kufanyika kwa hawa NAKO2NAKO SOLDIERS kama ilivyo kwa WASAFI. Huo mradi utafanyika hapo hapo ARUSHA.
Na ndio maana hauwezi kukuta SIMBA yaani MWASHITA aliyehamia mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO akakosa kazi, labda iwe kama hataki kufanya kazi, na awe anatamani kujiajiri.
Na hivi ndivyo ilivyo kwa upande wa CHUI yaani SERENGETI au kwa jina lingine wanaitwa RAMADHANI au RAMA yaani MARA inavyofanyika kwa TANZANIA nzima. Hawa CHUI waliohama kutoka MARA kwenda mikoa mingine ndio wanaopata nafasi nyeti SERIKALINI na kwenye CHAMA TAWALA.
Sema HAYATI MWALIMU aliwapa SIMBA yaani MWASHITA mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO kama kuwapima tu kipindi hicho, maana walikuwa hawawezi kufanya hivyo kwa TANZANIA nzima kwa sababu ya kuwa na uchumi mdogo ukilinganisha na uchumi wa CHUI.
Lakini hawa SIMBA wameenda mbali zaidi hadi kuenea TANZANIA nzima, yaani wamevuka malengo waliyowekewa na HAYATI MWALIMU.
Hawa SIMBA wameshika pia uchumi wa AFRIKA YA MASHARIKI kwa kumiliki makampuni ya utalii, makampuni ya simu, usafirishaji wa abiria na mizigo, vituo vya televisheni pamoja na redio.
Hiki ni kituo cha televisheni kinachoitwa KTN, hii ni kampuni kubwa sana inayopatikana KENYA na inayomilikiwa na SIMBA. Na wafanyakazi wake wengi ni SIMBA vile vile, yaani MWASHITA.
Kwa upande wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO kwa sasa iko chini ya SIMBA yaani MWASHITA. Kama unavyoona hapo juu.
Hao SIMBA ndio wanaonunua hoteli nyingi sana kwa sasa pale ARUSHA na KILIMANJARO. Na ndio wameshika uchumi wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO kwa pamoja.
Vile vile hii mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO inatumika kama EDUCATIONAL PATHWAY kwa wanafunzi kutoka MWASHITA [ MWANZA, SHINYANGA na TABORA ]. Kwa wale wanafunzi waliosoma mikoa hii watakubaliana na mimi, kuwa shule nyingi za bweni kwa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO zinachukua wanafunzi wengi kutoka MWASHITA [ MWANZA, SHINYANGA na TABORA ] yaani SIMBA.
Hiyo ndio "BATTLE GROUND" yaani "UWANJA WA VITA" kati ya SIMBA na CHUI iliyoasisiwa na HAYATI MWALIMU mwenyewe, ikiwa na lengo la kuzima vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa yaliyokuwa yakianza kufanyika kwa upande wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
Hiyo "BATTLE GROUND" yaani "UWANJA WA VITA" iliambatana na kumiliki sekta zote za kiuchumi zinazopatikana kwa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO.
Kwa wale wenyeji wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO watakubaliana na mimi, kuwa ni vigumu kwa NYATI [ mwenyeji asilia wa MANYARA, ARUSHA na KILIMANJARO ] kuweza kufanya BIASHARA kwa mikoa ya ARUSHA KILIMANJARO na MANYARA na akafanikiwa, wengi wao wanafilisiwa, wanabambikiwa kesi na hata kupunguzwa [ ⚰️ ]. Na wale wafanyabiashara waliolifahamu haya mapema walihamia nchi jirani ya KENYA kwa usalama wao.
Kwa miaka ya hivi karibuni wafanyabiashara wengi sana wa mikoa ya ARUSHA na KILIMANJARO walipunguzwa [ ⚰️ ] kwa namna tofauti tofauti. Na hiyo ndio "BATTLE GROUND" yaani "UWANJA WA VITA" na huo ndio mkakati wa SERIKALI inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI yaani CCM.