HAYATI MWALIMU na aliyekuwa Rais wa serikali ya wanafunzi ya CoHSS, mwaka 2012/13 ni Pete na Kidole - hauwezi kuwatofautisha wala kuwatenganisha. Sema HAYATI MWALIMU ni CHUI na yule mwingine ni SIMBA.
Tuachane na hayo! Kila awamu ya kipindi cha Urais kwa nchi ya Tanzania, kiongozi wa nchi - yaani Rais analazimika kuandaa upinzani wake na hii imekuwa ni kama desturi tangu kipindi cha HAYATI MWALIMU.
Sasa kipindi cha HAYATI MWALIMU kulikuwa hakuna mfumo wa vyama vingi, kulikuwa na mfumo wa chama kimoja tu.
Na kipindi ambapo HAYATI MWALIMU anakabidhiwa uhuru kutoka kwa Mwingereza kulikuwa na mshindani wake wa kipindi hicho, alikuwa anajulikana kwa jina la MAKWAIA. Huyu MAKWAIA alikuwa ni CHIFU anayetoka maeneo ya KISHAPU, mkoa wa SHINYANGA.
Huyu CHIFU alikuwa na elimu nzuri sana [ MASTERS ], alipata elimu yake kutoka Uingereza. Familia ya huyu CHIFU ilikuwa na ukwasi wa kutisha na ilikuwa ikiongoza kwa upande wa Afrika ya Mashariki kutokana na biashara ya almasi na biashara ya zao la pamba.
Baada ya HAYATI MWALIMU kupewa nafasi ya kufuatilia uhuru na kufanikisha kupewa uhuru kutoka kwa Mwingereza, wale waliokuwa washindani wake aliwafanya kuwa marafiki na kuwapa nyadhifa mbalimbali serikalini.
Vile vile HAYATI MWALIMU alifanikiwa kuua hizi tawala za kichifu kwa upande wa Tanzania bara kwa kuwapa nafasi serikalini wale waliokuwa na elimu kutoka familia za kichifu.
Lakini ushindani hafifu uliendelea kuwepo na ushindani ulikuja kushika kasi hasa baada ya kuanzishwa kwa vyama vya ushirika.
Kulikuwa na vyama vya ushirika kwa upande wa Tanzania Bara vilivyokuwa vikisimamia mazao ya biashara kwa kila mkoa husika.
Na vyama vya ushirika vilivyokuwa na nguvu ya kiuchumi kwa kipindi hicho, vilikuwa ni vyama vya ushirika kutoka mkoa wa Mwanza [ NCU ] waliokuwa wakisimamia biashara ya zao la pamba, mkoa wa Shinyanga [ SHIRECU ] waliokuwa wakisimamia biashara ya zao la pamba na mkoa wa Tabora [ WETCU ] waliokuwa wakisimamia biashara ya zao la tumbaku.
Lakini baadae kulikuja kutokea anguko kubwa sana la hivi vyama vya ushirika kushindwa kujiendesha kutokana na kuwa na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu - wizi na ubadhirifu wa mali ya umma ulikithiri, hivyo kupelekea vyama vya ushirika kushindwa kujiendesha.
Lakini hii yote, kulikuwa na baraka kutoka kwa HAYATI MWALIMU, kwa sababu hivi vyama vya ushirika vilikuwa vinatishia uhai wa CHAMA CHA MAPINDUZI. Kungelitokea vyama vya ushirika vimejiunga na kuunda chama kimoja cha siasa, vingeliweza kukitoa CHAMA CHA MAPINDUZI madarakani kwa sababu ya kupata uungwaji mkono mkubwa sana kutoka kwa vyama vya wafanyakazi pamoja na vyama vya wakulima.
Hivyo basi, wale watumishi wa vyama vya ushirika kutoka mikoa mingine walifikishwa mahakamani kutokana na wizi wa mali ya umma, wengine walifilisiwa na hata kufungwa lakini hawa wafanyakazi wa Chama Cha Ushirika Cha Mwanza [ NCU ], Chama Cha Ushirika Cha Shinyanga [ SHIRECU ] na Chama Cha Ushirika Cha Tabora [ WETCU ] walikuwa huru, sema kuna baadhi yao walifukuzwa kazi bila hata ya kuchukuliwa hatua yoyote. Na hii ilifanyika chini ya uangalizi wa HAYATI MWALIMU mwenyewe.
Hawa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU walikuja kuwa na ukwasi wa kutisha na wengine walikuwa na uchumi mkubwa kuliko hata aliyekuwa kiongozi wao wa kimila, yaani CHIFU MAKWAIA.
Na hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio watanzania weusi wenye uchumi mkubwa mpaka leo hii, ukiondoa wanasiasa wa CHAMA CHA MAPINDUZI.
Hawa wafanyakazi waliofanya ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU ndio waliokuja kuwa washindani wakubwa wa HAYATI MWALIMU kwa miaka iliyosalia kabla ya umauti kumkuta HAYATI MWALIMU. Na hawa ndio wapinzani halali wa CHUI yaani SERENGETI iwe ni kielimu, kiuchumi, kisiasa, kimichezo na burudani.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta za usafirishaji wa abiria pamoja na mizigo kwa Tanzania nzima. Narudia tena - "Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta za usafirishaji wa abiria pamoja na mizigo kwa Tanzania nzima".
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta ya kilimo kwa kumiliki viwanda vikubwa vya sukari vya KAGERA SUGAR na MTIBWA SUGAR kwa pamoja. Vile vile hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wameshikilia mazao ya biashara kama pamba, tumbaku na alizeti kwa kumiliki viwanda vya kuchambua na kukamua mafuta ya pamba pamoja na alizeti. Kwa lugha ya Kiingereza wanaita - Ginneries.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta ya kilimo cha ngano kwa kumiliki viwanda vya AZANIA WHEAT FLOUR, MeTL, CAMEL WHEAT FLOUR na PEMBE WHEAT FLOUR.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa viwanda vya SAYONA INDUSTRIES.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha TANGA PHARMACEUTICAL & PLASTICS LTD kinachotengeneza HERBAL PETROLEUM JELLY na mafuta ya kutumia mwilini yanayoitwa VESTLINE.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha kutengeneza maziwa freshi kinachoitwa TANGA FRESH kinachopatikana mkoani Tanga.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta ya mafuta ya kupikia, sabuni za kuogea na kufulia kwa kumiliki viwanda vya G&B industries, MeTL pamoja na AZANIA.
Tofauti na viwanda vya G&B industries, MeTL pamoja na AZANIA. Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kampuni ya MURZAH WILMAR EAST AFRICA LIMITED inayotengeneza mafuta ya kupikia ya KORIE.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta ya uagizaji wa mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa kwa kumiliki makampuni ya LAKE OIL, MOIL, PETRO AFRICA, MSN, SIMBA OIL, KILIMANJARO OIL, BIG BON, AFROIL, OILCOM, KOIL, MERU OIL, PRIME FUELS, UKOO PETROLEUM LTD na DALBIT PETROLEUM LTD [ Hizi ni kampuni za usafirishaji wa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa ], OLYMPIC OIL pamoja na CAMEL OIL.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha SIMBA CEMENT na CAMEL CEMENT kwa pamoja.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha MMM STEEL na KIOO INDUSTRY kwa pamoja.
Tofauti na viwanda vya MMM STEEL na KIOO INDUSTRY, hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha kutengeneza rangi kinachoitwa GOLDSTAR PAINTS TANZANIA LIMITED.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kampuni ya ukandarasi ya NYANZA ROAD pamoja na makampuni mengine yanayoshughulika na madini kama KILIMANJARO MINING na KASCO MINING.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kampuni ya SIMBA GROUP na SIMBA TRAILERS.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa makampuni yanayotengeneza na kuunganisha mabodi ya mabasi pamoja na malori. Makampuni hayo ni DAR COACH kwa upande wa TANZANIA🇹🇿, BANBROS LTD na MASTER FABRICATORS LTD kwa upande wa KENYA🇰🇪. Hii ndio sababu inayopelekea kushika sekta ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kipindi kirefu sana.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa benki za DIAMOND TRUST BANK [ DTB ], AKIBA COMMERCIAL BANK [ ACB ] na AZANIA BANK [ AB ] kwa pamoja.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kampuni ya mawasiliano ya TIGO [ Tanzania ].
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kampuni ya uchapishaji ya magazeti inayoitwa Mwananchi Communications Limited [ MCL ].
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kiwanda cha kutengeneza pipi za IVORI kinachopatikana Iringa.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wanaomiliki shule nyingi binafsi hapa nchini. Yaani wanamiliki shule nyingi sana kwa upande wa Tanzania bara kuliko hata taasisi za kidini yaani KANISA KATOLIKI, KKKT na ANGLIKANI.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa Hoteli ya KEMPINSKI na wana hoteli nyingi sana za kitalii kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Iringa, Morogoro, Kigoma na Zanzibar.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, yaani FGBF. Pale FGBF, Askofu Zakaria Kakobe ni mfanyakazi tu kama ilivyo kwa Profesa Ibrahim Lipumba, upande wa CUF.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio walioshika sekta ya michezo hususani mpira wa miguu kwa kumiliki timu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu. Timu hizo ni SIMBA SC ya mkoa wa Dar Es Salaam, BIASHARA MARA UNITED ya mkoa wa Mara, COASTAL UNION SC ya mkoa wa Tanga, KAGERA SUGAR FC ya mkoa wa Kagera pamoja na MTIBWA SUGAR FC ya mkoa wa Morogoro. Kuna timu nyingine za daraja la kwanza, daraja la pili na timu zinazoshiriki ligi ya mikoa.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa kundi la wasanii la Wasafi Classic yaani WCB, kituo cha televisheni pamoja na kituo cha redio. Na ndio hao hao waliokuwa wamiliki halali wa kundi la HipHop la Nako2Nako Soldiers linalopatikana Arusha. Na kuna wasanii wengine wengi tu, ndani na nje ya nchi ya TANZANIA 🇹🇿 kama vile UGANDA 🇺🇬, KENYA 🇰🇪, KONGO 🇨🇩, ZAMBIA 🇿🇲, KAMERUNI 🇨🇲 na AFRIKA YA KUSINI 🇿🇦.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa vyama vya siasa vya CUF - Chama Cha Wananchi na ACT - Wazalendo.
Hawa waliokuwa wafanyakazi wa vyama vya ushirika vya NCU, SHIRECU na WETCU ndio wamiliki halali wa Chuo Kikuu cha ECKERNFORDE TANGA UNIVERSITY. Kwahiyo, hawa watu sio watu wa mchezo mchezo! Ni watu wanaofahamu nini wanafanya. Hakuna ujanja ujanja wala uhuni uhuni! Elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa MWASHITA yaani SIMBA.
Hao ndio SIMBA! Hao ndio SIMBA waliokuwa na baraka zote kutoka kwa HAYATI MWALIMU tangu miaka ya 1984! Au kwa jina lingine wanaitwa MWASHITA [ Mwanza, Shinyanga na Tabora ]. Wapinzani halisi wa CHUI yaani SERENGETI au kwa jina jingine wanaitwa RAMADHANI au RAMA yaani MARA.
Hawa SIMBA ni tofauti kabisa na hiki kikundi kinachojiita SUKUMA GANG. Hii SUKUMA GANG ni kikundi cha wanasiasa wahuni wahuni tu, tena walionawili kipindi cha Marehemu Rais John Pombe Magufuli. Hii SUKUMA GANG ni kikundi cha wanasiasa ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI wasiokuwa hata na utashi wa kisiasa na wasiokuwa na maono ya kuona mbali. Hii SUKUMA GANG hata uchumi wa kuendesha chama cha kisiasa bado hawana.
Sasa tujiulize maswali mengine, ni kwanini CUF - Chama Cha Wananchi kimepoteza umaarufu ilhali watu walionyuma yake wana uwezo mkubwa kiuchumi? Jibu, ni kuwa hawa SIMBA waliokuwa nyuma ya CUF - Chama Cha Wananchi walipoteza muda mwingi sana kushindana na CHUI kiuchumi, yaani SIMBA na CHUI walikuwa wanashindana sana kuwekeza kiuchumi nje ya nchi.
Lakini sote yatupasa kufahamu kuwa, CHUI ndio mwenye CHAMA CHA MAPINDUZI na ndio mwenye DOLA YA TANZANIA. Kwahiyo kushindana na mwenye dola yataka moyo! Narudia tena - kushindana na mwenye dola yataka moyo! Sio kazi rahisi kama watu wengi wanavyofikiria.
SIMBA kuendelea kushindana na CHUI kuwekeza nje ya nchi kulimfanya kupoteza nafasi ya Chama Kikuu Cha Upinzani bungeni na nafasi yake kuchukuliwa na CHADEMA mwaka 2010 mpaka mwaka 2020. Hawa CHADEMA walipata uungwaji mkono mkubwa sana wa kisiasa kwa mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na baadhi ya sehemu za Tanzania. Vile vile wenyeji wa hii mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro wanajulikana kwa jina la NYATI au kwa jina lingine la utani wanaitwa NYUMBU [ 😁😁😁 ]. Na ndivyo jinsi walivyo!
Katika kuwekeza nje ya nchi, ilifikia hatua CHUI akimiliki Esperance de Tunis ya Tunisia, hawa SIMBA wanamiliki Raja Club de Athletic ya Moroko.
Hawa CHUI wakimiliki AlAhly ya Misri, SIMBA wanamiliki Zamalek ya Misri vile vile.
CHUI akimiliki Asec Mimosas ya Ivory Coast, SIMBA wanamiliki Horoya AC ya Guinea.
CHUI akimiliki Stellenbosch FC ya Afrika ya Kusini, hawa SIMBA wanamiliki Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini vile vile.
SIMBA akimiliki Tout Puissant Englebert Mazembe ya Kongo - Lubumbashi, hawa CHUI wanamiliki Wydad Club de Athletic ya Moroko.
Yaani ni tafrani! Na haya ndio makosa makubwa sana aliyoyafanya HAYATI MWALIMU kipindi yuko hai. Watangulizi wake wakina Ali Hassan Mwinyi, wakina Marehemu Benjamin Mkapa, wakina Mrisho Khalifani, wakina Marehemu John Magufuli na hatimaye Mama Samia Suluhu wote wameshindwa kuidhibiti SIMBA mpaka inakaribia kuchukua DOLA YA ZANZIBAR.
Lakini huo ndio upinzani alioutengenza na kuuacha HAYATI MWALIMU na ndio unaosumbua mamlaka za kiintelijensia mpaka leo hii, kwa sababu hao ndio wameshika uchumi wa Tanzania, mbali na wanasiasa wa CHAMA CHA MAPINDUZI.
Hawa SIMBA wameenda mbali zaidi hadi kutawala SOKA LA AFRIKA KWA UPANDE WA VILABU. Hii yote inatokana na kumiliki uchumi mkubwa mpaka nje ya mipaka ya TANZANIA. Hawa SIMBA ndio wamiliki halali wa timu ya FC PLATINUM ya ZIMBABWE 🇿🇼, KAIZER CHIEFS ya AFRIKA YA KUSINI 🇿🇦, NKANA FC ya ZAMBIA 🇿🇲, BIG BULLETS ya MALAWI 🇲🇼, PRIMEIRO DE AGOSTO ya ANGOLA 🇦🇴, ASANTE KOTOKO ya GHANA 🇬🇭, AKWA UNITED ya NAIJERIA 🇳🇬, TP MAZEMBE ya KONGO 🇨🇩, TOWNSHIP ROLLERS ya BOTSWANA 🇧🇼, KARIOBANGI SHARKS ya KENYA 🇰🇪, EXPRESS FC ya UGANDA 🇺🇬, RAYON SPORTS ya RWANDA 🇷🇼, VITAL'O ya BURUNDI 🇧🇮, AL HILAL OMDURMAN ya SUDANI 🇸🇩, AC HOROYA ya GUINEA 🇬🇳, COTONSPORTS ya KAMERUNI 🇨🇲, RAJA CLUB DE ATHLETIC ya MOROKO 🇲🇦, ETOILE SPORTIVE DU SAHEL ya TUNISIA 🇹🇳, ENTENTE SPORTIVE SETIFIENNE [ ES SETIF ] ya ALGERIA 🇩🇿, ZAMALEK ya MISRI 🇪🇬 pamoja na SIMBA SC ya TANZANIA 🇹🇿.
Hii yote inatokana na kumiliki uchumi mkubwa sana hata kwa upande wa nje ya mipaka ya TANZANIA.
Kama ilivyo kwa CHUI au jina lingine SERENGETI kuwa na uchumi mkubwa kuliko hata TISS na NSA kwa pamoja. Ndivyo ilivyo kwa upande wa SIMBA au jina lingine wanaitwa MWASHITA kuwa na uchumi mkubwa kuliko hata TISS na NSA kwa pamoja.
Na haya ndio makosa makubwa sana aliyoyafanya HAYATI MWALIMU kipindi cha uhai wake, upinzani alioutengenza yeye HAYATI MWALIMU, watangulizi wake wameshindwa kuudhibiti. Na ndio wanaoligharimu taifa mpaka wanakaribia kuchukua DOLA YA ZANZIBAR. Na wakimaliza DOLA YA ZANZIBAR, hawa SIMBA wanageukia TANZANIA BARA.