[
Inaendelea kutoka posti namba 910 ]
Vile vile kwa mwaka 1965, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alipishana kauli na HAYATI MWALIMU kwa mara ya kwanza, ni baada ya TANZANIA 🇹🇿 kuwa NCHI ya CHAMA kimoja.
Japo OSCAR SALATHIEL KAMBONA alipitisha hoja kama WAZIRI lakini hakuafiki mabadiliko hayo kwa madai ya kwamba - SERIKALI ikijisahau hakutakuwa na namna ya kuikumbusha na inaweza ikapelekea TANZANIA 🇹🇿 kuwa ni NCHI ya KIDIKTETA.
Baadae tena, mwaka 1967 wakati wa AZIMIO LA ARUSHA - OSCAR SALATHIEL KAMBONA alipingana na HAYATI MWALIMU kwenye suala la UJAMAA. Yeye, yaani OSCAR SALATHIEL KAMBONA alisema hivi - "Ni lazima UJAMAA ujaribiwe kwanza kwa sehemu chache za TANZANIA 🇹🇿 kuona kama unafaa au haufai na baada ya hapo kama utazaa matunda, ndipo UJAMAA utumike kwa nchi nzima".
Baada ya mabishano ya FARAGHA ya muda mrefu baina ya OSCAR SALATHIEL KAMBONA na HAYATI MWALIMU, akisaidiwa na RASHID MFAUME KAWAWA, hilo AZIMIO lilipita bila kupingwa.
Na wakati mwingine OSCAR SALATHIEL KAMBONA alinukuliwa akisema ya kuwa - "RASHID MFAUME KAWAWA anaendeshwa na HAYATI MWALIMU na hana maamuzi yake".
Basi baada ya hapo, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alijiuzulu nafasi zake zote za CHAMA na SERIKALI huku akisema kuwa, sababu za kiafya ndio zimepelekea achukue uamuzi huo.
Kuna taarifa zilikuwa zinasema ya kwamba, baada ya kujiuzulu kwa OSCAR SALATHIEL KAMBONA aliambiwa kuwa kuna mpango wa kumkamata na kumtia ndani, hivyo tarehe 26/07/1967 alijikusanya yeye na mkwewe na watoto wake na kuendesha gari mpaka NAIROBI - KENYA 🇰🇪 ambapo alipanda ndege na kuelekea UINGEREZA 🇬🇧.
Lakini pia, kuna taarifa zinazosema kuwa IDARA YA USALAMA WA TAIFA ilikuwa inajua OSCAR SALATHIEL KAMBONA anatoroka, ila ilimwacha aondoke ili kuepusha vurugu.
Huku nyuma kulikuwa na maneno ya kwamba OSCAR SALATHIEL KAMBONA ameondoka na PESA nyingi sana lakini OSCAR SALATHIEL KAMBONA alivyokuwa UINGEREZA 🇬🇧 alikanusha vikali na kuomba SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 iwasiliane na SERIKALI YA KENYA 🇰🇪 ili kupata uhakika lakini SERIKALI YA TANZANIA 🇹🇿 haikufanya hivyo.
Kutokana na matukio yale, hotuba ya HAYATI MWALIMU ya mwaka 1969 kwenye sherehe ya SIKU YA MAPINDUZI, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikejeliwa na kuimbwa na WANAFUNZI WA SHULE pamoja na MAJESHI ya NCHI nzima. Nyimbo nyingi za kumkejeli OSCAR SALATHIEL KAMBONA zilitungwa MASHULENI pamoja na MAJESHINI.
Mwaka 1969, OSCAR SALATHIEL KAMBONA na wenzake saba [ 7 ] akiwemo BIBI TITI MOHAMMED walishitakiwa kwa kosa la UHAINI, ikidaiwa walikuwa wamepanga njama za kufanya MAPINDUZI dhidi ya SERIKALI ya HAYATI MWALIMU. Kwenye ile kesi kuna watu ambao walifungwa miaka kumi [ 10 ], wengine walifungwa MAISHA ila OSCAR SALATHIEL KAMBONA kwa sababu hakuwepo TANZANIA 🇹🇿, yeye MAISHA yaliendelea kama kawaida.
Lakini pamoja na haya yote, OSCAR SALATHIEL KAMBONA huwa anafananishwa na MWANASIASA KIJANA kutoka nchi ya KENYA 🇰🇪 aliyekuwa anaitwa TOM MBOYA.
Masaibu, matukio ya kisiasa na mambo waliyoyapitia hawa WANASIASA wawili karibia wote wanafanana.
Na baada ya kuanzishwa kwa MFUMO WA VYAMA VINGI mwaka 1992, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alitangaza kurudi TANZANIA 🇹🇿 kwa masharti ya SERIKALI isije ikamkamata.
Baada ya kurudi TANZANIA 🇹🇿, OSCAR SALATHIEL KAMBONA aliitisha mkutano mkubwa wa KISIASA kwenye UWANJA WA JANGWANI - DAR ES SALAAM, ukiwa na malengo ya kuwaeleza WATANZANIA kilichomfanya kuwa mkimbizi na uchafu wa VIONGOZI WAKUBWA WA SERIKALI.
Kwenye ule mkutano alisema HAYATI MWALIMU ni MTUSI wa RWANDA 🇷🇼! RASHID MFAUME KAWAWA na HAYATI BENJAMIN MKAPA ni watu wa MSUMBIJI 🇲🇿 na huku JOHN MALECELA ni MKONGOMANI 🇨🇩.
Pia alidai HAYATI MWALIMU na RASHID MFAUME KAWAWA wameficha PESA nyingi sana ULAYA 🇪🇺. Kwa kuwa OSCAR SALATHIEL KAMBONA alikuwa hana ushahidi, basi watu wengi walimpotezea na umaarufu wake ulianza kupungua tangu siku ile.
Baadae OSCAR SALATHIEL KAMBONA alianzisha CHAMA CHA KISIASA cha TADEA ambacho hakikufanya vizuri KITAIFA. Na kipindi hicho alikuta hii JAMII ya MWASHITA yaani SIMBA 🦁 yaani wale wenyeji wa hii MIKOA MITATU [ 3 ] ya MWANZA, SHINYANGA NA TABORA walikuwa tayari wameshaanza kujijenga KIUCHUMI na KISIASA kupitia CHAMA CHA WANANCHI - CUF ☀️.
Mwaka 1997, OSCAR SALATHIEL KAMBONA alifariki dunia nchini UINGEREZA 🇬🇧 na walifuatana na ndugu yake OTIMI SALATHIEL KAMBONA. Huku kwa miaka michache ya baadae mtoto wake wa kwanza, pia alifariki kwa mazingira ya kutatanisha nchini UINGEREZA 🇬🇧. Hali hii ilileta sintofahamu kubwa sana kwa WATANZANIA.
Mwili wa OSCAR SALATHIEL KAMBONA ulirudishwa TANZANIA 🇹🇿 na kupokelewa na aliyekuwa WAZIRI WA MAMBO YA NJE kwa wakati huo na RAIS WA AWAMU YA NNE [ 4 ], Ndugu JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Licha ya kuwahi kuwa marafiki wakubwa, HAYATI MWALIMU hakuhudhuria MSIBA wa OSCAR SALATHIEL KAMBONA. [
Itaendelea.. ]