Tanzania ya viwanda inaendelezwa. Magari mia moja yaundwa Tanzania

Aina hiyo ya watu ndio sasa hivi wenye sauti kubwa ndani ya nchi hii, sasa utashangaa nchi itaendelea vipi ikiwa na watu wa aina hiyo, tena wengi wao ndio wanaoshikilia madaraka makubwa ya maamuzi ya hatma ya nchi.

Tuombe sana Mungu atusaidie kuibadili hali hii, vinginevyo taifa hili halina matumaini kabisa.
 
Ungekuwa hai ungejua kwamba tukiwahi kuwa na kiwanda cha kuunda Scania hapa. Lakini kwakuwa ndo umefufuka basi furahia mwanga wakati tunafanya Demagufulication
Tena zile Scania roho ya paka! Daah maisha yanabadilika sana
 
Kiwanda au Karakana ya Kuunganisha vifaa vya magari kutoka Ng'ambo...

Hata Japani hawana viwanda vya kutengeneza magari kwa taarifa wana vya kuunganisha magari.Injini za magari hawatengenezi wao wananunua makampuni ya kutengeneza injini,pia gia box hawatengenezi wao wananunua.Tairi pia hawatengenezi wao wananunua makampunu ya kutengeneza matairi.Nyaya za umeme unazoziona kwenye magari hawatengenezi wananunua unajidharau bure tu
 
Naona mnatukanana tu bila hata hoja ya kunufaisha wasomamaji. Kuna mtu kauliza bei ya hizo gari hakuna hata mtu mmoja aliyekuja na jibu!! Tuambieni hizo gari hata kama wanaunganisha tu hapo Kibaha bei yake ni shillingi ngapi?
Ilibidi mpandisha uzi autetee kwa kujibu maswali muhimu ya wachangiaji
 
Ni magari ya kochona au ya Kijapan? Hivi tunaenda mbele au tunarudi nyuma?

Tulikuwa na kiwanda cha kuunganisha malorry aina ya scania, matrekta aina Valmet, leo tunajivunia kuunganisha vigari vimekaa kama mikokoteni!!
Tunarudi nyuma baada ya kwenda mbeeereeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…