Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Hata kwenye jambo hili yani nchi yetu imeshindwa kuwa na msimamo kwenye jambo hili ambalo liko wazi kabisa tena linakwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora...
nani kakuambia hakuchokozwa? Unafikiri ni rahisi tu mtu kuamka na kuvamia nchi ingine? Soma historia na usisikilize chanzo kimoja cha habari.

Unaijua NAM (Non Alignment Movement) Unajua maana ya Ukraine kujiunga na NATO, unajua Minsk Agreement?? Unajua historia ya Cold War? Vyote hivi vinahusika, usipovifahamu basi upepo wa magharibi utakupeleka kila unapoenda!!
 
Nchi 135 zimepiga kura kuunga mkono na kutetea mipaka ya kinchi ya Ukraine, isipokuwa nchi 5 zimepiga kura kupinga . Na nchi 35 hazikupiga kura ya kuunga mkono au kukataa. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania...
Tanzania imekuwa banana republic siku hizi. Nchi ya ovyo ovyo isiyo na msimamo. Ni kama popo. Mnyama yupo ndege yupo. Tumesahau tulivyovamiwa na Idd Amin na kuomba support duniani.
 

Hii ishi ipo tangu enzi za nyerere yaani kuwa haifungamani na upande wowote(mrengo wa kati) hivyo ni ngumu kushiriki maana tangu mwanzo walishajitoa
 
Engineer soma hio!

 
Labda hiyo inasababishwa na Tanzania kutokujua kiini cha tatizo kilipo, waziri wetu wa mambo ya nje hajui kinachoendelea, tunaogopa kuchagua upande tugeuke bendera fuata upepo, tupo tupo tu.
Hii nayo ni point nzuri.
 
Ila swali kwanini watushirikishe mambo ya ukraine?
Huku ni kutiana ubaya.
Maana ukiwa huku yule atanuna ukiwa kule wa huku atanuna.
Na Vita vikuu vya 3 vya dunia viongozi wa africa msikubali kuingia katika Vita ambayo haiwahusu waacheni watwangane wenyewe
 
Nchi 135 zimepiga kura kuunga mkono na kutetea mipaka ya kinchi ya Ukraine, isipokuwa nchi 5 zimepiga kura kupinga . Na nchi 35 hazikupiga kura ya kuunga mkono au kukataa. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania...
Hiyo kura inasaidia nn mbele ya Marekan na Urusi wakiamua kufanya jambo lao? Mbona hakuna kura ya kupinga na kutetea mipaka ya Palestina? Ukraine ni nan haswa!
 
Sasa mtu una akili timamu unalipwa mihela mingi , unapanda ndege ukaae kimya kwenye chumba cha uchaguzi?
Wala usishangae, Nyakati za uchaguzi wapo watu wanaotumia nguvu kupata kitambulisho cha kura na kujiandikisha kwenye list ya wapiga kura ila saa ikifika hawapigi kura. Binadamu ni kiumbe complicated. Pana fursa ya safari,imepokelewa watu watapata posho n.k ila maekezo ni kura isipigwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…