Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Kuna baadhi ya mambo yanahitaji hekima kubwa saana katika kuyaamua, hayako kama wengi tunavyoyaona,

Kwenye hili suala la mzozo wa Ukraine na urusi nyuma ya Hawa Kuna mengi saana yanaendelea bila ya wengi kujua.

Watu wanahitaji washirika na uungwaji mkono kwenye kuhalalisha baadhi ya mambo kwa maslahi yao mbaya zaidi wanaomia Ni watu.

Katika suala hili binafsi naona Ni vyema nchi yetu kutoegemea kokote kama ilivyofanya ili kuendelea kuusoma mchezo wa huu mgogoro.

Watu wanacheza na akili za watu wengine hapa kwa lengo la kumpandisha au kumshusha mwingine kwenye nguvu ya dunia.

Sikuzote kwenye mtego wa mvuvi aumiae Ni chambo, wewe shuhuda ukiwa kimbelembele yatakukuta ambayo sio yako.

Hi Vita ingekuwa imeisha mapema saana kama Ni kweli wanaopigana mi Ukraine na urusi ila kiukweli naamin mambo hayako hivo na ndio maana inadumu mpaka kesho.

Suala la nchi nchi yetu kutokuwa na msimamo sio kweli maana kwenye huu mchakato kulikuwa na misimamo mitatu ikiwemo kutoegemea upande wowote, kwahyo nchi yetu imeamua kuwa kwenye upande huu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado hujapata akili siku wakikutoa puru nje ndo utaelewa
Niko timamu sana kichwani sio kama wewe ambae akili ni za kuvukia barabara tu.
Jitahidi kuwa na busara na kufikiri otherwise uzee wako ni kuchekwa na wa hovyo sana!
 
Ukraine yote itachukuliwa kurudi Urusi kama zamani (USSR)...
 
Achen unafiki nafik basi na ujuaji usio nampango.
Zingatien pia historia.

Mbona Tanzania na Nyerere alipopiga kelele kuhusu vurugu za Idd Amin kuhusu eneo la Kagera Dunia ilikaa kimya???

Tanzania na Nyerere huyo huyo alipoweka bayana kuunga mkono BIAFRa kujitenga huko nigeria mkamnanga kuwa anaunga mkono Ugaid na uhaini

Rais Tshekedi Felix hapo DR Congo ni juzi tu anapiga kelele kuingiliwa na Kiuvamizi na vikosi vinavyofadhiliwa na Rwanda mbona Dunia imenyamaza??

Mifano iko miingi sana ila kwakifup ni kwamba hakuna mtu anayewaza kuja kukupambania kama usipojimbania mwenyewe.
Kila mtu yuko busy na mambo yake hizo habar za kura ni formalities tu za kijinga ili ukijichanganya wajanja wakusome

Sisi ni nchi isiofungamana na uoande wowote ndio sera yetu hivyo tukipiga kura well and good na hata tusipopiga pia ni sawa hiyo yote ni misimamo yetu kama nchi
 
Safi sana acha wapambane na vita yao.
Mbona hawakutuita tukapige kura kutambua uhuru wa nchi ya libya, afghanistan, syria na kwingine hata iraq? Acha wacheze show yao wenyewe
 
Safi sana Tanzania
Mambo yao watajua wenyewe
Tupige kura tusipige Hatuwezi Badilisha Kitu
Nimependa United Republic of Tanzania ilivyopiga kura, kwa hii kumbe mama anamsimamo bora sana, anajiheshimu anaheshimisha Nchi! Rais napenda awe na msimamo unaotabirika!
 
Hata kwenye jambo hili yani nchi yetu imeshindwa kuwa na msimamo kwenye jambo hili ambalo liko wazi kabisa tena linakwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora!

Urusi imevamia Ukraine bila kuchikozwa ,urusi inaendelea kushambulia ukraine! Kuna mambo kweli tusifungamane na upande wowote lakini kwenye swala kama hili liko wazi ni wazi Tanzania ni nchi ya waoga na ya ajabu sana ambayo haiwezi simamia chochote!

Hii shida inaanzia kwa kiongozi wajuu! Shida ya Rais Samia anataka kuonekana mwema kwa kila mtu huku anataka aonekane mtenda haki wakati hapo hapo anapinga haki!

Nchi yetu inashida ya uoga!
Hayatuhusu hayo mambo !! Nchi nyingi tu zilishavamiwa tukakaa kimya kabla ya huu uvamizi !! Sisi ni miongoni mwa Non aligned countries !!
 
Nchi 135 zimepiga kura kuunga mkono na kutetea mipaka ya kinchi ya Ukraine, isipokuwa nchi 5 zimepiga kura kupinga . Na nchi 35 hazikupiga kura ya kuunga mkono au kukataa. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania.

Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.

Sisi tuna ugomvi wa mpaka kati yetu na Malawi, iwapo Dunia hasa Mataifa makubwa nayo wataamua kutugeuka na kuwa upande wa Malawi tusianze kulialia.

Angalia upigaji kura ulivyownda

View attachment 2385453
Mtoa mada ilipaswa kumripoti tu, ila maoni yako ya kijinga, Tanzania imepiga kura vizuri sana binafsi nimeridhika, point 3 kwa mh Rais Samia!
 
Naunga mkono kura ya Tz huko UN. "Why?". Soma Minsk Agreement. Tafakari kauli ya Papa Francis " Urusi imeivamia Ukrein kwa sababu NATO imeenda kubweka mlangoni mwa Russia"
 
Kwa lugha nyepesi Tanzania ni team Putin,hatuna nguvu ya kijeshi,kiuchumi na kisiasa. Hatuwezi kuitangazia Dunia msimamo wetu kama nchi. Ila tumeweka mtego wwtu hapa. Putin njoo uichukue Tanzania iwe sehemu ya Russia,tupo tayari kupiga kura.
 
Nchi 135 zimepiga kura kuunga mkono na kutetea mipaka ya kinchi ya Ukraine, isipokuwa nchi 5 zimepiga kura kupinga . Na nchi 35 hazikupiga kura ya kuunga mkono au kukataa. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania.

Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.

Sisi tuna ugomvi wa mpaka kati yetu na Malawi, iwapo Dunia hasa Mataifa makubwa nayo wataamua kutugeuka na kuwa upande wa Malawi tusianze kulialia.

Angalia upigaji kura ulivyownda

View attachment 2385453
Malawi akijichanganya tunamfua mapema.
 
Wananchi wa Tanzania nao waonesha msimamo wao :

Lviv, Ukraine 🇺🇦

Bobi Wine na Zitto Kabwe waonesha mshikamano na Ukraine.

Kwa pamoja mbali ya mazungumzo na viongozi wa Ukraine wakiwa mji wa Lviv pia wametoa kibao kikali cha video kuonesha Ukraine inaungwa mkono ktk mapambano dhidi ya mvamizi na raia wa, Ukraine wasijisikie upweke kwani jumuiya ya kimataifa ipo pamoja nao.

Zitto Kabwe and Robert Kyagulanyi Ssentamu, joined The Brenthurst Foundation on a field-trip to Ukraine


28 September in 2022, in the seventh month of the war launched by Russia against Ukraine, two African politicians, Zitto Kabwe and Robert Kyagulanyi Ssentamu, joined The Brenthurst Foundation on a field-trip to Ukraine, the fifth by the Foundation since the war started.

At the conclusion of the visit, Robert, better known by his stage name Bobi Wine, recorded two solidarity songs in Lviv with the local band String Mockingbird, both featuring Sofia Grabovetska, and written by Greg Mills, Robin Auld and Bobi. The production was managed in real time from Jenny Records in Lviv and Murray Anderson at Milestone studio in Cape Town. This is the first of the tracks, based on the original production of ‘Alone But Altogether’.

Source : The Brenthurst Foundation
 
It will be so hard for Tanzania to vote against Russia because of the close relationship we've had with them for centuries
 
Back
Top Bottom