Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Kama ilikua ni lazima kila nchi ichagie upande kulikua na haja gani ya kuweka option ya nchi kutokua na upande wowote? Na kama Russia kafanya kosa kuvamia Ukraine kuna haja gani tena ya kupiga kura si ishajulikana kafanya kosa kama adhabu ipo aadhibiwe, kura za nini tena?
 
mbona urusi hana wivu na nchi yako yenye siasa ya demokrasia

vita gani? hii ni oparation ya kawaida ya putin, vita kamili NATO akitia maguu
Kwani Zanzibar itakapoamua kujitenga na bara nakutaka kujiunga na Kenya wataonekana wamewakosea bara? Kwa vipi kwani Zanzibar si nchi huru?.Urusi waharibu miundombinu ya ukrein na kuua raia halafu Manashabikia ?
Na kwa kua huyo nyoka anaelekea kushindwa macho yake yanatazama silaha za nuklia,Ulimwengu unaelekea wapi?
 
Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.
Siyo rahisi kiasi hicho unachofikiria wewe mkuu 'Missile of the Nation.'
Jaribu pia kupanua wigo wako wa kujuwa tatizo linatokana na nini hasa katika mgogoro huo kabla ya kufikia hitimisho kama hili.
Huwezi kamwe kulinganisha kutwaliwa kwa Kagera na hayo yanayoendelea huko. Ni mifano isiyoshabihiana kabisa.
Hata hivyo, unakumbuka hao wakubwa wakilaani Nduli kuvamia?
Kama hukuwepo, hebu jaribu kusoma historia inasemaje kuhusu swala hilo.
 
Kwenye suala la Israel na palestina nchi ili simama na wapalestina weka kumbukumbu zako vzr.
Tatizo watoto wamezidi humu. Mwalimu Nyerere wala hakupepesa macho kuilaani Israeli na ndicho kisa cha kufunga ubalozi wa Israel na kuwatimua. Ujenzi wa hoteli ya KIlimanjaro uliokuwa unasimamiwa na Israel ilibidi usitishwe na Waisraeli waondoke Tanzania. Tanzania ilikuwa na msimamo, haikuwa popo kama ilivyo hii leo.
 
Na sisi siku Muungano ukivunjika mpaka wetu na Zanzibar sijui itakuwaje?
Njia pekee ya hilo unalowaza kuwezekana ni kwa Zanzibar kujikabidhi kwa mkubwa mwenye uwezo wa kufunga lango letu kuu pale baharini.
Hawe wengine wote hakuna namna ya kuiachia Zanzibar kwa vyovyote.
 
Ukitaka kuzurumu Mali ya mtu lazima nawe umuunge mkono au umsapoti,mzurumaji
Hivi hujui sisi hatuna chetu kwenye ziwa nyasa kwa mujibu wa ramani ya wakoloni? Ila hakuna namna lazima tuwalazimishe tugawane ziwa maana nasi tunahoja za msingi
 
Watu mnao washadadia

Ila africans tumelogwa
 

Attachments

  • VID-20221013-WA0045.mp4
    990.9 KB
Safi sana, tumegoma kutumiwa na mabeberu ili kulinda maslahi yao.
Kama ni territorial integrity wao wanafanya nini Syria? Wamevamia nchi huru na mipaka yake na kazi wanayofanya huko ni kuiba mafuta tu! Waliivamia Iraq kwa sababu za uongo za kutunga, kwani haikuwa na territorial integrity?
Safi sana Tanzania, sisi hatupendi ujinga
 
Hili genge la CCM wajaa laana ,vibaka ,wezi na wauaji hawa mlitegemea wasimaie Haki hawa mbw@?
Ifike mahali nchi za kipumbav zinazotetea maovu kama hii Tanganyika zikivamiwa au kupatwa na majanga mengine zitengwe Tu na zisipewe msaada wowote ,the world should act neutral towards hypocritical regimes & tyranny sympathisers
 
Tanzania imekuwa banana republic siku hizi. Nchi ya ovyo ovyo isiyo na msimamo. Ni kama popo. Mnyama yupo ndege yupo. Tumesahau tulivyovamiwa na Idd Amin na kuomba support duniani.
Na scenarios za uvamizi WA Idi Amin Kule Kagera ni zilezile kama Yule mpuuz Putin pale Ukraine
 
Hii ishi ipo tangu enzi za nyerere yaani kuwa haifungamani na upande wowote(mrengo wa kati) hivyo ni ngumu kushiriki maana tangu mwanzo walishajitoa
Hakuna kitu kama Hicho ,huo ni unafiki Tu na kutetea makomunist aka nchi washirika ndio kauli mbinu ya CCM , mbona serikali ya ccm hiyo hiyo huwa inapinga uvamizi na uonezi WA walowezi WA kiyahudi pale Israel ?
Ila likija suala linalohusu China,Russia ,Cuba ,north Korea na makomunist wengine ndio unafiki WA Non alignment movement ,what a stupid and pathetic argument that is
 
Anaewapigisha kura ni US aliomtoa ghadafi, ,huko Iraq palestina anaua kila leo, huyo huyo aliomdhoofisha Mugabe na bado mko Kama mazuzu
We ni mwehu mmarekani anaua palestina na Iraq sio ?
 
Huko nje ya Afrika, wenye akili kama zetu ni ;
Sri lanka
Vietnam
Uzubekstan
Armenia
Kyrgyzstan
Lao PDR
Mongolia
Pakistan
Tajikstan
Thailand
Hondurus.

What do we have in common with these countries?
Kuna chochote cha kujifunza hapa mkuu?
 
Kwamba China nayo ni Nchi waoga[emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…