Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Tanzania yagoma kupiga kura ya kuunga mkono Mipaka ya nchi ya Ukraine(Territorial Integrity) huko UN

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nchi 135 zimepiga kura kuunga mkono na kutetea mipaka ya kinchi ya Ukraine, isipokuwa nchi 5 zimepiga kura kupinga . Na nchi 35 hazikupiga kura ya kuunga mkono au kukataa. Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania.

Inashangaza sana nchi yetu ambayo imewahi kupigana vita kulinda Territorial Integrity ya nchi yetu leo inashindwa kusimama na kuiambia dunia kuwa mipaka ya nchi nyingine iheshimiwe.

Sisi tuna ugomvi wa mpaka kati yetu na Malawi, iwapo Dunia hasa Mataifa makubwa nayo wataamua kutugeuka na kuwa upande wa Malawi tusianze kulialia.

Angalia upigaji kura ulivyownda

20221013_070850.jpg
 
Hata kwenye jambo hili yani nchi yetu imeshindwa kuwa na msimamo kwenye jambo hili ambalo liko wazi kabisa tena linakwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora!

Urusi imevamia Ukraine bila kuchikozwa ,urusi inaendelea kushambulia ukraine! Kuna mambo kweli tusifungamane na upande wowote lakini kwenye swala kama hili liko wazi ni wazi Tanzania ni nchi ya waoga na ya ajabu sana ambayo haiwezi simamia chochote!

Hii shida inaanzia kwa kiongozi wajuu! Shida ya Rais Samia anataka kuonekana mwema kwa kila mtu huku anataka aonekane mtenda haki wakati hapo hapo anapinga haki!

Nchi yetu inashida ya uoga!
 
Kwa maana nyingine tunaunga mkono uporaji wa ardhi ya nchi nyingine.

Hapakuwa na sababu ya kuwa neutral wakati jambo lililofanywa na Urusi ni la kijinai kila mtu ameshuhudia.

Hadi ifike mahali nchi yako imevamiwa na kuporwa sehemu ya ardhi yako ndo uone umuhimu wa kutetea uhuru na mipaka ya nchi.
 
Vipi kuhusu US anapovamia ardhi za nchi zingine? vp Israel anapovamia ardhi ya Wapalestina? hiyo imekaaje yenyewe?
 
Bora hata Resolution ingehusu Urusi kuvamia Ukraine hapo tungeweza kujibaraguza na kuabstain LAKINI kura inahusu kutambua na kuheshimu mipaka ya Ukraine ambaye ni mwanachama mwenzetu wa UN , ambaye kasaini articles za kila nchi kuheshimu mipaka ya nchi nyingine kama sisi tulivyosaini, tunashindwaje kulinda hii principle kwa Wivu mkubwa?
 
Kwa maana nyingine tunaunga mkono uporaji wa ardhi ya nchi nyingine.

Hapakuwa na sababu ya kuwa neutral wakati jambo lililofanywa na Urusi ni la kijinai kila mtu ameshuhudia.

Hadi ifike mahali nchi yako imevamiwa na kuporwa sehemu ya ardhi yako ndo uone umuhimu wa kutetea uhuru na mipaka ya nchi.
Tunaunga mkono uporaji wa halali kama alivyofanya Urusi maana na sisi tunataka tuirudishe Rwanda na Burundi kwani ilikuwa sehemu ya Tanganyika enzi za Mjerumani
 
Vipi kuhusu US anapovamia ardhi za nchi zingine? vp Israel anapovamia ardhi ya Wapalestina? hiyo imekaaje yenyewe?

Heri nimepata mtu mwenye ufahamu wa ndani walahi
US kamtoa Ghadafi wetu, huko Syria ndio usiseme Palestina wanachinjwa kama kuku kila iitwayo leo! Kama wanashindwa kuheshimu nchi na jadi zake sembuse mipaka? Grow up jamani uwiii [emoji3062]
Ehh jamani watu mtakuwa lini mfahamu hizi mbinu za makaburu jamani?
Ewe kijana amka uisome history ya nchi yetu Tanzania [emoji1241] ndio maana Mwalimu Nyerere akasema Tanzania [emoji1241] haita fungamana na upande wowote!
Angalia hapo Kenya, mtu alie zaliwa masikini anakufa na umasikini wake! Kila eneo limeshikwa na makaburu!
Mshukuruni sana Mwalimu!
Asante Mama yetu Samia kwa kufuata nyayo za Mwalimu!!!
 
Back
Top Bottom