Mkurugenzi wa Africa CDC ameelezea kuwa na wasi wasi na jinsi Tanzania inavyopambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Dr. John Nkengasong ameieleza BBC kwamba hakuna takwimu za kutosha zinazoweza kutumika kuelewa hali halisi iliyopo Tanzania, amesema taasisi yao (CDC) iliweka mkakati wa kiushirikiano wa kimataifa kwa nchi zilizopo katika bara la Africa kuhusu namna ya kukabiliana na virusi hivyo.
Dr. Nkengasong amenukuliwa akisema "Tunaendelea kuwa na matumaini na kuwaomba Tanzania waje mbele na kusema hali halisi iliyopo Tanzania ili tuweze kushirikiana kuviondoa virusi hivi nje ya bara la Africa".
Aidha amehimiza umuhimu wa nchi zote za Africa kushirikiana katika mapambano hayo, Dr. Nkengasong amesema "Tumeendelea kujaribu kuwasiliana na Tanzania lakini hatupati majibu tunayoyatarajia".
Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania "imeokolewa" kutoka kwa virusi hivyo na hakuna virusi vya corona nchini Tanzania. Tanzania inajiandaa n a uchaguzi mkuu mwezi Oktoba na ipo katika mhemko wa uchaguzi, watu wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuvaa barakoa ama kupeana nafasi.
======
The director of Africa Centre for Disease Control has expressed concern about Tanzania's handling of the coronavirus pandemic.
Dr John Nkengasong told BBC's Newsday that there was no enough data to determine the situation in Tanzania.
He said the centre had developed a continental joint response strategy to be able to defeat the virus.
"We continue to hope and plead that Tanzania could come forth and report the situation as it is so that we can work collaboratively to stem this virus out of the continent," he said.
He emphasised on the need for all African countries to work together.
"We continue to reach out [to Tanzania] but we are not having the response that we expect," he said.
Tanzania's President John Magufuli has insisted that his country has been "saved" from the virus and declared the country virus free.
The country is getting ready for October elections and is an electioneering mood. People have been going about their business with no masks or social distancing.
Source :
BBC