field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 2,061
- 4,686
Tunalipwa 17% kwa ajili ya uvivu wa serikali yetu. Tulikuwa na idara ya Geology ya University of Dar es Salaam tangu mwaka 1961, tumeshindwa kupeleka wahitimu field ili kutafuta madini, gas, petroleum etc, wapo wanakaa ofisini. Badala yake tunaingia Sharing agreement (PSA) na nchi zingine au na watu wenye fedha.....Mnawaita mabeberu, halafu tunaambulia asilimia 17 tu. Nchi za kiarabu na Iran, baada ya uhuru zilikataa huu utumwa na kufanya mambo yao wenyewe, Wakichimba Helium, gas au chochote kile iwe mafuta etc, asilimia 100 inabaki nchini kwao kuendeleza nchi zao. Sisi hapa tunafurahia kupewa 17%. NI UPUMBAVU. Kuna habari kuwa gesi ya helium inaweza kuzalisha US$ Billion 7.2 mpaka iishe, kwahiyo tunachokipata ni USD 1.2 Bil, halafu watu mnapiga kelele nyingi kuwa tunafaidika? wao wamekula US$ 6.0 Bil, na ukitoa gharama za vifaa na kulipa watu, wanakula USD Bil.5 .Kwahy wenye Mali tunalipwa 17% au nimeona vibaya🙄🙄
Kwa jinsi hii tutaendelea kweli? Yatabaki mashimo tu.