Tanzania yajitetea Umoja wa Mataifa tuhuma za Kutesa, Kudhalilisha Wanaharakati

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Dk Abdallah Possi ametoa utetezi katika Baraza la Haki za Binadamu ofisi ya Geneva, Uswisi, kuhusu madai ya kutesa na kudhalilisha wanaharakati.

Tanzania Yajitetea Umoja wa Mataifa Tuhuma za Kutesa, Kudhalilisha Wanaharakati, Yasema Inachunguza

Tanzania imejibu tuhuma zilizofikishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, juu ya kuwatesa na kuwafanyia udhalilishaji unaotweza utu wa binadamu, wanaharakati Agather Atuhaire kutoka Uganda na Boniface Mwangi kutoka Kenya, waliokamatwa mnamo Mei 19,2025 walivyokuja kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu.

Akijibu hoja zilizowasilishwa na shirika la East and Horn of Africa Human Right Defenders Network, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Abdallah Posi, alisema wanaharakati hao hawakusema sababu ya ukweli iliyowaleta Tanzania.

"Pamoja na kuwa shutuma zao dhidi ya serikali zina mashaka makubwa, tunayachukulia kwa uzito mkubwa madai ya kuteswa,unyanyasaji wa kingono na vitendo vya ukiukaji wa maadili. Ndio maana serikali kwa sasa inachunguza, na ikithibitika, wahusika watachukuliwa hatua," alieleza Balozi Posi leo Juni 18, 2025.

Video

Your browser is not able to display this video.
 
Wale waliokokeza kuwa washughulikiwe, je wana maoni gani?

Kiongozi mjanja anapaswa kukwepa mtego unaotegea kweupe, mchana
 
What else?
 
Pamoja na kuwa shutuma zao dhidi ya serikali zina mashaka makubwa, tunayachukulia kwa uzito mkubwa madai ya kuteswa,unyanyasaji wa kingono na vitendo vya ukiukaji wa maadili. Ndio maana serikali kwa sasa inachunguza, na ikithibitika, wahusika watachukuliwa hatua," alieleza Balozi Posi leo Juni 18, 2025.🥺😡
 
Maneno ya kutongozea haya
 
Mbona into yako umeandika para zote tatu za mwanzo unarudia maneno hayo hayo?

Pia pamoja na kuandika into para 3 lakini haiziju maswali ya 4 'W' and 1 'H' habari nzuri lakini umendika kama vile unaharaka ya kumuwahisha mgongwa wa corona hospitali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…