Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,559
- 3,586
Huyu jamaa ana akili kweli?Serikali ya Tanzania imekanusha madai yaliyotolewa na wanaharakati wa Kenya na Uganda, Boniface Mwangi na Agather Atuhaire kuhusu kufanyiwa unyanyasaji wa kingono baada ya kushikiliwa nchini.
Akizungumza kwenye mahojiano na DW Kiswahili, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema madai hayo yaliyotolewa hayana ukweli na yana nia ya kuichafua Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.
"Hii nchi ina heshima zake, inaheshimiwa na kila mtu na watu wote wanaifahamu Tanzania, wao si watu wa kwanza kuja Tanzania, watu wengi wamekuja Tanzania. Kama wao wanakwenda kuzalisha tuhuma zao za uongo, wacha waendelee kufanya lakini Tanzania haiko hivyo. Wao walivunja sheria, wamechukuliwa hatua," amesema.
View attachment 3355009
Huyu jamaa anakula bata tu na inaonesha wazi kabisa kuwa hayuko aware na kilichofanyika na kinachoendelea kufanyika sasa nchini cha kuteka, kunyanyasa na kuuwawa watu bila kufikishwa mahakamani...
Walivunja sheria ipi? Na hata hasemi ni hatua gani za kisheria zilizochukuliwa
Labda kwa Polisi wa Tanzania kukamata raia wa kigeni kuwanyanyasa kingono, kuwavua nguo na Kuwabaka kama walivyofanya kwa yule mwanamke Mganda (Agather Atuhaire) na kumlawiti yule Mkenya (Boniface Mwangi p) ndiyo hatua zenyewe za kisheria anazomaanisha huyu msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa!