Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous

Tanzania yakataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge Selous

Serikali kujenga mradi kwenye hifadhi sawa.. Mbowe kuwekeza kilimo hapana...

Hivi sheria za mazingira zinasemaje...wasije wakajenga mradi huo mkuu wa wilaya akaja na kamati ya ulinzi akang'oa mashine zote.

Sent from my TECNO-C7 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo unatakaje
 
Nashindwa kuelewa humu watu mnafurahia adhari za kimazingira zinazoenda kutokea kutokana na ujenzi huo ndani ya hifadhi.
Isitoshe umeme wa maji kwa karne hizi si umeme tena kutegemea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni.
Gesi tunayo ya kutosha, makaa ya mawe tunayo pia na vyanzo vingine mbadala lukuki.

Nashindwa kuelewa why tunashabikia vitu ambavyo madhara yake ni makubwa zaidi ya faida.

Sent from my Lenovo A7600 using JamiiForums mobile app
 
Hao UNESCO warekebishe sheria zao maana sidhani kama 3% za eneo hilo zikitumika zitakuwa na madhara ukilinganisha na ukubwa wa eneo husika.

Task Force12
Wakati wewe HUDHANI wenzio UNESCO wameaply utaalam na kuona kuna madhara. Tunavyo vyanzo na rasilimali nyingi tu za kutupatia umeme, sioni haja ya kuharibu urithi wa dunia kwa kuwa tu vyerehani vi4 vinatumia stima
 
Hakuna mazingira ambayo yanaharibiwa pale kwa sehemu ndogo hiyo ya mradi. Tuache kufikirishwa
Tatizo watanzania wengi mna vichwa vya panzi. Si majuzi tu serikali hii hii ilituambia umeme utakaotokana na gesi asilia ukianza kuingizwa kwenye grid ya taifa tutakuwa na umeme wa kutosha mpaka mwingine tutaanza wauzia nchi jirani!??? Na umeme wa maji utabaki kuwa historia nchini!!?

Sent from my Lenovo A7600 using JamiiForums mobile app
 
Tusubiri utekelezaji.yasijekuwa maneno ya kusadikika tuu kama alivyokuwa akifanya Vasco da...........

Sent from my Leader Plus using JamiiForums mobile app
Bado tu upo ndotoni?
Hostel za UDSM
Nyumba za makazi magomeni
FLY over ubungo.
Reli ya SGR Dar -Moro
Makinikia
TICTS
ESCROW
Kubadili sheria za madini n.kn.k
Yaani Magufuli akiamua anatekeleza tu
 
Tatizo watanzania wengi mna vichwa vya panzi. Si majuzi tu serikali hii hii ilituambia umeme utakaotokana na gesi asilia ukianza kuingizwa kwenye grid ya taifa tutakuwa na umeme wa kutosha mpaka mwingine tutaanza wauzia nchi jirani!??? Na umeme wa maji utabaki kuwa historia nchini!!?

Sent from my Lenovo A7600 using JamiiForums mobile app
Kusema ni moja changamoto ni kitu kingine. Chochote chema kinachofanyika lazima kiungwe mkono.
 
Tanzania Yakataa Agizo La UNESCO La Kuitaka Kusitisha Ujenzi Wa Mradi Wa Stiegler's Gorge Katika Pori La Akiba La Selous

HAMZA TEMBA - WMU
Tanzania imesisitiza uamuzi wake wa kuendelea na mpango wa kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge Hydro Power Project) yaliyopo ndani ya Pori la Akiba la Selous mbele ya wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Watanzania.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa 41 wa wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ambao unaendelea katika Jiji la Krakov nchini Poland, Kiongozi wa msafara huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa mpango huo ulikuwepo katika ajenda ya Serikali ya Tanzania tangu miaka ya 1960's na kwamba ukubwa wa eneo litakalotumika kutekeleza mradi huo ni asilimia tatu tu ya eneo lote la pori hilo ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 50,000.

Aliongeza kuwa, “Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 1982 wakati pori hili (Selous) limewekwa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Asili (IUCN) liliutambua mradi huo wa Stiegler's Gorge kutokuwa na madhara makubwa katika uharibifu wa mazingira ukizingatia ukubwa wa pori hilo na eneo litakalotumika kujenga mradi huo”.

Aliwaeleza wajumbe hao kuwa, Serikali ya Tanzania inatekeleza sera ya kujenga uchumi wa viwanda hali inayopelekea kuwa na mahitaji makubwa ya nishati ya umeme hivyo kwa kuzingatia vyanzo vilivyopo imekuwa ni muhimu sasa kufikiria tena ujenzi wa mradi huo kama chanzo kingine muhimu cha nishati kuwezesha kufikia azma hiyo.

Alisema mradi huo utaongeza uzalishaji wa umeme nchini kufikia asilimia 144.8 hivyo kuondoa upungufu wa nishati uliopo kwa sasa na pindi utakapokamilika utawanufaisha watanzania wengi wanaoishi bila umeme ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji yake ya kuendesha viwanda.

Meja Jenerali Milanzi alilazimika kutoa maelezo hayo kwa kamati hiyo ili kuweka bayana dhamira ya dhati Serikali ya Tanzania ya kuendelea na ujenzi wa mradi huo kwa ajili ya maendeleo endelevu huku akitoa rai kwao kuwa Serikali bado ipo tayari kwa mazungumzo ya namna bora ya kutekeleza mradi huo kwa faida ya jamii, uchumi na mustakbali bora wa mazingira ya hifadhi ya Selous na taifa kwa ujumla.

“Kwa kutumia teknolojia bora zilizopo, mipango imara na usimamizi thabiti, mradi huu utakua na faida kubwa kwa taifa ikiwa na pamoja na kuboresha maisha ya watu maskini na jamii kwa ujumla bila kuathiri mazingira yanayotoa faida hizo”, alisema Milanzi.

Hapo awali, kabla ya mkutano huo, ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu huyo ulifanya mazungumzo na Maafisa Waandamizi wa Kituo cha Urithi wa Dunia na Bodi za Ushauri ya kituo hicho na kuwasilisha kwa maandishi msimamo wa Tanzania kuhusu ujenzi wa mradi huo.

Tanzania ilipinga vikali rasimu ya azimio No. 41 COM 7 A.17 aya ya 7 ambalo liliitaka kusitisha kabisa (to permanently abandon) ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge Hydro Power Project).

Baada ya tamko la Tanzania kupinga azimio hilo kipengele hicho kilifanyiwa marekebisho ipasavyo na neno “to permanently abandon” (kusitisha kabisa) liliondolewa katika azimio hilo kupisha majadiliano zaidi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama zilizosaini mkataba wa urithi wa Dunia wa mwaka 1972 huku ikiwa na maeneo saba yaliyorodheshwa katika urithi huo ikiwepo Pori la Akiba la Selous, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mji Mkongwe (Zanzibar), Hifadhi ya Ngorongoro na Michoro ya kondoa na Kilwa Kisiwani. Aidha, ni mwanachama wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha miaka minne hadi mwaka 2019.

Tokea ijiunge na kamati hiyo mwaka 2015, Tanzania imekua na msimamo wa kuwa na maendeleo endelevu katika ajenda za mikutano yake pamoja na miongozo yake ili kuruhusu kuendeleza maeneo ya urithi wa dunia kuweza kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi bila kuwepo kwa athari kubwa katika mazingira.

Mkutano huo wa 41 wa wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea katika jiji la Krakov nchini Poland umehudhuriwa na nchi wanachama 193 na unajadili mambo mbalimbali muhimu kuhusu uhifadhi na ulinzi maeneo ya urithi wa dunia pamoja na kutangaza maeneo mengine mapya ya urithi wa dunia yaliyowasilishwa na nchi nyingine wanachama katika mkutano huo.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ulijumuisha pia Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa UNESCO, Samwel W. Shulukindo na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii. Mkutano huo ulianza tarehe 2 Julai na unategemewa kumalizika tarehe 12 Julai, 2017.

Muonekano wa mto Rufiji kutokea angani ambao maporomoko yake yatatumika kuzalisha umeme katika mradi unaotarajiwa kujengwa na Serikali wa Stiegler's Gorge.

Sehemu ya mto Rufiji unakatiza katika Pori la Akiba la Selous.

Pori la akiba la Selous lina vivutio vingi vya utalii ikiwemo wanyamapori mbalimbali wakubwa kama Tembo, Simba, Nyati, Chui, Twiga na Viboko.

sawa acha tupunguze wanyama tupate umeme wa viwanda vyetu vipya.
Naipenda TZ yangu.
 
Bado tu upo ndotoni?
Hostel za UDSM
Nyumba za makazi magomeni
FLY over ubungo.
Reli ya SGR Dar -Moro
Makinikia
TICTS
ESCROW
Kubadili sheria za madini n.kn.k
Yaani Magufuli akiamua anatekeleza tu

Reli ya SGR ni mpaka MZ siyo Moro, maana wameisha anza kuwabomolea huko Mz South.
Rufiji Stigler Gorger Power Project umeisahau mkuu.
 
Serikali kujenga mradi kwenye hifadhi sawa.. Mbowe kuwekeza kilimo hapana...

Hivi sheria za mazingira zinasemaje...wasije wakajenga mradi huo mkuu wa wilaya akaja na kamati ya ulinzi akang'oa mashine zote.

Sent from my TECNO-C7 using JamiiForums mobile app
Mkuu yaani unafananisha bustani ya mboga ya mbowe na mradi mkubwa wa uzalishaji umeme (H.E.P)?!

Sent from my HUAWEI G510-0200 using JamiiForums mobile app
 
Serikali kujenga mradi kwenye hifadhi sawa.. Mbowe kuwekeza kilimo hapana...

Hivi sheria za mazingira zinasemaje...wasije wakajenga mradi huo mkuu wa wilaya akaja na kamati ya ulinzi akang'oa mashine zote.

Sent from my TECNO-C7 using JamiiForums mobile app
Usichanganye mazingira na mambo ya urithi wa dunia!

Mbowe ametuwekea kitu inaitwa POPs(Persistent Organic Pollutants) kwenye mazingira ni wa kuogopwa kama ukoma.
 
Maamuzi haya nayafananisha na yale ya Lowassa ya kujenga mradi wa maji wa Ziwa Victoria. Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
hata maamuzi ya richmond vilevile......

Sent from my HUAWEI G510-0200 using JamiiForums mobile app
 
Wao walitaka kujenga viwanda vya nucleur wako mbele kama.....
Leo sisi tunajenga mfumo wa umeme wao wanaleta kihele...
 
kama vipi hao unesco walichukue hilo eneo walipeleke huko kwao.
 
Wakati wewe HUDHANI wenzio UNESCO wameaply utaalam na kuona kuna madhara. Tunavyo vyanzo na rasilimali nyingi tu za kutupatia umeme, sioni haja ya kuharibu urithi wa dunia kwa kuwa tu vyerehani vi4 vinatumia stima
Nchi wana chama wana wivu tu lakini sio mbaya hata wakiitoa tutabaki na 6 zitatutosha maana wamekuwa wakitupigia kelele kwa muda mrefu,ila kuhusu suala hili hamna namna sasa lazima tujitoe kafara maana kiasi cha umeme kinachozalishwa hakitoshi kuendesha hivyo viwonder vya cherehani nne.

Task Force12
 
hivi kati ya tembo wakiopo ktk hifadhi na watanzania nan ana thamani kubwa?

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app

Aliuliza swali mb wa serengeti chadema "mtu akiua tembo fain ni 25 Milion, lakini tembo akiua mtu fidia ya serikali ni 400,000 tsh" ?
jiulize kwanini?
dhahabu ikikutwa kwenye eneo lako ni ya serikali lakini ikiwa bangi ni ya kwako ?
 
Safi kabisa. Kipindi hiki Hatutaki kusikiaga upuuzi eti athari za mazingira na kadhalika. Mradi tunautaka zaidi ya kutunza hayo mazingira tena ni asilimia 3 itakayotumika kwenye mradi. Kwa hiyo UNESCO waanze kujityuni kuzungumzia asilimia 97.
Hivi Mbowe nae kule Moshi ametumia Asilimia Ngapi... hawajaona na kumlalamikia wanataka kuzuia Mto rufiji! UNESCO wakakae KIBITI
 
Back
Top Bottom