Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
watanzania sio kwamba hawataki kutoka nje ya nchi? Serikali ndio tatizo. Imagine mpaka leo kupata passport ni ishu kubwa sana ambayo hadi uipate kuna urasimu ndani yake?

Kuna mambo mengi ambayo uki dig deeper utajua kwanini serikali huwa inabana watu wengi wasiondoke bongo?
 
IMG_20230519_020137_338.jpg

Watz lazima tukubali, we are very unique creatures.
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Dah ! Nimecheka sana
Ila fresh tutafika tu
 
Hizi zote ni mbinu za kiutawala kuwafanya raia wake wasitoke nje ili wasiwe na exposure ambayo wakirudi bongo ule ujinga ujinga wa kina mwiguli wataukataa..
 
Roho mbaya tu anayetangulia hataki wengine wafike huko

Ni kweli kabisa, Passport ni haki ya kila raia ila nchi yetu kuna bureaucracy ya hali ya juu saana kupata hiyo passport
Kwa hiyo unataka kusema ni urasimu na kukosekana kwa pasi ndio maana Watanzania ni wachache kwenye Diaspora?

Hii ipo kwa watanzania tu sijui kwanini
Haijalishi kila mtu atadadavua ripoti hiyo kwa namna yake, unaonekana ripoti imekukasirisha kuona Watanzania sio wengi kwenye Diaspora kana kwamba ni kitu kibaya au? Aikambee
 
Kiswahili ni janga Kiswahili ni umaskini.Kukumbatia Kiswahili ni kujichelewesha tu bila sababu ya msingi,hicho Kiswahili utakiongea wapi? Watu wanaogopa kwenda kutafuta fursa nje ya nchi kwa sababu ya lugha huo ndio ukweli.Hata hao tunaosema diaspora wengi wao ni watanzania wenye asili ya Asia,hatuwaoni wenzetu Wakenya,Waganda, Wanigeria nk.Sisi tumekalia eti kiswahili kiswahili. Viongozi wenyewe wanapeleka watoto wao kwenye shule nzuri zinazofundisha kwa kiingereza.Binafsi lugha ya Kiswahili siipendi kabisa,ni umaskini.
 
That's a good thing.... in so far as Tanzania has to offer not so good when it comes to exposure....

Jiulize nchi kama UK ingekuwa na good weather na mazingira mazuri yenye marashi ya mimea na maliasili unadhani kuna mtu angetoka kwenye kisiwa chao ?

Migration nyingi apart from economical nyingine ni political... niambie hizo nchi zinazoongoza takwambia kwanini ?

Anyway apart from uongozi mbovu Tanzania still has a lot to offer you can squeeze opportunities here and there.... Just turn a blind eye kwa upuuzi wa hapa na pale....
Kwa taarifa iliyotolewa, hata Botswana imeipita Tanzania. Utailinganisha Tanzania na Botswana katika suala zima la fursa?

Wasouth wametuzidi, kadhalika na Canada, Marekani, n.k. Huoni kwamba kiwango cha uelewa kinachochea pia watu kutoka nje ya mipaka ya nchi zao? Na kwa kadiri wanavyopata exposure huchochea pia maendeleo yao binafsi na za nchi zao?
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Si kweli
Passipoti haitegemei barua ya chuo. Nawaelewa Watanzania wengi ambao wamepata pasi bila hata ya ushahidi wa kusafiri
Weka hapa fomu ya maombi ili kuthibitisha
 
Sasa hv hata ukienda uhamiaji kutafuta passport unaulizwa unakwenda nje kufanya nini!?
Halafu ukiwaambia unaenda kutembea, watakuambia uwapelekee bank statement utadhani kama huna hela ya kutosha watakuongezea. Maswali mengine yanahalalisha kushuku uwezo wa kufikiri wa baadhi ya watu waliopewa dhamana.
 
Mchawi ni kiswahili kiswahili, naendaje Marekani au Ulaya.Kubishana masuala ya Simba na yanga kwa kiswahili kuna raha yake sheikh
Hiyo inaweza ikawa ni sababu mojawapo lakini si kubwa kama inayosababishwa na Serikali.

Passport! Kwa namna tu inavyobana passport, ni rahisi watu wengi kutokufikiria kutoka nje ya mipaka yao.

Serikali inahusika pakubwa sana na hayo.
 
Na nchi zinazoongoza ni zile zenye machafuko......
Middle east na ukanda wa Red sea, ndio zinaongoza hapo.
Unataka watanzania waondoke wanakimbia nini?
Laiti nusu ya Watanzania wangeenda kuishi ughaibuni alau kwa miaka mitatu tu kisha wakarejea nyumbani, kungewasaidia sana katika kuboresha uwezo wao wa kufikiri. Naamini, ingelikuwa hivyo, hata watawala wasingekuwa wepesi kuwadanganya kirahisi rahisi.
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.

Mbwa kala Mbwa
 
Back
Top Bottom