Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Wanavyouliza maswali sasa, utazani wao ndiyo wanahati miliki

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Passport ztu wanazibania

Hao dayaspora watatoka wapi.

Ukienda uhamiaji ukiwa mmatumbi utazungushwa hadi ukome

Lakini wakie da waarabu Koko na magabachori fasta sana wanapewa passport
 
Shangaa serikali Yako.

Inatia ugumu upatikanaji wa passport ila kwenye mikataba fasta inatia Saini bila hata kufikiria.

Passport tu yaweza ongeza Pato kwa serikali just imagine raia milioni 15 waziombe na kupewa so Hela ndefu hio.
 
Kukaa nje ni kipaji, lazima kichwa kiwe 'smart' , waswahili wanasema uwe na akili kubwa. Kutokana na hicho kigezo, ndio maana tupo huku tunashangilia timu zetu za jadi
 
Inamaanisha nini?
1. Huduma zimerahishwa sana siku hizi hivyo kila anayefika huhudumiwa haraka sana?

2. Wengi wamekata tamaa kufuatilia?

3. Kila kitu kinafanyikia mtandaoni?
Unajaza maombi mtandaoni lakini lazima uende Makao Makuu na kila kitu ili maombi yahakikiwe. Itakuwa passport kwa sasa siyo kila mtu anastahili. Lazima uwaridhishe Uhamiaji kwa nini unahitaji passport.
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Hahahahaha

Misingi ya Baba wa Taifa hiyo

enzi zake Hati zetu za kusafiria kupata tu ni mbinde Harare na pale page ya kwanza kabisa ziliorodheshwa Nchi ambazo hupaswi kwenda

pamoja na vikwazo vyote watu walivuka boda kutafuta maisha

vijana wa siku hizi laini sana hawajui ku force
 
Passport ztu wanazibania

Hao dayaspora watatoka wapi.

Ukienda uhamiaji ukiwa mmatumbi utazungushwa hadi ukome

Lakini wakie da waarabu Koko na magabachori fasta sana wanapewa passport
Hata Mmatumbi mwenye "kitambi" hawezi kusumbuliwa. Najua umeelewa!
 
Unajaza maombi mtandaoni lakini lazima uende Makao Makuu na kila kitu ili maombi yahakikiwe. Itakuwa passport kwa sasa siyo kila mtu anastahili. Lazima uwaridhishe Uhamiaji kwa nini unahitaji passport.
Kwani shida yao ni nini hasa? Watanzania ni wahalifu saana, hivyo Serikali yetu imeamua kufany majukumu ya Polisi wa dunia?

Hata nikichukua nikaenda kuifanya pambo la nyumbani kwangu, inawauma nini?

Hawaoni kuwa utoaji passport ni njia mojawapo ya kuiipatia Serikali fedha halali?
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu wnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Uongo ina maana Watanzania wengi wanapaspoti za nchi nyingine lakini wanaficha hawasubutu kusema ukweli kwa hiyo ukitaka kujua ukweli ni kuambia nchi zote duniani waweke wazi data za watu ambao ni Watanzania na wana uraia wa nchi nyingine tuwasiliane
 
Ningependekeza kila anayemaliza form six (21) aende nje hata kwa miezi sita, mwaka mmoja kwa kudhaminiwa na serikali / vyuo.

Ingesaidia sana kuongeza exposure. Miaka 16 kila Mtanzania apewe passport, NIDA, kitambulisho cha kupiga kura.
 
Siupendi huo msamiati ulioutumia lakini umefikisha ujumbe barabara.
Huyo kawa mstaarabu mimi anesema kuishi Tanzania ni kama kuishi utumwani na mnyapara ni mwenyekiti wa mtaa. Mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na raisi wa nchi kama mwendazake
 
Countries By Number Of Emigrants​

RankCountyNumber of Emigrants (Millions)
1India16.6
2Mexico13
3Russia10.6
4China10
5Bangladesh7.5
6Syria6.9
7Pakistan6
8Ukraine5.9
9Philippines5.7
10United Kingdom4.9

Hapo ukichukua UK ambayo hali ya hewa leaves a lot to be desired utaona a certain common denominator Pia population Density Bongo unaweza ukajinafasi mpaka ukamwagika....

Anyway Bongo advantages nyingi sana ambazo tunazipoteza bila kutengeneza a safety net ya wengi mwisho wa siku tunapoelekea huenda kukawa na machungu kupitiliza...

Tanzania is still a virgin we have a way to mold it to everyone advantage bila kufanya makosa waliyofanya wengine....

Tanzania Cradle of Human Kind.....
 
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
Ungeandika tu kichwa
Tanzania ni nchi ya Africa yenye Diaspora wachache.
Ondoa hilo neno "yaongoza" haviendani hata kidogo.
Kiswahili!!!
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Yani uchawi upo tusikatae tunalogana wenyewe kwa wenyewe
 
Back
Top Bottom